TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, October 31, 2014

HABARI ZILIZOTAWALA KWENYE VYOMBO MBALI MBALI VYA HABARI SIKU YA ALHAMIS HIZI HAPA: Rais Kikwete afungua Maadhimisho ya miaka 10 ya Tume ya Utumishi wa Umma,Viongozi wa Msondo wamtembelea Rais Kikwete Ikulu,PINDA AZUNGUMZA NA WATANZANIA WAISHIO OMAN,Tigo na Facebook kutoa huduma za internet bure kupitia Internet.org,KAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA YAENDELEA NA UKAGUZI KATIKA MIGODI,TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI, KAMATI YA BUNGE YATEMBELEA BWAWA LA KUZALISHA UMEME MEROWE, Serikali yashauriwa kuwekeza katika sekta ya Filamu, PSPF YAKABIDHI MABATI 300 KWA WILAYA ZA KILOLO NA MUFINDI, HABARI KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF), WANAUME WATAKIWA KUSHIRIKI SAWA NA WANAWAKE KATIKA MASUALA YA AFYA YA UZAZI. RAIS MALINZI ATUMA RAMBIRAMBI MSIBA WA SATA, MEYIWA, Ofisi ya Taifa ya Takwimu yazindua ripoti ya mapato na matumizi ya kaya. Rais Dk.Shein atembelea Benki ya Damu Salama, SHIWATA WAGAWA MASHAMBA KWA WANACHAMA WAKE, Taarifa ya Kifo Cha Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse, SERIKALI YAAHIDI KUTAFUTA UFUMBUZI SUALA UHABA WA MAGHALA.,

Rais Kikwete afungua Maadhimisho ya miaka 10 ya Tume ya Utumishi wa Umma

 D92A1608Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya miaka 10 ya Tume ya tutmishi wa Umma lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam . D92A1654Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya miaka 10 ya Tume ya tutmishi wa Umma lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam . D92A1782Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Maadhimiso ya miaka 10 ya tume ya Umma lililofanyika jijini Dar es Salaam.D92A1837Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa tatu kushoto) pamoja na makatibu wakuu Kiongozi wastaafu Matern Lumbanga(kulia) na Philemon Luhanjo(kushoto)(picha na Freddy Maro)
========================================================================

Viongozi wa Msondo wamtembelea Rais Kikwete Ikulu


D92A1998Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na viongozi wa Bendi ya Msondo ngoma ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Viongozi hao walimtembelea Rais Kikwete ikulu  na kufanya naye mazungumzo(picha na Freddy Maro). D92A1988Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha ya pamoja  na viongozi wa Bendi ya Msondo ngoma ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Viongozi hao walimtembelea Rais Kikwete ikulu  na kufanya naye mazungumzo(picha na Freddy Maro).
===================================================================

PINDA AZUNGUMZA NA WATANZANIA WAISHIO OMAN

DSC03728Waziri Mkuu, Mizengo pinda akizunguma na Watanzania waishio nchini Oman akihitimisha ziara yake nchini humo Oktoba 29, 2014. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maalim Mahadhi nakushoto ni Balozi wa  Tanzania nchini Oman, Ali Ahmed Saleh. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A8342 Baadhi ya watanzania waishio Oman wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipowahutubia kwenye hoteli ya Al Bustan mjini Muscut Oktoba 29, 2014. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu) PG4A8357 Baadhi ya watanzania waishio Oman wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipowahutubia kwenye hoteli ya Al Bustan mjini Muscut Oktoba 29, 2014. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu) PG4A8365 Baadhi ya watanzania waishio Oman wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipowahutubia kwenye hoteli ya Al Bustan mjini Muscut Oktoba 29, 2014. 
(Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu) PG4A8371 Waziri Mkuu, Mizengo pinda akizunguma na Watanzania waishio nchini Oman akihitimisha ziara yake nchini humo Oktoba 29, 2014.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
===============================================================

