TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, December 11, 2014

RAIS DK. JAKAYA KIKWETE ATUNUKU NISHANI IKULU

unnamed Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku nishani ya miaka 50 ya Muungano daraja la pili Augustino Stephene Ramadhan katika hafla kutunuku nishani katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam sambamba na maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara jana.[Picha na Ikulu.] unnamed2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku nishani ya miaka 50 ya Muungano daraja la pili Ali Salum Ahmed katika hafla kutunuku nishani katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam sambamba na maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara jana.[Picha na Ikulu.]
unnamed4Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku nishani ya miaka 50 ya Muungano daraja la pili Mohammed Fakih Mohammed katika hafla kutunuku nishani katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam sambamba na maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara jana.[Picha na Ikulu.] unnamed5Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku nishani ya miaka 50 ya Muungano daraja la tatu Amani Issack Abraham Sepetu kwa niaba ya Baba yake Issack Abraham Sepetu (marehemu) katika hafla kutunuku nishani katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam sambamba na maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara jana.[Picha na Ikulu.] unnamed6 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku nishani ya miaka 50 ya Muungano daraja la tatu Ali Ameir Mohamed katika hafla kutunuku nishani iliyofanyika  viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam sambamba na maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara jana.[Picha na Ikulu.] unnamed7Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku nishani ya miaka 50 ya Muungano daraja la nne Haji Machano  Haji  katika hafla kutunuku nishani iliyofanyika  viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam sambamba na maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara jana.[Picha na Ikulu.] unnamed8Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku nishani ya miaka 50 ya Muungano daraja la nne Bibi Johari Yussufu Akida katika hafla kutunuku nishani iliyofanyika  viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam sambamba na maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara jana.[Picha na Ikulu.]
unnamed9Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein (kutoka kushoto) Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi (katikati) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda wakiwa  hafla kutunuku nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano iliyofanyika  viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam sambamba na maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara jana.[Picha na Ikulu.]
===========================================================

Katibu wa CCM mkoani Iringa HASSANI MTENGA ameahidiwa ushindi

 Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Iringa HASSANI MTENGA akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kihesa Mgagao.
 Baadhi ya wananchi waliohudhulia mkutano huo.
NA FREDY MGUNDA,KILOLO
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Iringaha HASSANI MTENGA, amefungua rasmi kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa katika kijiji cha kihesa mgagao na kulakiwa na mamia ya wananchi katika kijiji chicho kilichpo wilayani kilolo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kampeni hizo Katika Kijiji hicho  HASSANI MTENGA alisema kuwa kampeni hizo zinazotaraji kufikia kikomo Disemba 13 Mwaka huu, zilipaswa kufanyika muda mrefu hivyo kilichochelewesha uchaguzi huo ni mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya.
MTENGA ametumia nafasi hiyo pia kuwanadi mgombea nafasi ya uenyeviti wa kijij hicho ambapo amewaomba  wananchi wa kijiji hiocho kumchagua PHILIPO KAGINE  awe mwenyekiti wao.
Akizungumzia sakata la vyama vya upinzani kutaka kugomea uchaguzi amesema kuwa wasimamizi wa uchaguzi nchini wanaangalia vigezo vya wagombea hivyo kama hawakuwa na vigezo kusingekuwa na usamaria mwema kwenye kwenye jambo.
nao wananchi wa kijiji hicho walimwambia katibu huyu kuwa mgombea wao kupitia chama cha mapinnduzi atashinda kwa kishindo kwa kuwa kijiji hicho ni ngome ya CCM.
====================================================================

KONGAMANO LA SIKU MBILI LA UKATILI WA JINSIA DHIDI YA WANAWAKE NA WALEMAVU LILILOANDALIWA NA SHIRIKA LA SEED TRUST LAFIKIA TAMATI MKOANI MOROGORO

