TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, December 11, 2014

DR. ALI MOHAMMED SHEIN MGENI RASMI TUZO ZA TASWA KESHO

indexMAANDALIZI kwa ajili ya Tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania, zinazotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA) yamekamilika.
Tuzo hizo zitatolewa kesho Ijumaa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam, kuanzia saa 12 jioni, ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein.
Wanamichezo mbalimbali wanatarajiwa kupewa tuzo hizo kutokana na kufanya vizuri katika michezo yao kwa kipindi cha Juni 2013 hadi Juni 2014, ambapo bendi ya Kalunde ya Dar es Salaam itatumbuiza.
Washindi wa kila mchezo watawania nafasi ya Mwanamichezo Bora wa Tanzania mwaka 2013/2014 na mshindi atatangazwa ukumbini na Dk. Shein, ambaye pia atamkabidhi tuzo yake.
Baahi ya waliopata kutwaa tuzo ya Mwanamichezo Bora Tanzania ni Samson Ramadhani (2006), Martin Sulle (2007) na Mary Naali (2008) wote wanariadha.
Mwaka 209 tuzo ilienda kwa mcheza netiboli Mwanaid Hassan, ambaye pia alitwaa tuzo hiyo mwaka 2010, wakati mwaka 2011, ambapo tuzo yake ilitolewa mwaka 2012 mshindi alikuwa mwanasoka Shomari Kapombe.
Tuzo ya mwaka 2012 iliyokuwa itolewe mwaka 2013 haikufanyika kutokana na wadhamini kujitoa dakika za mwisho. Kwa kawaida tuzo ya mwaka husika hutolewa kati ya Juni hadi Agosti mwaka unaofuata.
Wanamichezo wengine watakaoshinda kwenye michezo yao kesho watakabidhiwa tuzo zao na wageni mbalimbali walioalikwa wakiwemo wanamichezo wa zamani, viongozi wa serikali na wa kisiasa.
Tuzo za mwaka huu zimedhaminiwa na Selcom Wireless, Said Salim Bakhresa & Co Ltd – Bakhresa Group, IPTL, A to Z, mifuko ya hifadhi ya jamii, PSPF na NSSF.
Pia kutatolewa tuzo ya Heshima, ambayo itatangazwa na mgeni rasmi na ndiye atakayekabidhi zawadi kwa mshindi huyo.
Tuzo ya Heshima inatolewa kwa mdau yeyote ambaye TASWA inaona anastahili kutokana na mchango wake katika masuala mbalimbali ya michezo.
TASWA imewahi kutoa Tuzo ya Heshima kwa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, pia imewahi kutoa Tuzo ya Heshima kwa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ iliyokuwa ikicheza mechi za kufuzu fainali za mataifa ya Afrika mwaka 1980 zilizofanyika Lagos, Nigeria.

No comments:

Post a Comment