Tigo na Facebook kutoa huduma za internet bure kupitia Internet.org

2
- Inatarajia kuongeza idadi ya watumiaji wa intenet nchini
- Upatikanaji wa intanet kupitia simu za ‘smartphone’ za bei nafuu kutoka Tigo
Tigo jana imetangaza kwamba watashirikiana na kampuni ya mtandao wa kijamii Facebook kuwapatia mamilioni ya Watanzania huduma ya intanet kwa bei nafuu kupitia ‘application’ maalum ya Internet.org.
Tigo pia inatoa fursa ya wateja kununua na kumiliki simu za kisasa ‘smartphones’ kwa bei nafuu, kuwapatia huduma bora ya intanet na kutoa huduma ya bure kabisa kwa tovuti zinazohusiana na elimu, afya, habari na mitandao ya kijamii kupitia Internet.org.
App ya Internet.org itaanza kutumika kuanzia 29 Oktoba na itawapatia wateja wa Tigo fursa ya kutumia tovuti na apps kama: AccuWeather; BabyCenter & MAMA; BBC News & BBC Swahili; BrighterMonday; The Citizen; Facebook; Facts for Life; The Girl Effect; Messenger; Mwananchi; Mwanaspoti; OLX; Shule Direct; SuperSport; Tanzania Today and Wikipedia.
Akizungumzia kuhusu uzinduzi wa huduma hizo leo, Mkuu wa Idara ya Data na Vifaa vinavyotumia Intanet, David Zacharia, alisema, “Kupitia ushirikiano huu na Facebook tunadhamiria kuongeza wigo wa matumizi ya kidijitali nchini kwa kuwahamasisha Watanzania wengi zaidi kuingia mtandaoni.”
Zacharia aliendelea kusema kwamba ushirikiano huo kati ya Tigo na Facebook itazidi kuendeleza matumizi ya intanet nchini lakini pia itasaidia kufungua milango mipya ya fursa za kiuchumi na kijamii kwa walio katika sekta mbali mbali za elimu, teknolojia, sanaa na biashara.
Ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaeleza kwamba watumiaji wa intanet nchini Tanzania imeongezeka kutoka milioni 7.5 mwaka 2012 mpaka milioni 9.3 mwezi wa Juni 2014 ambayo ni sawa sawa na ongezeko la asilimia 18.
Tigo, kupitia mmiliki wake Millicom, tayari wana ushirikiano na Facebook nchini Tanzania na Paraguay ambayo inawapatia wateja wake matumizi ya bure kabisa katika mtandao huo wa kijamii.
“Leo tunapanua ushirikiano wetu na Tigo nchini Tanzania kutoka katika kutoa huduma za bure kupitia mtandao wetu wa Facebook na kujumuisha huduma za kupata taarifa muhimu kwenye sekta ya afya, elimu, mawasiliano, uchumi, ajira na habari za kitaifa. Kwa kuwapatia Watanzania teknolojia na huduma hizo kwa gharama nafuu tunaamini ya kwamba tunaweza tukaharakisha mchakato wa kuwaunganisha kila mtu katika ulimwengu wa intanet na dijitali,” alisema Meneja Bidhaa wa Internet.org kutoka Facebook, Andrew Bocking.
Wateja wa Tigo nchini wanaweza wakapata app ya Internet.org kupitia huduma ya Google Play Store, kwa kutembelea www.internet.org kupitia simu zao za mkononi, kupitia ‘Tigo Portal’ na pia kupitia ‘bookmark’ iliyopo katika huduma ya kuperuzi ya Opera Mini. Huduma hii inaweza ikatumika kupitia simu za kisasa ‘smartphones’ au simu za kawaida pia.
Internet.org ni mpango maalum uliobuniwa na Facebook yenye lengo la kuwapatia huduma za intanet yenye gharama nafuu kwa theluti tatu ya watu duniani ambao bado hawajaunganishwa na intanet ili kuweza kuwapatia fursa zile zile ambazo theluthi ya watu duniani iliyobaki wanaendelea kupata.    
App ya Internet.org inafanya mtandao wa intanet kuwafikia watu wengi zaidi kupitia kundi la huduma za bure ambazo zinawezesha watu kuperuzi taarifa na tovuti mbali mbali zenye msaada kwao bila kuingia gharama yeyote.
=================================================================

KAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA YAENDELEA NA UKAGUZI KATIKA MIGODI

Kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Mazingira imeendelea na ukaguzi katika Migodi ya dhahabu kufahamu utekelezaji wa Sheri a ya Mazingira. Katika Mgodi wa Bulyanhulu Kamati iliangalia jinsi maji yenye kemikali yanavyohifadhiwa na udhibiti wa taka za plastiki mgodini hapo. Migodi iliyotembelewa mpaka sasa ni Mgodi wa North Mara, Geita na Bulyanhulu. Hii leo Kamati hii itaendelea na ziara yake katika mgodi wa Buzwagi.20141029_131450Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kutoka kulia) akitoa ufafanuzi wa kisheria mbele ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira. Kamati hiyo iko katika ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa Sheria ya Mazingira katika Migodi. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Mh. James Lembeli (wa tatu kulia), Mh. John Mnyika na Mh. Henry Shekifu wajumbe wa Kamati hiyo. Wa kwanza (kushoto) ni Bw. Peter Burger, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu 20141029_160529Pichani ni taka za plastiki zilizohifadhiwa vizuri kwa ajili ya urejelezwaji katika Mgodi wa Bulyanhulu.
20141029_162046Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Mgodi wa Bulyanhulu wakati wa ukaguzi katika Mgodi huo kuona utelekezaji wa Sheria ya Mazingira.
20141029_164357Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Mgodi wa Bulyanhulu mara baada ya ukaguzi katika Mgodi huo kuona utelekezaji wa Sheria ya Mazingira.
==================================================================