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Seed Trust, Margareth Mkanga (MB) akizungumza katika kongamano hilo. Kulia ni Mwenyekiti wa Shirika hilo, Stephen Mashishanga. Kongamano hilo la Majadiliano kuhusiana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na walemavu limeshirikisha wadau mbalimbali kutoka baadhi ya mikoa ya Tanzania na kuandaliwa na Shirika la Seed Trust la mjini Morogoro kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA)
Mwenyekiti wa Shirika hilo, Stephen Mashishanga, akichangia mada katika kongamano hilo.
Dk.Ernest Rugiga akitoa mada kuhusu afya ya uzazi.
Mwezeshaji Victor Mulimila akizungumzia kwa ujumla kuhusu vitendo vya ukatili. Kulia ni Dk.Ernest Rugiga
Ofisa Tarafa wa Manispaa ya Morogoro, Mlange Pakalapakala Jumamosi, akichangia mada kwenye kongamano hilo.
Wanahabari walikuwepo kwenye kongamano hilo wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi. wa Bwalo la JKT mkoani humo.
Maofisa wa Shirika la Seed Trust wakiwa kwenye kongamano hilo.
Washiriki wa kongamano hilo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
======================================================

Tathimini ya ripoti mradi wa GEWE yazinduliwa Dar

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka pamoja na meza kuu wakionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka pamoja na meza kuu wakionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi (CRC), Bi. Gladness Munuo (wa kwanza kushoto) akizungumza katika uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) leo jijini Dar es Salaam
Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi (CRC), Bi. Gladness Munuo (wa kwanza kushoto) akizungumza katika uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) leo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) leo jijini Dar es Salaam.
TAMWA Yazinduwa Tathmini ya Ripoti Mradi wa GEWE
Mratibu wa Mradi wa GEWE kutoka TGNP Mtandao, Matha Samwel akizungumza na vyombo vya habari katika uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam.
kurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akizungumza na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa waliokuwa katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya GEWE jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akizungumza na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa waliokuwa katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya GEWE jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanahabari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa ripoti ya GEWE jijini Dar es Salaam Makao Makuu ya Ofisi za TAMWA Sinza Mori Dar es Salaam.
Baadhi ya wanahabari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa ripoti ya GEWE jijini Dar es Salaam Makao Makuu ya Ofisi za TAMWA Sinza Mori Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka pamoja na meza kuu wakionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka pamoja na meza kuu wakionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam.
CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na taasisi anuai za kijamii kimezinduwa tathmini ya ripoti juu ya utekelezaji wa mradi wa Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE).
Akizinduwa ripoti hiyo leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka alisema mradi huo umekuwa na mafanikio makubwa kwa jamii katika kujitambua na kuibua vitendo vya Ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari kuibua vitendo hivyo zaidi ya hapo awali.
Alisema idadi kubwa ya habari, makala na vipindi vya redio na televisheni juu ya masuala ya ukatili vimefanywa maeneo mbalimbali nchini, jambo ambalo limeonesha mafanikio ikiwa ni pamoja na jamii kuelewa zaidi masuala ya ukatili na unyanyasaji na wengine kuanza kuyapiga vita kwa ushirikiano.
Aidha Mkurugenzi huyo Mtendaji wa TAMWA alisema mradi huo ulitekelezwa kwa pamoja kwa ushirikiano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Kituo cha Usuluhishi cha TAMWA (CRC), kinatekeleza mpango wa kutokomeza ukatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE II) katika wilaya 10 za Tanzania bara na Zanzibar.
Kwa upande wake Matha Samwel Mratibu wa Mradi wa GEWE kutoka TGNP Mtandao, akizungumza alisema mradi huo umekuwa na mafanikio makubwa kiasi cha kuibua changamoto ambazo zinaitaji utatuzi kwa ushirikiano na wadau wengine mbalimbali.
“…Katika kipindi cha utekelezaji wa mradi wa GEWE kumekuwa na mafanikio makubwa, moja wapo kubwa ni kuanzishwa kwa vituo vya taarifa na maarifa katika wilaya zote 10 za mradi, ambapo vituo hivyo vimekuwa vikitumika kama sehemu ya kutolea taarifa kwa jamii…sehemu ambayo wanajamii wanawake na wanaume wanakutana na kubadilishana taarifa na kuangalia namna ya kutatua matatizo yao yanayotoka katika jamii kama kubakwa, vipigo au kulawitiwa na mengineyo,” alisema Bi. Samwel.
Hata hivyo aliongeza kuwa vituo vya taarifa na maarifa vimekuwa na msaada mkubwa katika maeneo hayo kwani jamii zimeweza kuvitumia pia kwa kujadili namna ya kukuza uchumi kwenye familia zao kwa kuanzisha vikundi vya kijasiriamali vinavyochangia pia kupunguza umasikini kwenye jamii suala ambalo linachangia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye jamii.
Anasema vituo vya taarifa na maarifa vimekuwa vikiunganisha nguvu na serikali na vyombo vingine vya dola kuhakikisha wanapambana na vitendo vya ukatili kwa kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake kwa watu wanaohusika ama kutuhumiwa na vitendo vya ukatili. Alitolea mfano katika eneo la Mwananyamala Kituo cha Taarifa na Maarifa kilishirikiana na Serikali kwa kuibua taarifa ya kuteswa kwa binti wa kazi za ndani na mwajiri wake jambo ambalo liliwezesha bosi huyo kufikishwa mahakamani.
“…Hivyo waweza kuona matokeo makubwa katika mradi wa GEWE ni kuanzishwa vituo vya taarifa na maarifa sehemu ambayo imekuwa ni kimbilio la wengi, na pili ni nguvu ya pamoja ya jamii katika uwajibikaji. Lakini changamoto iliyopo sasa ni namna ya kuwasaidia kwa kuwaifadhi waathiriwa wa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii,” alisema Mratibu huyo.
Aidha aliitaka Serikali na wadau wengine kujitokeza na kushirikiana katika kujenga kituo kikubwa cha kuwasaidi wananchi ambao wamekumbana na ukatili wa kijinsia wakati wakipatiwa huduma kabla ya kurejea katika jamii yao. “…Mfano kumekuwa kuna mabinti hata hapa Dar es Salaam wamekuwa wakikimbia kukeketwa na familia zao lakini hakuna sehemu ya kuwaifadhi, hivyo tunaiomba Serikali na wadau wengine wajitokeze ili kuunganisha nguvu tujenge kituo hiki,” alisema. *Imeandaliwa na www.thehabari.com
==================================================

