TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, October 31, 2014

BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI LACHOCHEA UBORA WA UTENGENEZAJI SAMANI NCHINI

images
KAMPUNI ya Furniture Centre (FCDL), na Shirikisho la Watengenezaji Samani Nchini (TAWOFE), wamesaini makubaliano (MoU) kuongeza ubora wa bidhaa za samani zinazotengenezwa nchini na kuzifanya zipate soko ndani na nje ya nchi. Makubaliano haya yamekamilika ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ikiwa ni mwendelezo wa Tathimini iliyofanywa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani, katika kuiwezesha sekta ya Samani nchini kupitia vikundi na makampuni ya ndani. Tathimini hiyo ya Baraza ya mwaka 2008, ilijikita katika kubaini mahitaji na changamoto zinazoikabili sekta ya samani hapa nchini. Baraza liliweza kuandaa warsha iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali na ambapo matokeo ya tathmini hiyo yaliwasilishwa. Wadau kutoka sekta ya umma na binafsi walishiriki katika mrejesho wa tathmini hiyo na wao pia kuchangia maoni zaidi kwa ajili ya kuiboresha. Washirika hao walisaini makubaliano hayo katika hafla iliyoshuhudiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji wa Uchumi na Uwekezaji), Dk Mary Nagu. Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dk Anacleti Kashuliza, alisema pamoja na kuwepo kwa fursa kubwa ya soko la samani hapa nchini bado ushiriki wa vikundi na makampuni ya ndani katika soko hilo ni mdogo sana kulinganisha na samani zinazoagizwa kutoka nje ya nchi. Alisema tunatoa wito kwa taasisi za Umma na Binafsi ziunge mkono jitihada hizi kwa kununua samani toka kwa watengenezaji samani wa ndani na ili kuwapa ushirikiano zaidi utakaowezesha kuimarisha sekta ya samani zitengenezwazo ndani ya nchi. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TAWOFE, Bw Fredrick Waibi, alielezea makubaliano kati ya FCDL na TAWOFE ni mkakati mzuri utaomjengea uwezo fundi seremala kuweza kutengeneza bidhaa zitakazoweza kukubalika kimataifa, kuongeza tija kazini na kupunguza umaskini kati ya mafundi seremala. Naye Mkurugenzi Mkuu wa FCDL, Bw Shafik Bhatia, alisema kama wadau muhimu wa samani nchini wameona umuhimu na wanajivunia kushirikiana na Tawofe katika kuboresha huduma za samani nchini .

No comments:

Post a Comment