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

DSC00217
MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA YASSINI HEZRON (14) MKAZI WA KIWIRA ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.235 AFB AINA YA M/CANTER LILILOKUWA LIMEBEBA MATOFALI LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE FREDY MPONDO KUSHINDWA KUPANDA MLIMA NA KISHA KURUDI NYUMA NA KUANGUSHA MATOFALI NA KUSABABISHA KIFO KWA TINGO HUYO.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 29.10.2014 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO MAENEO YA NEW LAND BAR, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA TUKUYU/KYELA. CHANZO CHA AJALI NI GARI HILO KUSHINDWA KUPANDA MLIMA NA KURUDI NYUMA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO HILO NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] KUZITOA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. OTHAZ ANGOLILE (18) 2. SAMSON MWANGOMILE (46) 3. FORD SAMSON (20) NA 4. BARAKA JOSEPH (23) WOTE WAKAZI WA AIRPORT JIJINI MBEYA WAKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI AINA YA BOSS NA RIDDER PAKETI 108.
WATUHUMIWA WALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 29.10.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO KATIKA MTAA WA AIRPORT, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WAUZAJI WA POMBE HIZO NA TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA/KUUZA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
===========================================================

KAMATI YA BUNGE YATEMBELEA BWAWA LA KUZALISHA UMEME MEROWE

IMG_0078Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Prof. Peter Msolla wakiwa kwenye kiwanda cha nyama ya kuku wakiangalia utendaji na uendeshaji wake.
IMG_0146Mjumbe wa Kamati, Prof. David Mwakyusa akiangalia moja ya kifaa cha kisasa katika Hospitali ya Mji wa Merowe.
IMG_0179Ujumbe wa Tanzania ukisikiliza taarifa ya Mji wa Merowe kutoka kwa Inj. Mohamed Elsheikh. IMG_0245Mtambo wa kuzalisha umeme katika Bwawa la Merowe IMG_0281Ujumbe wa Tanzania, viongozi wa Sudan na wataalam mbalimbali wa Bwawa la kuzalisha umeme la Merowe wakiwa katika picha ya pamoja katika bwawa hilo.
IMG_0300Ndani ya jengo la bwawa la kuzalisha umeme la Merowe.
……………………………………………
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imetembelea Bwawa la Kuzalisha Umeme la Merowe katika Mji wa Merowe na kujionea namna ya wenyeji wanavyotumia maji ya Mto Nile kwa kuzalisha umeme wa kutosha kwa ajili ya mji huo na nchi nzima ya Sudan.
Mradi wa Bwawa la Merowe ni mkubwa katika nchi ya Sudan na mbali na kuzalisha umeme, pia unatumika kwa shughuli za kilimo cha umwagiliaji ambacho kwa aslimia mia kinategemea Mto Nile.
Aidha, mradi wa bwawa hilo pia umechangia kuleta maendeleo makubwa kiuchumi kwa kuwezesha kujengwa kwa uwanja bora wa ndege wa kisasa, hospitali bora ya kisasa na kiwanda kikubwa cha nyama ya kuku katika mji wa Merowe.
Hivyo, kuonyesha jinsi gani nchi ya Sudan inavyotumia fursa ya maji ya Mto Nile vizuri katika kuleta maendeleo ya Sekta zote nchini mwao.
Hii ni muendelezo wa ziara ya siku nne nchini humo kwa kamati hiyo, katika kujifunza namna ya kutumia vizuri rasilimali ya maji ya Mto Nile katika kukuza maendeleo ya nchi.
===================================================================

Serikali yashauriwa kuwekeza katika sekta ya Filamu

unnamed Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akiowaonyesha mabango ya filamu za Tanzania wageni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Kenya (hawapo pichani) walipotembelea ofisi za Bodi hiyo ili kujifunza namna ya Uendeshwaji wa Bodi ya Filamu jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw. Silyvester Sengerema.
unnamed1Kutoka kushoto ni Afisa Mult Media kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Kenya (CA) Bi. Jacquline Kinyanjui, Afisa Mult Media kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Kenya Bi. Mercy Tepla na Afisa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. George Charles wakisikiliza maelezo kutoka kwa uongozi wa Bodi ya Filamu Tanzania walipotembelea ofisi za Bodi hiyo jana jijini Dar es Salaam.
unnamed2Ujumbe kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Kenya wakiwa katika kikao cha pamoja na Watendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania jana jijini Dar es Salaam.
unnamed3Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo(wa pili kutoka kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wageni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Kenya walipotembelea ofisi za Bodi hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Picha na Frank Shija, WHVUM
==========================================================