Viongozi wa Dini Mbalimbali wamuombea dua Rais Kikwete ikulu


unnamedViongozi wa Dini wakimuombea dua Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati walipomtembelea kumjulia hali na kumuombea ikulu jijini Dar es Salaam. unnamed1Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na baadhi ya viongozi wa dini mbalimbali waliomtembelea na kumjulia hali pamoja na kumuombea dua ikulu jijini Dar es Salaam(picha na Freddy Maro) unnamed3Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na baadhi ya viongozi wa dini mbalimbali waliomtembelea na kumjulia hali pamoja na kumuombea dua ikulu jijini Dar es Salaam(picha na Freddy Maro)

Tigo yatoa dola 40,000 kwa miradi ya wajasiriliamali jamii

unnamedMkurugenzi Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez akimkabidhi cheti cha ushiriki kwenye shindano la Tigo Digital Changemakers kwa Severin Philemon wakati wa kutangaza washindi wa shindano hilo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
unnamed1Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez akimkabidhi cheti cha ushiriki kwenye shindano la Tigo Digital Changemakers kwa Mohamed Juma wakati wa kutangaza washindi wa shindano hilo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
unnamed2Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez (kushoto) akiwa na mmoja wa washindi wawili wa shindano la Tigo Digital Changemakers, Leka Tingitana, mara baada ya kumkabidhi zawadi ya mfano wa hundi wa dola 20,000 za Kimarekani ikiwemo cheti cha ushiriki kutoka Tigo na Reach for Change mapema leokwa mradi wake wa kijitali eAfya.
unnamed3Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez (kushoto) akiwa na mshindi mmoja wa shindano la Tigo Digital Changemakers Innocent James Sulle mara baada ya kumkabidhi zawadi ya mfano wa hundi dola 20,000 za Kimarekani ikiwemo cheti cha ushiriki kutoka Tigo na Reach for Change mapema leo kwa mradi wake wa kijitali Travelling Library.
  unnamed6Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez (kushoto) na Mkurugenzi wa kanda ya Afrika wa Reach For Change Bi.Amma Lartey(kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa shindano la Tigo Digital Changemakers, Leka Tingitana na Innocent James Sulle baada ya kutangazwa kuwa washindi wa shindano hilo lenye kutumia nyenzo za kidijitali kwa ajili yakuwasaidia watoto nchini.
……………………………………………………………………………..
Tigo kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali Reach for Change leo imetangaza washindi wawili wengine wa wajasiriliamali jamii watakaodhaminiwa kiasi cha dola elfu 20,000 kila mmoja kwa ajili ya kuendesha miradi yao inayolenga kuinua hali ya maisha ya watoto nchini. Washindi hao walichaguliwa katikati ya ushindani mkali ambapo mamia ya maombi na mawazo zaidi ya 557 yenye kutumia nyenzo za kidijitali kwa ajili yakuwasaidia watoto nchini yalipokelewa, alisema Mkurugenzi Mkuu Diego Gutierrez katika tafriija maalum jijini Dar es Salaam. Majina na miradi ya wawili hao ambao wanaungana na washindi wengine watano wa nyuma kama wajasiriliamali jamii katika shindano la Tigo Digital Changemakers ni kama ifuatayo: 1. Leka Tingitana, eAfya; o Hii ni teknolojia inayotumika kuongeza ufanisi katika mawasiliano na utendaji wa kazi wa sekta ya afya nchini kwa kuwafikishia huduma za afya wagonjwa kwa uharaka zaidi. Teknolojia hii inawalenga watumishi wa afya katika jamii. 