TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, October 29, 2014

WASANII WAASWA KUZINGATIA MUDA KWENYE KAZI ZAO

???????????????????????????????Kundi la Wakali Sisi likionesha vitu vyeo kwenye Jukwaa la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema wiki hii.
???????????????????????????????Kiongozi wa Kundi la Kudansi la Wakali Sisi lililoshinda katika Shindano la Dansi mia mia hivi karibuni Yasin Haji (Kulia) akiongea na wadau wa Sanaa waliohudhuria kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema wiki hii. Kushoto ni Afisa Sanaa kutoka BASATA, Ernest Biseko.
???????????????????????????????Mdau wa Sanaa kutoka Kikundi cha Sanaa za Majukwaani cha Binti Leo Lena Jackson akizungumza jambo kwenye Jukwaa la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema wiki hii. Kushoto kwake ni mkongwe wa Sanaa za Maonesho nchini, Baraka Mpelemba maarufu kwa jina la Jangala na Mwenyekiti wa Chama cha Sanaa za Maonesho Nkwama Bhallanga.
…………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
Wasanii nchini wameaswa kuzingatia muda wanapohitajika kufanya onesho au kazi yoyote ya jamii ili kuepuka kudharaulika na kuonekana watu wa hovyo na wasiyojali muda.
Rai hiyo imetolewa na Afisa Sanaa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ernest Biseko wakati akihitimisha Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki ambapo Kikundi cha Wakali Sisi kilichoshinda kwenye onesho la dansi mia mia kilitoa burudani.
“Hakuna kitu muhimu na cha msingi kwa msanii kama kuzingatia muda. Wasanii tumekuwa tukilalamikiwa sana kuchelewa kwenye maonesho au kwenye shughuli za kijamii ambazo zinatutaka tuwahi. Hii haipendezi” alisema Biseko.
Aliongeza kwamba, wadau wengi wa Sanaa hawafurahishwi hata kidogo wanapoona msanii anafika kwa kuchelewa kwenye shughuli hali ambayo imekuwa ikiwafanya wachukie na kuchukua maamuzi ya kufanya vurugu.
Mdau mwingine wa Sanaa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Sanaa za Maonesho nchini Nkwama Bhalanga alisema kuwa, wasanii wamekuwa wakidharaulika na kuonekana wa hovyo-hovyo kutokana na kutokuzingatia muda hali ambayo inawafanya washindwe hata kufanya vizuri jukwaani kutokana na muda mfupi wa maandalizi.
“Msanii lazima afike kwenye tukio walau saa moja kabla ya onesho ili azoee mazingira lakini pia afahamu wapi pa kubadilishia mavazi, kupumzika na kuoga baada ya onesho lake” alisisitiza Bhallanga.
Awali katika Jukwaa hilo, Kikundi cha kudansi cha Wakali Sisi ambacho wiki kadhaa zilizopita kiliibuka kidedea kwenye onesho la Dansi Miamia kilitoa burudani ya kuvutia kwa wadau wa Sanaa.

No comments:

Post a Comment