PSPF YAKABIDHI MABATI 300 KWA WILAYA ZA KILOLO NA MUFINDI

unnamed
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Gerald Guninita akipokea msaada wa mabati 200 kutoka kwa mwakilishi wa PSPF kutoka makao makuu Amelia Rwemamu kwa ajili ya ujenzi wa maabara za sayansi katika shule za sekondari wilayani humo, Makabidhiano yalifanyika juzi katika ofisi za wilaya ya Kilolo(picha na Denis Mlowe)
……………………………………………………………………
Na Denis Mlowe,Mufindi
 
KATIKA kutekeleza maagizo ya Rais Jakaya Kikwete kila shule iwe na maabara tatu ifikapo Novemba mwaka huu Mfuko wa Pensheni ya Watumishi wa Umma (PSPSF) umetoa msaada wa mabati 300 yenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni sita katika wilaya za Kilolo na Mufindi, mkoani Iringa kufanikisha ujenzi wa maabara hizo na hosteli kwa chuo cha Ualimu Mufindi.
Wakati wilaya ya Kilolo imepata bati 200 zitakazotumika kusaidia kukamilisha ujenzi wa maabara unaoendelea  katika shule zake za sekondari, Chuo cha Ualimu Mufundi(MUTCO) kilichopo mjini Mafinga wilayani Mufindi kimepata bati 100 ikiwa ni kutumiza ahadi iliyotolewa na Meneja wa Sheria wa PSPF Abrahamu Siyovelwa aliyotoa May 27 katika mahafali ya chuo hicho.
 
Akikabidhi msaada huo kwa mkuu wa wilaya ya Mufindi Monica Kalalu juzi katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Mufindi(MUTCO) Afisa Mfawidhi wa PSPF mkoa wa Iringa Baraka Jumanne alisema lengo la msaada huo ni sehemu ya mpango wao katika kusaidia sekta ya elimu nchini na kutekeleza maombi yaliyoombwa na viongozi wa wilaya hizo katika kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete kila shule ya sekondari iwe na maabara ifikapo Novemba mwaka huu.
“PSPF ni shirika la mfuko wa pensheni hivyo faida lazima iifikie jamii hasa katika suala la elimu ya za sekondari na msingi hivyo tumeamua kuwapatia mabati 100 chuo cha Mufindi na wilaya ya Kilolo mabati 200 kutekeleza maombi yao kwa shirika la PSPF kusaidia ujenzi wa maabara na ujenzi wa hostel kwa chuo cha Mutco hivyo leo tunawakabidhi madawati haya mia tatu kwa lengo la kutekeleza ahadi ya shirika.” Alisema Jumanne.

Aidha Jumanne alitoa wito kwa viongozi kuwashawishi wafanyakazi Kilolo  na wanafunzi wa chuo cha Ualimu Mufindi kujiunga mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma wa PSPF kwa huduma bora na mafao bora yakiwemo mafao ya uzeeni,ulemavu,mirathi,mafao ya rambirambi za mazishi, malipo ya wategemezi na malipo ya penshini ya kila mwezi.
Alitoa faida ya kujiunga na PSPF kwa kuwa kuna baadhi ya mafao mbalimbali yanayotolewa na mfuko  huo yanalenga kuwawezesha watumishi kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utumishi wao kabla na baada ya kustaafu
 
Aliongeza kuwa PSPF ina mpango imeweka mahususi wa kuhakikisha unaboresha maisha wa wanachama wake wakiwemo wasio wafanyakazi kwa kuweka akiba isiyo ya hiyari itakayowawezasha kufaidika kwa faida ya maisha yao.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mufindi Monica Kalalu alilishukuru shirika la PSPF kwa msaada huo na kutoa wito kwa wanafunzi na walimu na kuwataka wadau wengine wajitokeze kuisaidia sekta ya elimu hususani ujenzi wa maabara ambao unaendelea nchi nzima kwa sasa,
 
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Gerald Guninita alisema kuwa msaada huo utazisaidia shule za sekondari za wilaya ya Kilolo katika kukamilisha ujenzi wa maabara na kuwataka pspf wasiishie hapo katika kutoa msaada zaidi katika sekta ya elimu.
Na Amelia Rweyimamu ambaye ni Muwakilishi wa PSPF makao makuu Dar es salaam, akizungumza wakati wa kukabidhi bati hizo alisema kuwa PSPF inatambua umuhimu wa kuwepo kwa maabara hapa nchini hivyo ofisi yake imeona vyema kushiri katika ujenzi huo kwa kutoa bati hizo.
 