2. Innocent James Sulle, Travelling Library; o Hii ni maktaba maalum ya kidijitali kwa ajili ya kuwapatia watoto fursa ya kujenga tabia ya kusoma vitabu kupitia njia za kusoma kielektroniki. “Tunayofuraha kubwa sana kufanikisha miradi ya kibunifu yenye suluhu za kidijitali kuweza kuinua hali ya maisha ya watoto nchini. Hii inadhihirisha kwamba tunadhamira ya dhati kabisa ya kusaidia jamii kupitia suluhu za kidijitali na hasa hasa katika kuwekeza kwa watoto ambao ndio taifa la kesho,” alisema Gutierrez. Aliendelea, “Wajasiriliamali hawa wawili wataingia katika mpango maalum wa maendeleo ambapo watapatiwa msaada wa kubadilisha mawazo yao kuwa miradi endelevu. Mbali na dola 20,000 wanazo zawadiwa, pia watapatiwa uongozaji maalum na ushauri wakitaalam kutoka maafisa waandamizi wa Tigo na Reach for Change.” Agosti mwaka huu, Tigo na Reach for Change walizindua kwa mara ya tatu nchini Tanzania mpango huu wenye malengo ya kuwatafuta na kuwasaidia wajasiriliamali jamii wenye mawazo mazuri ya kidijitali ya jinsi ya kusaidia kuinua hali ya maisha ya watoto. Mkurugenzi wa Kanda wa Reach for Change nchini Tanzania Amma Lartey pia aliwapongeza washindi hao pamoja na washiriki wote wa shindano la Tigo Digital Changemakers kwa kile alichoita “miradi mizuri” ambayo yalijaa ubunifu mkubwa. Hakika ilikuwa mchakato wenye ushindani mkubwa kuweza kuwachagua washindi wawili tu kati ya mamia na mamia ya miradi ambayo tulipokea. Imechukua zaidi ya miezi mitatu kuweza kupitia na kuchuja maombi ya kila mmoja aliyetuma na kuweza kufanya usaili kwa baadhi ya wale waliopita katika mchujo. Tunayofuraha kwamba mchakato huu umeisha kwa mafanikio makubwa huku tukiwapata washindi hawa wawili ambao tunaamini miradi yao yatakuwa chachu kubwa katika kuchangia kuleta maisha bora kwa watoto wengi nchi nzima,” Lartey alisema. Tigo na Reach for Change ilianza mchakato wa kuwatafuta wajasiriliamali jamii kutoka kila nchi ambayo kampuni ya Tigo inafanya kazi barani Afrika kuanzia Agosti 2012, mashindano hayo yalianzia Rwanda, ikifuatiwa na Tanzania, Congo DRC, Ghana, Chad halafu Senegal. Mpango huu wa Digital Changemakers ipo katika malengo ya Tigo ya kuleta maisha ya kidijitali nchini. Huu ni mwaka wa tatu tangu Tigo na Reach for Change wameanza kwa pamoja kuwadhamini wajasiriliamali jamii kuweza kutimiza miradi yao. Kwa muda huo wajasiriliamali jamii watano wamekwishapatiwa msaada wa kifedha kwa ajili ya kuendesha miradi yao ambapo mpaka sasa watoto 9,500 wameshanufaika nchi nzima.
=============================================================

