TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, October 29, 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

DSC00217
MTU MMOJA AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE MARA MOJA, UMRI KATI YA MIAKA 25 – 30, JINSI YA KIUME ALIUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KISHA KUCHOMWA MOTO NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BAADA YA KUKUTWA AKIWA AMEVUNJA NYUMBA YA HUSSEIN HASHIM (22) TANYBOY NA KUIBA TSHS 400,000/=.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 28.10.2014 MAJIRA YA SAA 04:00 USIKU HUKO MTAA WA VIWANDANI, KATA YA MWAKIBETE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA MHANGA BAADA YA KUMUONA MTUHUMIWA ALIPIGA KELELE ZA KUOMBA MSAADA NA WANANCHI KUJITOKEZA NA KUMSHAMBULIA MAREHEMU. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA UCHUNGUZI WA KITABIBU.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWENDESHA PIKIPIKI MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA VAVA ZAKARIA, UMRI KATI YA MIAKA 50 -55 ALIYEKUWA AKIENDESHA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.439 BDV AINA YA KING LION ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI ISIYOFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI WALA DEREVA WAKE.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 28.10.2014 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO MAENEO YA TAZARA, KATA YA IYUNGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUDUMA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO HILO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA MTUHUMIWA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] KUZITOA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment