TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, December 12, 2014

FUNZO LA MASHAIRI YA WIMBO ‘’STAKI KAZI’’ WA NIKI WA PILI

Photo: FUNZO LA MASHAIRI YA WIMBO ‘’STAKI KAZI’’ WA NIKI WA PILI

Hapa nitajadili mistari sita muhimu ya kujifunza kwenye wimbo huu; 

1. Nimekataa kuwa mtumwa, najituma. Kataa kuwa mtumwa, jitume. 

Ni kweli kwamba kuna tofauti ndogo sana kati ya kuajiriwa na utumwa. Tofauti ni kwamba kuajiriwa ni utumwa ambao huujui na hivyo kuendelea kuufurahia. Kama mtu atakupangia ni muda gani uamke, muda gani ule na hata aweze kukupangia ni kiasi gani cha fedha utapata, huwezi kujitofautisha na mtumwa. Uzuri ni kwamba nguvu ya kuondoka kwenye utumwa huu unayo, ni wewe kuamua kuchukua hatua. 

2. Mishahara imejaa makato, biashara mjini ndio zimejaa mapato. 

Ni vigumu sana kupata uhuru wa kifedha kupitia kuajiriwa. Hii inatokana na sababu nyingi sana ikiwemo mazingira ya kazi kuwa magumu, makato, na mishahara isiyoendana na hali ya kiuchumi. Kutokana na haya ni vyema kufanya kazi kwa malengo ili baadae kuweza kujiajiri au kuanzisha biashara ambayo itakupa uhuru mkubwa wa kifedha na maisha kwa ujumla.

3. Kazi ni mpaka wa akili yako, mpaka ufukuzwe kazi ndio ugundue kipaji chako.

 Hili limekaa wazi kabisa, moja ya vitu ambavyo aliekuajiri anavifanya ili aendelee kukufanya mtumwa ni kufanya akili yako iamini kwamba maisha yako hayawezi kwenda bila ya ajira yako. Hii imewafanya wengi kudumazwa kiakili na kutumikia ajira kwa maisha yao yote. Kuonesha kwamba anachokwambia mwajiri wako ni uongo kuna watu wengi wamefukuzwa au kukosa kuajiriwa ila maisha yao ni mazuri kushinda wewe uliyeajiriwa. Hii inaonesha kwamba inawezekana kufanya mambo makubwa hata kama hujaajiriwa, hivyo kuliko kukazana kuomba kazi au kung’ang’ania kazi ambayo haikuridhishi, hebu jua vipaji vyako na uanze kuvitumia kutengeneza ajira yako mwenyewe.

4. Elimu bongo imekosa plani ya pili, kosa la pili haufundishwi kuwa tajiri. 

Mfumo wetu wa elimu ni mbovu na hauendani na wakati. Hili linaashiriwa na idadi kubwa ya wahitimu tulionao huku tukiwa na nafasi finyu sana za ajira. Kama elimu yetu ingekuwa inafundisha jinsi mtu anavyoweza kutoka kimaisha bila hata ya ajira, vijana wengi wangeingia mtaani wakiwa na mtazamo tofauti.
5. Nakuza network najuana na watu, nauza network naunganisha watu.

 Mafanikio yako kwenye kazi na hata biashara yanatokana na idadi ya watu ulionao kwenye mtandao wako. Hivyo badala ya kukazana kutafuta kazi ni vyema kutafuta mtandao mzuri ambao utakusaidia sana kwenye kujiajiri na hata biashara.

6. Sitafuti kazi, nataka nitafutwe na wanaotafuta kazi. Sitaki kazi, natengeneza ajira mtaa niupe kazi.

 Utakapoamua kujiajiri hutajisaidia tu wewe mwenyewe bali utaweza kuwasaidia wengine ambao hawajaweza kupata ufahamu kama wa kwako wa kuweza kujiajiri au kuanzisha biashara. Hivyo badala ya kuwa mbinafsi na kutengeneza mshahara wako tu, hebu tengeneza ajira ambazo zitakuwanya wewe kuwa huru na kuwasaidia wengi zaidi. Wimbo huu ni mzuri sana kwa watu wote ambao wanatafuta kazi ila bado hawajapata na hata wale ambao wanafanya kazi ila hawaridhishwi na mazingira ya kazi zao au kipato wanachopata. Unao uwezo mkubwa sana wa kuweza kuchukua hatua juu ya maisha yako. Maisha hayatakuwa na maana kwako kama hufurahii kile unachokifanya. 

No comments:

Post a Comment