Watanzania wahaswa kuendelea kusaidia sekta ya Michezo nchini

unnamed
WaziriwaHabari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na wadau wa michezo ya Ngumina na Karate wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa Ulingo wa Ngumi wa Kimataifa pamoja na hundi yenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya kusaidia mchezo wa Karate kutoka kwa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya Zantel Tanzania leo jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Pratap Ghose.
unnamed1Ulingo wa kisasa kwa ajili ya Mchezo wa Ngumi uliotolewa kama msaada na Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya ZANTEL na kupokelewa naWaziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara leo jijini Dar es Salaam.
unnamed3Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (Kulia) akijaribu baadhi ya vifaa vya mchezo wa ngumi (Gloves) wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa Ulingo wa Ngumi wa Kimataifa pamoja na hundi yenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya kusaidia mchezo wa Karate kutoka kwa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya ZANTEL leo jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Pratap Ghose na katikati yao mwenye suruali nyekundu ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) Bw.Lukelo Willilo.
unnamed4Afisa Mtendaji Mkuu wa ZANTEL Pratap Ghoe akisalimiana na Bingwa wa mchezo wa ngumi Tanzania Bondia Francis Cheka (kushoto) wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa Ulingo wa Kimataifa kwa ajili ya mchezo huo leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni wa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Picha zote na: Frank Shija, WHVUM
========================================================

ILIKUJUA MAHITAJI YAO SANJARI NA KUBADILISHA MITAALA YA ELIMU

WAZIRI wa
Kazi na Ajira , Gaudensia Kabaka 
wakati alipokuwa akizindua kongamano
lililoshirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kwaajili ya
kujadili changamoto
wanazozipata wadau hao
 
waziri wa ajira na kazi
Gaudensia Kabaka akiwa katika picha ya pamoja wadau
waliouthuria katika  konga mano
hilo

 Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi
akiwa anaongea katika kongamano hilo


wadau kutoka sekta ya gesi na petrol wakiwa
wanafatilia

katibu mkuu wa  VET Pro.Sifuni Mchome akiwa
anawakilisha mada

Na Woinde Shizza,Arusha
 Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi
(Veta)wametakiwa
kuhakikisha wanasikiliza maoni ya wadau ili kujua mahitaji yao sambamba na
kubadili mitaala ya elimu ya mafunzo yanayotolewa kwenye vyuo
hivyo ili kuendana na soko la ajira lililopo
hivi sasa.

Hayo yanesemwa leo  jijini hapa na WAZIRI wa
Kazi na Ajira , Gaudensia Kabaka 
wakati alipokuwa akizindua kongamano
lililoshirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kwaajili ya kujadili changamoto
wanazozipata wadau hao na nini chakuongeza kwa vijana wanaopitia Veta na kupata
ajira katika sekta mbalimbali sanjari na kuzindua kitabu kinachoanisha mahitaji
ya soko la ajira kwa vijana
 
Aidha  aliwataka vijana  kutumia fursa za kujiunga na
Veta ili waweze kujiariri badala ya
kufanya biashara za kuuza vitu mikononi
bali  watumie taaluma walizozipata
kuzalisha vitu vyenye ubora.
Alisema vijana
wanaopitia vyuo vya mafunzo Veta si wengi sana huku wimbi la vijana likiwa bado
mitaani na kuuza bidhaa zao mabarabarani hivyo ni vyema sasa vijana hao
wakaondoka barabarani na kujiunga na vyuo vya ufundi ili waweze kupata mbinu za
kutengeneza vitu sambamba na kupata masoko ya
uhakika.

waandishi  wa habari wa Mkoa wa Arusha wakimuoji
mwenyekiti wa bodi
Alisema ni
vyema sasa Vyuo vya Veta vikaweka mkazo katika sekta ya madini na gesi ili
waweze kuangalia mahitaji ya wataalam ni yapi na kutoa elimu hiyo ambayo
itawezesha vijana wengi kupata ajira na kukuza uchumi wan
chi.
 