Rweyimamu alisema PSPF inatoa mafao mbalimbali ikiwa ni pamoja na fao la uzeeni, fao la ulemavu, fao la kifo, fao la mazishi, fao la wategemezi lisilo na kikomo, fao la kujitoa, fao la uzee, fao la kufukuzwa kazi, na fao la ujasiriamali.
Aidha aliongeza kuwa PSPF inatoa fao la elimu ambapo mfuko hudhamini mikopo katika bodi ya mikopo ya wanafunzi, lengo kubwa ikiwa ni kujenga uwezo wa kuhudumia wanafunzi wengi katika taaluma mbalimbali ikiwemo pia taaluma ya sayansi, Teknolojia na Afya.
=================================================================

HABARI KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

index17
TFF YAOMBA WADAU WABUNI JEZI MPYA YA TIMU ZA TAIFA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linakaribisha wabunifu, kubuni mwonekano wa jezi mpya za timu ya Taifa kwa mechi za nyumbani na ugenini. Ubunifu ni lazima uzingatie rangi za bendera ya Taifa.
  Mshindi wa jezi ya nyumbani atapata sh. 1,000,000 (milioni moja), na mshindi wa jezi ya ugenini atapata pia sh. 1,000,000 (milioni moja).
Ubunifu utumwe kwenye anwani ya barua pepe: info@tff.or.tz au uwasilishwe kwa CD au flash zikiwa katika mfumo wa PDF katika ofisi za TFF zilizopo ghorofa ya tatu katika Jengo la PPF Tower, Mtaa wa Ohio na Garden Avenue. Mwisho wa kupokea designs ni Novemba 15, 2014.
Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba; 0713 210242 au 0714 634838.
SDL KUANZA KUTIMUA VUMBI NOVEMBA 22
Michuano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) inayoshirikisha timu 24 zitakazocheza katika makundi manne ya timu sita sita kwa mtindo wa nyumbani na ugenini itaanza kutimua vumbi Novemba 22 mwaka huu.
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyoketi jijini Dar es Salaam jana (Oktoba 29 mwaka huu) chini ya Mwenyekiti wake Geofrey Nyange ilipitia maandalizi maandalizi ya ligi hiyo ikiwemo mwongozo wake (roadmap).
Kwa mujibu wa mwongozo huo, usajili wa wachezaji utamalizika Oktoba 31 mwaka huu. Kipindi cha pingamizi ni kuanzia Novemba 1 hadi 7 mwaka huu wakati Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji inatarajia kukutana Novemba 11 mwaka huu kwa ajili ya kupitisha usajili.
Pia Kamati ya Mashindano imepitisha viwanja vya timu zote, isipokuwa uwanja wa timu ya Mpanda United ya Katavi na ule wa Town Small Boys ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Uwanja wa Town Small Boys haukupitishwa kwa vile hauna uzio wa kudumu ( wa chuma) wa kutenganisha wachezaji na washabiki, na pia ufikaji wa timu Tunduru ni mgumu kutokana na ubovu wa barabara ikizingatiwa kuwa ligi hiyo itachezwa hadi kipindi cha Masika.
Kwa upande wa uwanja wa Mpanda United, umekataliwa kwa vile hauna vigezo vya msingi vinavyotakiwa ikiwemo vyumba vya kubadilishia nguo, kutokuwa na nyasi na uzio wa kudumu kutenganisha wachezaji na washabiki.
===========================================================

WANAUME WATAKIWA KUSHIRIKI SAWA NA WANAWAKE KATIKA MASUALA YA AFYA YA UZAZI.

index
Na Magreth Kinabo_MAELEZO_Dar es salaam
Wanaume wametakiwa kushiriki katika wa masuala ya afya ya uzazi ili waweze kusaidia katika ukoaji wa maisha ya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinisia na watoto Dkt. Pindi Chana wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Uzazi na Malezi bora Tanzania(UMATI).
Kauli mbiu ya mkutano huo ni miaka 55 ya kutoa huduma bora za uzazi wa mpango Tanzania ni tumia uzazi wa mpango , okoa maisha.
Amesema katika kusherekea maika 55 ya UMATI ni vema wadau wote washirikiane na wataalamu wa sekta ya afya katika kutekeleza kazi zinatokana na hali halisi ya mahitaji ya huduma ya afya ya uzazi kwa jamii husasani kwa wanawake, watoto na vijana ili kuokoa maisha ya wananchi.
Dkt. Chana amesema kuwa takwimu kwa Tanzania zinazonyesha kuwa vifo vinavyotokana na uzazi ni takribani 454 kwa kila vizazi hai 100,000 .
Ameongeza kuwa idadi hiyo inaweza kupungua iwapo huduma bora, taarifa sahihi na elimu kuhusu afya ya uzazi itawafikia Watanzania wengi ili liwe taifa lenye uelewa mkubwa kuhusu masuala ya uzazi.
Dkt. Chana ametoa wito kutumia njia ya makundi  rika  kama mabaraza ya watoto ,vilabu vya watoto na vyama vya FEMATALK ili kufikisha ujumbe kwa ajili ya kuokoa maisha ya mama na mtoto.
Amewataka wajumbe wa mkutano huo kuendelea na juhudi za kuhamasisha jamii ili kuondoa vitendo vya ubaguzi wa kijinsia kama vile ndoa za utotoni na wanaume kutoshiriki katika masuala ya afya ya uzazi sawa na wanawake.
Dkt.Chana ametoa wito kwa UMATI kuendelea na juhudi hizo katika harakati za kumukomboa mtoto wa kike.
================================================================

