TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, October 31, 2014

Halmashauri zashauri kutenga maeneo ya uwekezaji.

unnamed
Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stela Manyanya akikagua bidhaa za wajasiliamali na waoneshashi kwenye viwanja vya maonesho ya SIDO yaliyojumuisha mikoa mitano ya Njombe,Mbeya,Rukwa ,Katavi na Kigoma sanjali na kongamano la uwekezaji kwa mikoa ya ukanda wa ziwa Tanganyika ambayo,Katavi Rukwa na Kigoma yanayoendelea kwenye uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga Mkoani Rukwa
……………………………………………………………..
Na Kibada Kibada –Rukwa. Halmashauri za Wilaya zimeshauriwa kutenga maeneo ya uzalishaji na kuendeleza maeneo maalum kwenye baadhi ya mipaka ili kuweza kupata sehemu bora za kuuzia bidhaa za wananchi zinazozalishwa katika maeneo hayo. Ushauri huo ulitolewa na waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdalah Kigoda katika Hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stela Manyanya wakati wa ufunguzi wa maonesho ya kumi na mbili ya Kanda ya Nyanda za Juu kusini ya wajasiliamali wadogo na kati Mjini Sumbawanga. Dkt Kigoda ameeleza kuwa bidhaa kwenye maeneo maalum na ya pamoja hususani ya mipakani kunasaidia katika kuleta ushindani na uboreshaji wa bidhaa. Akasema serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kulitumia soko la AGOA na masoko mengine ambayo Serikali imeridhia ambayo ni Afrika Mashariki AECna lile la kusini mwa Afrika SADC. Akashauri kufanya biashara halali na nchi jirani na kutunza kumbukumbu sahihi ya biashara zinazofanyika nchi za jirani na nchi ya Tanzaznia ili kuweza kuandaa sera mahususi za kuwasaidia. Waziri Kigoda Katika Hotuba yake akasisitiza kwa Halmashauri zote nchini kushiriki moja kwa moja katika Program ya SIDO ya ’Wilaya moja Bidhaa moja’ ambayo inasisitiza kuwa kila wilaya iwe inatambulika kwa uzalishaji wa bidhaa moja itakayotiliwa mkazo zaidi kuliko nyingine zilizopo kwenye wilaya husika. Hii ikiwa na maana kutoa kipaumbele kwenye upande wa kuendeleza bidhaa kwa kuipa huduma zaidi kwenye upande wa kupata mafunzo teknolojia,masoko na mikopo,lengo ikiwa ni kuongeza mapato na ajira kwa vijana katika maeneo husika. Pia Wafanya biashara, wajasiliamali na wasindikaji wa bidhaa wa Mikoa ya Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini na ule wa kanda ya ziwa Tanganyika wametakiwa kuwa wabunifu katika kubaini nini kinahitajika na mahali gani na lini wakati wa kuzalisha kadiri ya mahitaji ya soko. Mikoa mitano ya Kanda ya nyanda za juu na ukanda wa ziwa Tanganyika imejaliwa kuwa na rasilimali nyingi na hali ya hewa nzuri inayovutia na kufaa katika kuzalishaa bidhaa na kutoa huduma mbalimbali. Ambapo bidhaa zinazotokana na maliasili,mifugo,na mazao ya kilimo ambayo mikoa yote mitano ya kandahii imejaliwa ambayo ni Njombe Mbeya, Rukwa Katavi na Kigoma ambapo Serikali inajitahidi kuweka miundombinu ili kuwezesha huduma na bidhaa kusafiri kwa urahisi kutoka mikoa hiyo kwenda kwenye mikoa mingine na nchi jirani za Zambia,Jamhuri ya Kidemkrasi ya Kongo DRC,Burundi, Malawi na Rwanda, kwa kutumia barabara na majini Maziwa Tanganyika,Rukwa na Nyasa, Ambapo ili kutumia fursa hiyo wanatakiwa kuwa wabunifu katika kubaini mahitaji.

No comments:

Post a Comment