“Mahitaji ya
vijana ni mengi katika sekta rasmi na zisizo rasmi na kia sekta inamtegemea mtu
fulani hivyo ni vyema Veta mkasikiliza mahitaji ya wadau sambamba na kutafuta
mbinu za kufundisha zaidi ili kuendana na mahitaji ya soko na nyinyi vijana
tokeni barabarani mkajiunge na vyuo vya ufundi ili kuweza kuuza biashara zenu
kwa ubora badala ya kukimbilia kuuza barabarani “.
 
Naye
Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi alisema kongamano hilo hufanyika
kila mwaka na kushirikisha wadau katika sekta mbalimbali ili kujadili masuala
mbalimbali na mahitaji ya wadau hao katika sekta ya ajira sambamba na kuboresha
mitaala itakayokwenda na wakati na kuwezesha vijana wanaopitia Veta kuwa bora
zaidi kipindi cha kumaliza chuo na kupata ajira.
 
Alisema pia
Veta inakabiliwa na uhaba wa rasilimali fedha
kwenye ujenzi wa vyuo vipya   kwenye Wilaya mpya ambazo ni
Katavi, Geita,
Njombe na Simiu lakini pia kuonaongezeko kubwa la vijana na watu mbalimbali
ambao wanajiunga na vyuo hivyo nchini kwaajili ya kupata mafunzo mbalimbali
yanayowawezesha kupata ajira.
 
 Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Veta, Profesa
Idrissa Mshoro alisisitiza kuwa  Veta
inatambua na kuthamini maeneo mbalimbali yanayohitaji soko la ajira ndio maana
vijana wanaopata ujuzi kupitia veta wanafanya kazi kwa makini na kujipatia
vipato zaidi.
 
Aliongeza
kuwa hivi sasa Veta inashirikiana na tasisi na mashirika mbalimbali hususan ya
sekta ya madini na gesi na kutoa mafunzo kwaajili ya kuwasaidia vijana
kukabiliana na soko la ajira .
==============================================================

flydubai announces three new routes including Hargeisa, Somaliland

141210f2
flydubai will become the first carrier to operate to Hargeisa, Somaliland from Dubai with four weekly flights
…………………………………………………………………………………………………………
From 05 March 2015, flydubai will become the first carrier to operate to Hargeisa, Somaliland from Dubai with four weekly flights. flydubai has expanded its network in Africa in 2014 to 13 points served by 60 weekly flights.
Commenting on the new announcements, Hamad Obaidalla, Chief Commercial Officer at flydubai, said: “2014 continues to be a very busy year for flydubai. We have announced 26 new routes since January and took delivery of eight new aircraft to support the phenomenal growth plans. We are very excited about the untapped opportunities in the emerging African markets, the progress the UAE has made on the bilateral front in India and the ongoing strong ties with Saudi.”
The new announced routes underline flydubai’s commitment to connecting the UAE to previously underserved markets. The carrier has linked Dubai to 56 underserved destinations since it started its operations in 2009.
Sudhir Sreedharan, Senior Vice President Commercial (GCC, Subcontinent, Africa) for flydubai, said: “We are committed to bringing flydubai’s high quality and reliable services to underserved markets like Hargeisa and giving passengers more options to travel to the UAE and beyond through Dubai’s aviation hub. We are sure that both our Economy Class and Business Class will exceed the passengers’ expectations and live up to the Dubai brand we proudly carry in our name.”
flydubai has a brand new fleet of 43 new Next-Generation Boeing 737-800 aircraft and operates more than 1,200 flights a week across the Middle East, GCC, Africa, Caucasus, Central Asia, Europe and the Indian Subcontinent.
======================================================

