TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, December 12, 2014

Haya ndiyo makosa ambayo hutakiwi kufanya unapokuwa na pesa:-

1. Acha kutumia kiasi kikubwa cha pesa kuliko ya kile unachokipata.

Watu wengi wanapata shida katika maisha yao kwa sababu ya kufanya kosa hili la kutumia kiasi kikubwa cha pesa kuliko ya kile wanachokipata. Unapotumia pesa nyingi kuliko ya zile unazozipata, mwisho utajikuta wewe ni mtu wa madeni na unakuwa unashindwa hata kuweka akiba ambayo inaweza kukusaidia kuwekeza katika miradi yako hapo baadae. 

Kama una malengo na mipango imara ya kuwa tajiri katika maisha yako, hakikisha kuanzia sasa, unaepuka kuishi juu ya kipato chako na mafanikio utayaona. Utaweza kufanikisha hili kama utajiwekea bajeti yako vizuri na kuisimamia. Acha maisha ya tamaa ambayo yatakuingiza kwenye matumizi yasiyo lazima, na mwisho utajikuta unatumia pesa hovyo kuzidi kipato chako.

 


2. Acha kufanya kosa la kutojilipa wewe mwenyewe kwanza.

Ili uweze kufanikiwa na kuona ndoto zako zinatimia, unalazimika kujilipa wewe kwanza kwa kile unachokipata. Ni muhimu kujilipa, kwa sababu wewe ndiye mtu wa kwanza ambaye umekuwa ukiifanyia kazi hiyo pesa uliyoipata.

Wengi wetu tumekuwa tukifanya kosa hili mara kwa mara kwa kutumia kiasi chote cha pesa tunachopata na kusahau kujilipa. Kama unaishi maisha haya ya kutojilipa, sahau kuwa tajiri katika maisha yako. Hivyo, unapopata pesa hakikisha unatenga asilimia kumi ambayo ni malipo yako kwanza. 

3. Acha kuishi maisha ya kutegemea chanzo kimoja cha kipato.

Wengi tunaishi maisha ya kutegemea chanzo kimoja tu cha kipato na wakati mwingine huwa ni watu wa furaha hiyo yote kuonyesha tunakubaliana na kile tunachokipata. Kama kweli unataka kuwa tajiri katika maisha yako, unalazimika kutengeneza vyanzo vingi vya fedha ambavyo vitakusaidia hata pale mambo yako yanapokwenda vibaya.

Unapokuwa na pesa acha kufanya kosa la kutokuwekeza. Jifunze, kuwekeza zaidi na zaidi kwani utakuwa unapanda mbegu ambayo utakuja kuivuna katika maisha yako baadae na hatimaye utajenga nguvu ya kukufanya kuwa tajiri kutokana na miradi ambayo umejiwekea.

4. Acha kununua vitu visivyo vya lazima kwako.

Ili tuweze kufanikiwa na kusonga mbele katika maisha yetu, ni muhimu kujenga tabia ya kununua vitu vile tunavyovihitaji ambavyo ni lazima kwa matumizi na si vinginevyo. Acha kununua vitu kwa sababu ya tamaa ya macho au kwa sababu umeona jirani yako amenunua kitu Fulani nawe unataka kununua. 

Kama unaishi maisha haya ya kuangalia Fulani kafanya nini, utashindwa kusonga mbele. Ishi maisha yako wewe kama wewe, tengeneza bajeti yako itakayokuongoza kwa siku, wiki au hata mwezi kisha uifate. Acha kufata mkumbo.

5. Acha kuishi maisha ya kutokuwa na mipango endelevu.
 
Hakikisha una mipango imara ambayo ipo mikononi mwako na itakufikisha kwenye uhuru wa kifedha unaoutaka. Pesa hizo ulizonazo hata kama unaona ni kidogo zipangilie vizuri, zitakusogeza hapo ulipo na kukupeleka sehemu nyingine ambayo hukutarajia hapo mwanzoni. Kama unaona pesa zako hazitoshi, jifunze kutunza pesa zako kidogo kidogo mpaka ziwe nyingi.

Acha kuzitumia pesa zako hovyo kwa kuzidharau eti ni kidogo, hapo utakuwa unakosea. Kumbuka kila pesa yoyote ile iliyopo mikononi mwako, ina thamani kubwa sana kuliko unavyofikiri. Unaweza ukaanza kuishi maisha yako ya kuwa na mipango endelevu leo na sio kesho kama ambavyo umekuwa ukiahirisha mara kwa mara.

Kama unataka kuwa tajiri katika maisha yako, naomba nikwambie ukweli huu tena, acha kufanya makosa haya unapokuwa na pesa. 
 
 Katika maisha hakuna njia rahisi, hakuna njia ya mkato zaidi ya kupambana na kujitoa mhanga kwa kila hali na kukubali kukabiliana na changamoto unazokutana nazo na kuzishinda. Kwa kila nafasi unayopata unapokuwa na pesa itumie vizuri utajiri utakuwa ni wako.

No comments:

Post a Comment