TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, December 12, 2014

MOJA KATI YA MATUKIO YA AJABU DUNIANI YAKIAMBANA NA UPENDO, AFUNGA NDOA NA MAITI

 picha hii hapa ni wakati wa mapenzi yao kabla ya kifo kilichotokea

Moja kati ya matukio ya kushangaza sana hapa Duniani, ni tukio la kijana mmoja, aliyeomba kufunga ndoa na mchumba wake ambaye alifariki ghafla kutokana na ajali muda mfupi kabla ya kufunga ndoa yao!!

 
Kijana mmoja Chadil Deffy  katika nchi ya  Thailand amefunga ndoa na  girlfriend wake ambaye amekufa ili  kutimiza ahadi yake ya upendo.  Kijana huyo mwenye umri wa miaka29 na mchumba wake mwenye umri wa miaka 28 anayeitwa Sarinya Kamsook walikuwa wamepanga  kuoana mwaka huu.

Sarinya Kamsook kwa bahati mbaya alifariki katika ajali ya gari, siku moja kabla ya tukio kubwa la harusi yao, Deffy aliamua kuendelea na harusi yao kama ilivyopangwa. Sarinyaalihusika katika ajali mbaya ya gari, na kupata majeraha makubwa. Madaktali walijitahidi kumhudumia . Hata hivyo madaktari wakiwa katika jitihada za kuokoa maisha yake ili na kuchelewa kumhamishia hospitali nyingi badala ya ile aliyokuwa amelazwa kuna na msongamano mkubwa. Na alifariki baada ya masaa sita. Ibada hiyo ya harusi iliunganishwa na ibada ya mazishi iliyofanyika katika kitongoji cha Surin, Thailand, kijana Chadil Duffyalimvisha pete mpenzi wake huyo ambaye ni  marehemu. Na tukio hilo likawa ni tukio la kipeke kutokea hapa duniani ambalo ni ibada ya harusi na mazishi kwa wakati mmoja.
 
 picha hii hapa inaonyesha matukio manne huyu kijana akimvika pete na kuonyesha aina zote za kufunga ndoa na mchumba wake ambaye sasa ni marehemu!!!
"Deffy na Sarinya alikuwa pamoja kwa miaka 10, na hatimaye waliamua kukaa chini.Walikuwa wameahirisha  harusi mara kadhaa, kutokana na kutokupata muda muafaka naukweli kwamba Deffy alitaka kumaliza elimu yake kabla ya kufunga  ndoa. Hata hivyo,baada ya kifo cha mpenzi wake Sarinya Deffy aliona hakuna kizuizi cha yeye kutimiza shauku yake ya kufunga harusi na mchumba wake huyo, hivyo aliamua kufunya harusi kabla ya kumzika. Sherehe hiyo ya Kibuddhist  ilifanyiaka katika mji wa Surin kaskazini mwaThailand. Deffy  alisema mbele ya jamaa na marafiki waliokuwepo katika sherehe kuwa ibada hiyo amefanya ili kuonyesha upendo wake mkubwa  kwa Sarinya. Marafiki na jamaakadhaa walihudhuria harusi hiyo, na tukio hilo lilivuta hisia za watu wengi nchini humo na kufanya TV ya taifa ya nchi hiyo kurusha tukio hilo live. Hadithi, pamoja na picha kutoka kwenye harusi hiyo sasa vimevuta hisia za watu wengi katika internet, hivyo kuzua mijadala kadhaa. "

No comments:

Post a Comment