ZIARA YA NAIBU WAZIRI OFISI YA MAKAMU WA RAIS MH. UMMY MWALIMU MTWARA

unnamedAfisa Uhusiano wa kampuni ya SBS, Bw. Geofrey Kanenge  (katikati) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb) (wa pili kushoto)  kuhusu udhibiti wa utiririshaji wa maji taka yatokanayo na usafishaji wa mapipa yenye kemikali unavyofanywa na kampuni hiyo wakati wa ziara ya ukaguzi wa mazingira mkoani Mtwara.
Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb) Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais alifanya ziara ya kukagua Mazingira Mkoani Mtwara hususan katika eneo la Mdenga, Manispaa ya Mtwara. Chimbuko la ziara hii ni malalamiko yaliyotolewa na wananchi kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Abdulrahman Kinana alipokuwa kwenye ziara ya kikazi mkoani humo unnamed1Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu (katikati) akipata maelezo kuhusu ubanguaji wa korosho kutoka kwa Uongozi wa Kiwanda cha Micronix  kilichopo mkoani Mtwara wakati wa ziara aliyoifanya mkoani humo. unnamed2Sehemu ya Wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kukagua hali ya Mazingira ya viwanda  aliyoifanya mkoani Mtwara unnamed4Eneo la bwawa la asili la Mdenga lililofukiwa kinyume cha sheria na kampuni ya SBS inayojishughulisha na urejelezaji wa taka mkoani Mtwara na kusababisha uharibifu wa mazingira katika eneo hilo.
=================================================================

WATAKIWA KUHAKIKISHA WANASIKILIZA WADAU KUJUA MAHITAJI

images
Mahmoud Ahmad Arusha
WAZIRI wa Kazi na Ajira , Gaudensia Kabaka ametoa rai kwa  Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta) kuhakikisha wanasikiliza maoni ya wadau ili kujua mahitaji yao sambamba na kubadili mitaala ya elimu ya mafunzo yanayotolewa kwenye vyuo  hivyo ili kuendana na soko la ajira lililopo hivi sasa.
Aidha vijana wameaswa kutumia fursa za kujiunga na Veta ili waweze kujiariri badala ya kufanya biashara za kuuza vitu mikononi  bali  watumie taaluma walizozipata kuzalisha vitu vyenye ubora.
Hayo yalisemwa jana Jijini hapa na Kabaka wakati alipokuwa akizindua kongamano lililoshirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kwaajili ya kujadili changamoto wanazozipata wadau hao na nini chakuongeza kwa vijana wanaopitia Veta na kupata ajira katika sekta mbalimbali sanjari na kuzindua kitabu kinachoanisha mahitaji ya soko la ajira kwa vijana .
Alisema vijana wanaopitia vyuo vya mafunzo Veta si wengi sana huku wimbi la vijana likiwa bado mitaani na kuuza bidhaa zao mabarabarani hivyo ni vyema sasa vijana hao wakaondoka barabarani na kujiunga na vyuo vya ufundi ili waweze kupata mbinu za kutengeneza vitu sambamba na kupata masoko ya uhakika.
Alisema ni vyema sasa Vyuo vya Veta vikaweka mkazo katika sekta ya madini na gesi ili waweze kuangalia mahitaji ya wataalam ni yapi na kutoa elimu hiyo ambayo itawezesha vijana wengi kupata ajira na kukuza uchumi wan chi.
“Mahitaji ya vijana ni mengi katika sekta rasmi na zisizo rasmi na kia sekta inamtegemea mtu fulani hivyo ni vyema Veta mkasikiliza mahitaji ya wadau sambamba na kutafuta mbinu za kufundisha zaidi ili kuendana na mahitaji ya soko na nyinyi vijana tokeni barabarani mkajiunge na vyuo vya ufundi ili kuweza kuuza biashara zenu kwa ubora badala ya kukimbilia kuuza barabarani “.
Naye Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi alisema kongamano hilo hufanyika kila mwaka na kushirikisha wadau katika sekta mbalimbali ili kujadili masuala mbalimbali na mahitaji ya wadau hao katika sekta ya ajira sambamba na kuboresha mitaala itakayokwenda na wakati na kuwezesha vijana wanaopitia Veta kuwa bora zaidi kipindi cha kumaliza chuo na kupata ajira.
Alisema pia Veta inakabiliwa na uhaba wa rasilimali fedha  kwenye ujenzi wa vyuo vipya   kwenye Wilaya mpya ambazo ni Katavi, Geita, Njombe na Simiu lakini pia kuonaongezeko kubwa la vijana na watu mbalimbali ambao wanajiunga na vyuo hivyo nchini kwaajili ya kupata mafunzo mbalimbali yanayowawezesha kupata ajira.
 Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Veta, Profesa Idrissa Mshoro alisisitiza kuwa  Veta inatambua na kuthamini maeneo mbalimbali yanayohitaji soko la ajira ndio maana vijana wanaopata ujuzi kupitia veta wanafanya kazi kwa makini na kujipatia vipato zaidi.
Aliongeza kuwa hivi sasa Veta inashirikiana na tasisi na mashirika mbalimbali hususan ya sekta ya madini na gesi na kutoa mafunzo kwaajili ya kuwasaidia vijana kukabiliana na soko la ajira .
========================================================