RAIS MALINZI ATUMA RAMBIRAMBI MSIBA WA SATA, MEYIWA

DSC_5014
 Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewatumia salamu za rambirambi vyama vya mpira wa miguu vya Zambia (FAZ) na Afrika Kusini (SAFA) kutokana na vifo vya Rais Michael Sata na kipa wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini, Senzo Meyiwa.
Ametuma salamu hizo kwa Rais wa FAZ, Kalusha Bwalya na Rais wa SAFA, Danny Jordan na kuongeza kuwa amepokea kwa masikitiko taarifa za vifo vya ghafla vya Rais Sata na kipa huyo wa Bafana Bafanavilivyotokea wiki hii.
Rais Malinzi amesema kuwa misiba hiyo si pigo kwa Zambia na Afrika Kusini pekee bali Afrika kwa ujumla kwa vile walikuwa na mchango mkubwa kwa ustawi wa mchezo wa mpira wa miguu.
Amewaomba Rais Jordan na Rais Bwalya kutuma salamu zake za rambirambi kwa familia ya Sata, na familia ya Meyiwa, na kuzitaka kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha misiba hiyo mizito kwao.
Rais Sata (77) alifariki dunia juzi kwenye Hospitali ya King Edward VII nchini Uingereza alipkuwa kwenye matibabu, wakati kipa Meyiwa aliuawa kwa kupigwa risasi Jumapili mjini Vosloorus.
===================================================================

Ofisi ya Taifa ya Takwimu yazindua ripoti ya mapato na matumizi ya kaya.

unnamed
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum
………………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum jana jijini Dar es salaam alipokuwa akizindua chapisho la la utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi wa mwaka 2011/2012 ambalo linaonesha mwenendo wa hali ya uchumi nchini.
Waziri Saada amesema kuwa utafiti unaonesha kuwa kwa kila watu 100 waliokuwa na uwezo wa kufanya kazi mwaka 2011/2012, watu 75 walijishughulisha na kilimo na uvuvi.
“Chapisho ninalolizindua linatoa taarifa muhimu kwa Serikali katika kutathmini na kurekebisha baadhi ya sera na mipango ya maendeleo ya kukuza uchumi na kupunguza umaskini kwa wananchi” alisema Waziri Saada.
Hata hivyo, Waziri Saada ameongeza kuwa matumizi ya zana duni za kilimo bado ni changamoto kubwa inayoendelea kulikabili taifa.
Utafiti unaonesha kwa asilimia 96.5 ya kaya zinazojishughulisha na kilimo bado zinatumia jembe la mkono na asilimia 0.1 wanatumia zana za kisasa za kilimo likiwemo jembe la plau na trekta.
Kwa upande wa washirika wa maendeleo, mwakilishi wa Benki ya  Dunia nchini Philippe Dongier amesema kuwa wapo begakwa began a Serikali ya Tanzania katika  kupunguza umaskini kwa wananchi ili waweze kupata mahitaji yao ya muhimu katika maisha ya kila siku.
Naye Balozi Finland nchini Bi. Sinikka Antila akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washirika wengine  wa maendeleo waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi amesema kuwa wataendelea kushirikiana na Tanzania kutokana na mahusiano mzuri yaliyopo baina ya  washirika hao wa maendeleo.
Chapisho la Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa mwaka 2011/2012 limeandaliwa naSerikali kwa ushirikiano wa washirika mbalimbali wa maendeleo nchini wakiwemo Benki ya Dunia, Umoja wa Nchi za Ulaya (EU), Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID), Taasisi za Umoja wa Mataifa ikiwemo UNDP, UNFPA na UNICEF.
==============================================================

