TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, October 31, 2014

MISS TANZANIA 2014 SITTI MTEMVU KUVULIWA TAJI RASMI


sitti_mtemvu_miss_tanzania_crown_taji
WAKATI serikali kupita Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), ikisema itakifuta cheti cha kuzaliwa cha Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu,  taarifa zinasema kwamba hawezi tena kuendelea na taji hilo   imethibitisha kwamba uamuzi umekwisha kufanyika wa kumvua Sitti taji hilo alilovikwa katika mazingira tata, uamuzi unaotarajiwa kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa. Hata hivyo, haijafahamika kama hatua hiyo itachukuliwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) ama Sitti mwenyewe baada ya kubainika kwamba taji hilo linazidi kuiweka pabaya familia ya Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, ambaye ni baba yake.

Uchunguzi wetu umebaini kwamba hata hatua ya awali ya kuwania taji hilo ilichukuliwa na Sitti na baadhi ya wanafamilia bila kushirikishwa kwa Mbunge Mtemvu, jambo ambalo lilimsononesha awali katika ushiriki wa Miss Temeke, na kwamba Mbunge Mtemvu amekerwa na hali inayoendelea ikiwa ni pamoja na kuwapo utata wa cheti cha kuzaliwa cha mwanae Sitti, pamoja na kuwa anawajibika kisheria kwa anayoyafanya kutokana na kufikia umri wa zaidi ya miaka 18. Kwa upande wake, RITA imesema inaweza kukifuta cheti kilichotolewa Temeke na kuchukua hatua stahiki ikibainika kwamba alitoa taarifa za uongo wakati wa kuwasilisha maombi ya kukupata cheti hicho. Mtendaji Mkuu wa RITA, Philip Saliboko, leo Alhamisi Oktoba 31, 2014 amesema kwamba kwa sasa wanakamilisha uchunguzi wa kina kuhusiana na cheti hicho, baada ya kuibuka utata wa taarifa za kuwapo vyeti viwili vinavyotofautiana mwaka wa kuzaliwa. Baada ya kuibuka kwa utata huo, RITA ilianza upekuzi maalumu wa nyaraka alizowasilisha Sitti katika ofisi za RITA Temeke ili kubaini kwanza uhalali wa cheti, kabla ya kutafuta ukweli wa taarifa zilizowasilishwa chini ya kiapo. Kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Vizazi na Vifo (Sura ya 108 Toleo la 2002), ni kosa la jinai kutoa taarifa za uongo kwa Msajili na pia ni kosa la jinai kughushi. Imeelezwa kwamba sababu kubwa ya kuchelewa kwa uchunguzi huo ni kutokana na uchunguzi huo kuhusisha nyaraka zote za watoto waliozaliwa Temeke katika miaka ya 1980 hadi 1992 kipindi ambacho Sitti anadai alizaliwa.
http://www.fikrapevu.com/wp-content/uploads/2014/10/Cheti.jpg
Katika mashindano ya Miss Temeke yaliyofanyika Jumamosi Agosti 23, 2014, Sitti aliyeibuka mshindi alidai amezaliwa mwaka 1991 kabla ya kupata cheti kilichodaiwa kutolewa na RITA Septemba 9, 2014 kikionyesha kazaliwa nyumbani (si hospitali), Temeke Mei 31, 1991.
passport_sitti_abbas_mtemvu
Hati ya kusafiria ya Sitti inaonyesha alizaliwa Mei 31, 1989 na si 1991 kama alivyodai. Hati hiyo namba AB202696 ilitolewa Dar es Salaam,  Februari 15, 2007. Hati hiyo ni ya pili baada ya hati ya mwanzo kwisha muda wake.

No comments:

Post a Comment