TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, December 11, 2014

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima azindua Mtambo wa Kuzalisha Kimiminika cha Nitrogeni

???????????????????????????????Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mkoani KATAVI Paza Mwamlima mwesnye suti ya bluuakipata maelezo toka kwa wataalam wa mifugo baada ya  kuzindua Mtambo wa Kuzalisha  Kimiminika   cha Nitrogeni Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda,wengine ni wataalamu wa mifugo Laurensi Eliasi ayelivaa Tishiti ya mistari na Mzozomo Mbogo.  ???????????????????????????????Hapo Mzozomo Mbogo akimpatia maelezo Mkuu wa Wilaya namna mtambo unavyofanya kazi na Faida zake kwa Halmashauri wafugaji na Taifa kwa ujumla . (Picha zote na Kibada Kibada-Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Mpanda.)
………………………………………………………………………………………………
Na Kibada Kibada-Katavi
 
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Paza Mwamlima  amezindua Mtambo wa Kuzalisha Kimiminika cha Nitrogeni utakaotumika  katika kuhifadhi mbegu bora za  mifugo kwa ajili ya uhamilishaji mifugo na kuwezesha upatikanaji wa  kosaafu za ng’ombe zenye tija.
 
Akitoa Taarifa ya Mtambo huo, kwa Mkuu wa Wilaya Afisa Mifugo  kutoka Idara ya Mifugo na Uvuvi  Laurensi Elias  ameeleza kuwa Mtambo huo  uliletwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi tangu mwezi juni mwaka huu na usimikwaji wake umekamilika mwezi septemba mwaka huu shughuli iliyofanywa na Kampuni ya Cooporation Group Ltd
Amesema gharama za Mtambo huu hadi kufukishwa Wilayani Mpanda umetumia kiasi cha shilingi milioni 400 pamoja na gharama za usimikaji zilizogharimu kiasi cha shilingi milioni 37.2 hivyo kufanya jumla yote kuwa shilingi milioni 437.290,950/-
Mtambo huo ni aina ya Cryomech 120 una uwezo wa kuzalisha lita 5 kwa saa, kiasi hiki huzalishwa baada ya muda wa kuwa tayari takribani saa nne baada ya mtambo kuwashwa.
 
Ili mtambo uweze kuanza kazi kinahitajika kiasi cha shilingi milioni 39.7 kwa ajili ya kununulia vifaa na gharama ya kuwapeleka watalaam kwenye mafunzo ili waweze kusaidia kuendesha mtambo huo.
Amefafanua kuwa Ili mtambo ufanye vizuri ni lazima mambo ya umeme sahihi na wa kutosha uwepo, mfumo sahihi wa maji ya kutosha kwa ajili ya kupooza mtambo wakati wa uzalishaji,uwepo wa mzuunguko mzuri wa hewa ya kutosha isiyo na joto pamoja na usafiwa kutosha kuzuia vumbi inayoweza kuathiri mtambo.
 
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpanda Estomihn Chang’ah ameeleza kuwa mtambo huo ni wa kisasa na hapa nchini ni unapatikana katika Mkoa wa Arusha,Iringa na Mbeya Pekee na huu ulioletwa katika Halmashauri ya wilaya ya Mpanda utasaidia sana kuhudumia,Mikoa ya  Kigoma,Rukwa Tabora,Mbeya  na Iringa  nao  watanufaika na mtambo huo  kwa kuboresha mifugo kwa njia ya uhamilishaji.
 
Aidha utaongeza kipato cha Halmashauri kwa njia ya kuuza kimiminika katika taasisi mbalimbali kama Hospitali na maeneo mengine ya jirani  na mapato yatokanayo na gharama za uzalishaji,Pia utainua kipato cha Taifa na wafugaji kwa kuuza ng’ombe waliobora na wenye tija kuboresha lishe ya mwananchi.
 
Pia itapunguza maambukizi ya magonjwa ya mifugo yanayotokana na kupandisha ng’ombe kwa kutumia madume mfano ugonjwa wa kutupa mimba.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima ameshauri Halmashauri kujenga urafiki na wafugaji kwa kuwapa elimu  ili wawe pamoja wafugaji wote na utoaji wa huduma kwa kutumia mitambo huo utakuwa natija tofauti na sasa wafugaji wakiwaona watalaam wanawakimbia wanakuwa kama maadui.
Elimu itolewa kwa wafugaji waone mtambo huo kuwa utawasaidia kubadili hali ya ufugaji wao.

No comments:

Post a Comment