TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, December 11, 2014

MAANDALIZI YA MECHI YA NANI MTANI JEMBE

index
Maandalizi ya mechi ya Nani Mtani Jembe yamekamilika. Mchezo huu utachezwa Jumamosi ya Tarehe 13 Desemba 2014 Uwanja wa Taifa kuanzia saa 10:00jioni. Milango itafunguliwa kuanzia saa 04:00 asubuhi. Tiketi zitaanza kuuzwa saa 02:00 asubuhi siku ya Ijumaa tarehe 12 Desemba 2014 katika vituo vifuatavyo:

  1. Karume Stadium.
  2. Uwanja wa Taifa.
  3. Steers – Samora Avenue.
  4. Stand ya Mabasi Makumbusho.
  5. Ubungo kituo cha Oil Com.
  6. Buguruni Kituo cha Mafuta cha Kobil.
  7. Mbagala Dar Live.
  8. Mwenge Stand ya mabasi ya Zamani.
  9. Mnazi mmoja.

Viingilio katika mchezo huu vitakuwa kama ifuatavyo:
  • Mzunguko                        –       Sh. 7,000
  • Orange                            –        Sh. 15,000
  • VIP C                              –       Sh. 20,000
  • VIP B                               –        Sh. 30,000

TFF inatoa angalizo kuwa hitaruhusiwa kuingia uwanjani na silaha ya aina yoyote, chupa, baruti na mabegi. Pia watazamaji wanatahadharishwa kutonunua tiketi nje ya magari rasmi yatakayokuwa na namba maalum ya TFF. Tiketi zitakuwa na alama maalum ya SIRI hivyo atakayebainika kuwa na tiketi ambayo sio halali atachukuliwa hatua za kisheria.
Waamuzi wa mchezo watakuwa ni:
  • Jonesia Rukyaa (Mwamuzi wa kati).
  • Josephati Bulali (Mwamuzi Msaidizi Na. 1).
  • Mohamed Mkono (Mwamuzi Msaidizi Na. 2).
  • Kennedy Mapunda (Mwamuzi Na. 4).
Mgeni rasmi atakuwa Mh. Dr. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No comments:

Post a Comment