TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, November 1, 2014

MFUKO WA WANAFUNZI WALIOHITIMU SHULE KONGWE ILBORU WATARAJIA KUTUMIA ZAIDI YA MILIONI 20 KUKARABATI MAJENGO

New Picture
 Na Gladness Mushi,Arusha

MFUKO wa wanafunzi waliohitimu zamani katika shule kongwe ya vipaji maalum ya  Ilboru(Ilboru Alumni Foundation)wanatarajia kutumia kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 20 hadi ifikapo  desemba mwaka huu kwa ajili ya kukarabati majengo  ya shule hiyo ili kuweza kuirejesha katika mazingira mazuri .
Aidha kwa sasa shule hiyo pamoja na kuwa ni ya vipaji maaluma lakini mazingira yake hayako katika hali nzuri hali ambayo iliwafanya wanafunzi hao waliomaliza miaka ya nyuma kuungana ili kuikarabati na kuirejeshea mzingira yake ya miaka ya nyuma kwa lkuwa mazingira mabaya yanachangia kufelisha wanafunzi.
Hayo yalisemwa na mtendaji mkuu katika mfuko huo ambaye ni dr Daniel Maro alipokuwa akikabidhi rasmi funguo za darasa moja lililomalizika kukarabatiwa katika mahafali ya 25 ya kidato cha nne ya shule hiyo ambapo darasa hilo limegharimu kiasi cha  zaidi ya milioni 4 .
Dr Maro alisema kuwa shule hiyo imekuwa ikizalisha wataalamu mbali mbali sana lakini bado ina changamoto nyingi ambazo zinawahitaji wadau wa elimu kuziunga mkono ili kuhakikisha kuwa watoto wanasomea katika mazingira mazuri.
“sisi tumeungana kwa pamoja tuliosoma kwa kipindi cha kuanzia 1999 katika kuhakikisha kuwa tunarejesha mzingira ya nyuma kwani mazingira ya sasa nay a kipindi tulichokuwa tunasoma yalikuwa ni tofauti sana na mzingira mabaya yanasababisha hata watoto kutosoma vizuri”aliongeza dr Maro.
Alifafanua kuwa hadi sasa wameshafanikiwa kukarabati darasa moja na wana mpango wa kuendelea na madarasa mengine manne ambayo kila moja litagharimu zaidi ya milioni nne ambapo wanatarajia hadi ifikapo desemba wawe wameshakamilisha mchakato wa kukarabato majengo hayo ambayo yamekuwa chakavu mno.
Aidha dr Maro alisema kuwa mara baada ya kumaliza kukarabati majengo hayo bado wataendelea kutatua changamoto nyinginzo zinazoikabili shule hiyo huku akiwataka wale wote waliomaliza katika shule

No comments:

Post a Comment