Rais Dk.Shein atembelea Benki ya Damu Salama

IMG_9977 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akizungumza na wafanyakazi wa Kituo cha Damu Salama kiliopo Sebleni Nyumba za Wazee Mjini Zanzibar leo alipofanya ziara fupi.[Picha na Ikulu.] IMG_9831Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Meneja wa Kituo cha Damu Salama Dk.Mwanaheri Mahmoud Ahmed alipotembelea katika Ofisi za Kituo hicho Sebleni Nyumba za Wazee Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu.] IMG_9884Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifutana na Meneja wa  Kituo cha Damu Salama Dk.Mwanaheri Mahmoud Ahmed (kulia) katika chumba maalum alipotembelea katika Ofisi za Kituo hicho Sebleni Nyumba za Wazee Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu.] IMG_9893 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiangalia Damu Salama zilizohifadhiwa katika mashine maalum akiwa na Aaza Humud katika chumba maalum alipotembelea katika Ofisi za Kituo hicho Sebleni Nyumba za Wazee Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu.] IMG_9927 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifutana na Meneja wa  Kituo cha Damu Salama Dk.Mwanaheri Mahmoud Ahmed (kushoto) baada kutembelea chuma maalkum cha kuhifadhi Damu Salama iliyochangiwa na wananchi Mbali mbali  huko Sebleni Nyumba za Wazee Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu.] IMG_9956Afisa Mhamasishaji wa Kituo cha Damu Salama Omar Said Omar (kulia) akitoa mchango wake wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipozungumza na wafanyakazi  wa kituo hicho alipofanya ziara maalum ya kutembelea kuangalia maendeleo ya utendaji kazi Sebleni Nyumba za Wazee Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu.]
=============================================================

SHIWATA WAGAWA MASHAMBA KWA WANACHAMA WAKE

Msanii Maarufu nchini Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’ wa kwanza kulia akimsikiliza mwenyekita wa SHIWATA Cassim Taalib wa pili kushoto  walipokuwa wakigawa mashamba kwa ajili ya wanachama wao
Watakaohamia kijiji cha wasanii kupewa bustani bure Na Mwandishi Wetu
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umetoa bure kwa wanachama wake wanaomiliki nyumba katika kijiji chao cha Mwanzega Mkuranga ya eneo la kulima bustani.
Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa watakaonufanika na ofa hiyo ni wale watakaohamia katika nyumba zao kabla ya Desemba mwaka huu ambapo mtandao unaadhimisha miaka 10 kutoka uanzishwe.
Alisema wanachama hao wanatakiwa kufika SHIWATA kugaiwa maeneo hayo ambayo yatalimwa mazao ya muda mfupi (ambayo si ya kudumu) kama vile pilipili,mahindi, matango, pilipili hoho, mananasi, mbogamboga, matikiti maji ambayo hustawi kwa wingi maeneo hayo.
Katika hatua nyingine SHIWATA imeamua kusafisha shamba la ekari 200 ambazo zimekwisha gaiwa kwa wanachama ambao walijitokeza kulima katika shamba hilo la 500 zinazomilikiwa na mtandao huo kwa ajili ya maandalizi ya kilimo kwanza msimu huu katika kijiji cha Ngarambe, Mkuranga.
Mwenyekiti Taalib alisema SHIWATA imeingia mkataba na Kampuni ya Willy Enterprises Ltd ya Dar es Salaam kukodisha mtambo wa kusafisha shamba (Buldoza) kwa ajili ya wanachama zaidi ya 100 waliojitokeza kulima.
Alisema SHIWATA itatumia sh. mil. 22.2 kukodisha buldoza hilo kusafisha shamba la ekari 200 zilizogaiwa kwa wanachama ambapo kila mmoja atalipa gharama ya sh. 111,000 kwa ekari moja.
Jitihada za kusafisha shamba hilo zinafanywa na SHIWATA ikiwa ni maandalizi ya kufikiwa kwa malengo ya kuanzishwa mtandao huo utakaoadhimisha miaka 10 ya kuanzishwa mwaka 2004.
Mpaka sasa SHIWATA inao wanachama 8,000 kutoka fani mbalimbali za uigizaji, muziki wa dansi, muziki wa kizazi kipya, taarab, soka, netiboli, vijana na waandishi wa habari.
Mwanachama wa siku nyingi wa Shiwata Manase Zabron ambaye ni kocha wa mpira wa kikapu nchiniakienda kuoneshwa shamba lake
Baadhi ya viongozi wa Mtandao wa wasanii Tanzania ‘SHIWATA’ wakishudia ugawaji wa mashamba kwa wanachama wake juzi Ngarambe Mkulanga Mkoa wa Pwani
===========================================================

