TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, October 27, 2014

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU TETESI ZA KUWEPO MGONJWA ANAYEHISIWA KUWA NA UGONJWA WA EBOLA MKOANI KILIMANJARO

index
Utangulizi
Mnamo tarehe 22 Oktoba 2014, Wizara ilipokea taarifa kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ya kuwepo kwa mgonjwa aliyehisiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola. Mgonjwa huyu mwanaume ana umri wa miaka 37, na mkazi wa Dar es salaam (Kimara ) ambaye alikwenda Kilimanjaro tarehe 20 Oktoba 2014 katika kijiji cha Kirua kwa ajili ya kusalimia ndugu. Mgonjwa huyu alikuwa na dalili za homa kali ( 38.2 0c), maumivu ya Misuli, kuchoka na maumivu ya kichwa pamoja na maumivu ya koo na kupoteza hamu ya kula. Mgonjwa huyu anatibiwa katika Kituo cha Afya Shirimatunda, Kilimanjaro kuanzia tarehe 22.10.2014 ambako yupo hapo hadi sasa. Mgonjwa huyu kikazi ni “Land Surveyor” na hufanya kazi zake nchini na nje ya nchi ikiwemo nchi ya Senegali. Mnamo siku za karibuni alikwenda nchini Senegali kwa kazi za mkataba na kurejea nchini mwanzoni wa Oktoba 2014. Hata hivyo, mgonjwa huyu hakuwa na historia ya kusafiri kwenda nchi zilizoathirika na ugonjwa wa Ebola yaani Liberia, Guinea au Sierra Leone. Hatua zinazochukuliwa hadi sasa;
i. Sampuli ya damu ya mgonjwa kwa ajili ya uchunguzi wa Kimaabara ilifanyiwa uchunguzi na kuonekana kuwa na malaria. Matokeo ya awali dhidi ya magonjwa ya jamii ya ebola yakiwa ni pamoja na Dengue na Chikungunya yanaonyesha kuwa mgonjwa hakuwa na magonjwa haya. ii. Mgonjwa anaendelea kuhudumiwa katika kituo cha Afya cha Shirimatunda. iii. Wanafamilia wa karibu pia wamechunguzwa na kuonekana kuwa hawana dalili za ugonjwa wa Ebola.
Mwongozo wa utambuzi wa ugonjwa huu (Standard Case Definition) unaeleza kwamba ili mgonjwa aweze kuhisiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola anatakiwa akidhi vigezo vifuatavyo: i. Dalili za awali ni homa kali ya ghafla, kulegea mwili, maumivu ya misuli, kuumwa na kichwa, na kutokwa na vidonda kooni. Mara nyingi dalili hizi hufuatiwa na kutapika, kuharisha,kutokwa na vipele vya ngozi, kwa baadhi ya wagonjwa hutokwa na damu ndani na nje ya mwili ii. Awe amesafiri kwenda sehemu zilizothibitishwa kuwa na ugonjwa wa ebola ndani ya kipindi cha wiki 3 na hizi zikiwemo Guinea, Sierra Leone na Liberia. Aidha Shirika la Afya Duniani (WHO) limeshatangaza kutokuwepo kwa ugonjwa huu nchini Senegali na Nigreia na hivyo kuzitoa nchi hizi kwenye nchi hatarishi. iii. Dalili nyingine ni Kugusa majimaji kutoka kwa mgonjwa, maiti au mnyama anayehisiwa au kuthibitishwa kuwa na ugonjwa wa Ebola.
Hitimisho
Wizara inapenda kuwatoa hofu wananchi kuwa hadi sasa HAKUNA MGONJWA yeyote aliyethibitishwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola hapa nchini. Mgonjwa huyu kutoka Kilimanjaro hana ugonjwa wa Ebola bali anatibiwa kama mgonjwa wa MALARIA.
Adiha Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu ila wanatakiwa kuendelea kuchukua tahadhari za kuepuka kupata maambukizi ya ugonjwa huu ambazo:- o Kuepuka kugusa au kuingiwa na mate, damu, mkojo, jasho, kinyesi, machozi na majimaji mengine yanayotoka mwilini mwa mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola kupitia sehemu zenye michubuko au vidonda. o Kuepuka kushughulikia maiti ya mtu aliyekufa akiwa na dalili za ugonjwa wa Ebola; badala yake watoe taarifa kwa uongozi wa kituo cha huduma za Afya kwa ushauri. Wataalam watasimamia maziko ikiwa itatokea. o Wananchi waepuke mila na desturi zinazoweza kuchelewesha kupata huduma muhimu na kusababisha kuzidi kueneza kwa ugonjwa wa Ebola. o Kutoa taarifa mapema kwa viongozi wa Serikali na watoa huduma za Afya katika ngazi zote pale anapotokea mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola. o Kuwahi katika vituo vya kutolea huduma za Afya pale mtu anapohisiwa kuwa na dalili za ugonjwa huu Imetolewa na, Dkt. Donan Mmbando
KAIMU KATIBU MKUU 24 Oktoba, 2014

No comments:

Post a Comment