Taarifa ya Kifo Cha Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse

unnamed
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange anasikitika kutangaza kifo cha Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse (mstaafu) kilichotokea tarehe 29 Oktoba 2014 katika Hospitali ya Appolo nchini India alikokuwa akipata matibabu.
Mwili wa marehemu Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse (mstaafu) unatarajia kuwasili Tanzania tarehe 31 Oktoba 2014 saa 7:30 mchana na kuhifadhiwa katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo.
Heshima za mwisho kwa Viongozi, Wanajeshi na Watumishi wa Umma zitatolewa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo tarehe 01 Novemba 2014, kuanzia saa 4.00 hadi saa 5.00 asubuhi na mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Njombe kwa mazishi, ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika tarehe 02 Novemba, 2014 saa 8.00 mchana.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
====================================================
1Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere  leo mara baada ya kuwasili  akitokea katika ziara yake ya Ulaya  na Mashariki ya Kati Oman. 2Baadhi ya viongozi alioongozana nao katika ziara hiyo wakiwa katika mkutano huo.
…………………………………………………………………..
Na Magreth Kinabo – MAELEZO
Waziri Mkuu Mizengo  Pinda amesema  Serikali imeanza kulifanyia kazi tatizo la wakulima kukosa mahali pa kuhifadhia ya mazao yao, hivyo  litapatiwa  ufumbuzi katika kipindi cha miezi mitatu hadi minne ijayo baada ya mpango wa kujenga maghala makubwa kuanza.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri Mkuu, Pinda  katika mkutano wake na waandishi wa habari alioufanya mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu  Julius  K.Nyerere  uliopo jijini Dares Salaam kufuatia ya ziara yake ya kikazi katika nchi za Uingereza, Poland na Oman. yenye lengo la kuhimarisha mahusiano.
Waziri Mkuu Pinda alisema ametembelea nchi ya Poland, ambayo ilikuwa na lengo la kuhimarisha mahusiano na ushirikiano na kutafuta msaada wa mfumo wa mkopo wenye masharti nafuu wa kusaidia kupambana na tatizo la uhaba wa maghala  kwa ajili ya kuhifadhia nafaka au chakula.
Alisema katika nchi hiyo amejionea jinsi ilivyo kuwa na mfumo  maalum  wenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi chakula.
“Unahitajika mfumo huu wa Poland wenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi  chakula. Hivyo tunahitaji kiasi cha fedha cha  Sh.  bilioni 240 hadi  bilioni 260  kwa ajili ya kukabilian na tatizo hili, tumeandika ombi na tumeshapeleka  kwa Serikali,” alisema Waziri Mkuu Pinda.
 Aliongeza kwamba  pia wameomba mkopo wenye masharti nafuu ili kusaidia kupambana na tatizo la uhaba wa maghala kwa ajili ya kuhifadhia chakula, hivyo kwa kuanzia wameomba mkopo wa Euro milioni 500 katika nchi ya Poland,ambao wenye riba  nafuu ya kiasi cha 0.25.
 Alisema lengo ni kujenga maghala kubwa katika  baadhi ya mikoa, ambayo aliitaja kuwa ni  Rukwa, Ruvuma, Iringa, Njombe, Dodoma,  Tanga na ghala dogo katika  Kanda ya Ziwa.
Akizungumzia kuhusu uzalishaji wa mahindi nchini alisema wakulima wameweza kuzalisha tani 500,000 za mahindi, lakini changamoto iliyopo iliyopo   ni mahali pa kuhifadhia.
 Aliongeza kuwa uwezo wa maghala ya  Wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa Chakula(NFRA) ni tani 240,000  wakati bado kuna tani zaidi ya 200,000 zilizozalishwa mwaka jana (msimu uliopita) za mahindi na katika kipindi cha sasa wamepanga kununua  tani 3.
Waziri Mkuu Pinda alisema Serikali imeshirkisha sekta  binafsi ili iweze kununua tani 200,000 na lakini bado chakula ni kipo cha kutosha.
 Alisema kwa upande wa mpunga kuna tani zaida 800,000 kwani msimu huu zilimezalishwa tani milioni 1.5. hali hiyo imechangiwa na matumizi ya mbegu bora, mbolea na  matumizi ya matrekta.
Waziri Mkuu aliwapongeza wakulima kwa juhudi zao za kulizalisha chukula cha kutosha.
Akizungumzia kuhusu ziara yake nchini Oman alisema ilikuwa na lengo la kuhimarisha mahusiano na ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara.
Alisema nchi hiyo mwikitio wa nchi hiyo wa kuwekeza ni mzuri hususan kwenye kilimo, mifugo na uvuvi.
“ Eneo walioonesha hisia ni la mifugo,  hasa

No comments:

Post a Comment