RAIS WA ZANZIBAR DR. ALI MOHAMMED SHEIN MGENI RASMI TUZO ZA TASWA

2Makamu mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari za Michezo TASWA Bw. Egbert Mkoko kushoto   na Katibu Mkuu wa TASWA Amiri Mhando wakionyesha tuzo zitakazotolewa kwa wanamichezo bora wa mwaka wa TASWA  katika hafla itakayofanyika ijumaa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP mgeni rasmi akiwa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh Dr. Ali Mohammed Shein. Mkutano wa uongozi wa TASWA na  waandishi wa habari umefanyika kwenye mgahawa wa City Sports Lounge jijini Dar es salaam1Makamu mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari za Michezo TASWA Bw. Egbert Mkoko  katikati akielezea mambo mbalimbali yatakayojiri katika tuzo hizo wakati akiongea na waandishi wa habari leo kushoto ni Katibu Mkuu wa TASWA Amiri Mhando na kushoto ni Mjumbe wa TASWA Mwani Nyangasa.
……………………………………………………………………………………..
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania Ijumaa wiki hii.
 
Tuzo hizo zinaandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na mwaka huu zimedhaminiwa na Selcom Wireless, Said Salim Bakhresa & Co Ltd – Bakhresa Group, IPTL, mifuko ya hifadhi ya jamii, PSPF na NSSF.
 TASWA inaishukuru Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano wake na kukubali Rais Dk. Shein aje katika tuzo zetu, ambazo zitafanyika ukumbi wa Diamond Jubilee, VIP Dar es Salaam.
 
Kukubali kwa Dk. Shein kuwa mgeni rasmi kunaonesha jinsi gani alivyokuwa mwanamichezo wa kweli na mwenye nia ya dhati ya kushirikiana na wadau wa michezo nchini.
 Wanamichezo 44 wanatarajiwa kupewa tuzo siku hiyo baada ya kufanya vizuri katika michezo mbalimbali kuanzia Juni 2013 hadi Juni 2014. Pia itatolewa Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa jumla na Tuzo ya Heshima.
 
TASWA imewahi kutoa Tuzo ya Heshima kwa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, pia imewahi kutoa Tuzo ya Heshima kwa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ iliyokuwa ikicheza mechi za kufuzu fainali za mataifa ya Afrika mwaka 1980 zilizofanyika Lagos, Nigeria.
 
 Tunaamini zitakuwa tuzo za aina yake, ambapo tayari Kamati ya Kusimamia Tuzo hizo imeshatangaza majina ya wanamichezo zaidi ya 100 wanaowania tuzo mbalimbali.
==============================================================

FID-Q AZINDUA KAMPENI YA KUHAMASISHA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA MCHAKATO WA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA TAIFA LETU.

01Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Farid Kubanda Fid Q akizungumza na waandishi wa habari kwenye mgahawa wa City Sports Lounge wakati akitangaza kuanza kwa kampeni maalum ya kuhamasisha vijana kushiriki katika chaguzi mbalimbali kwa njia ya matamasha inayoitwa(#Tuo8January).  ambayo itaanza jumamosi mkoani Njombe  kutoka kulia ni Promota  Tale Msanii Dito na kutoka kushoto ni mtayarishaji wa muziki  Lamar Fishcrabmusic na Promota Said Fella wakiwa katika mkutano huo. 02Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Farid Kubanda Fid Q akizungumza na waandishi wa habari kwenye mgahawa wa City Sports Lounge wakati akitangaza kuanza kwa kampeni maalum ya kuhamasisha vijana kushiriki katika chaguzi mbalimbali kwa njia ya matamasha inayoitwa(#Tuo8January).  ambayo itaanza jumamosi mkoani Njombe  kutoka kulia ni Promota  Tale Msanii Dito na kutoka kushoto ni mtayarishaji wa muziki  Lamar Fishcrabmusic na Promota Said Fella wakiwa katika mkutano huo.
……………………………………………………………………………………………..
Msanii nguli wa miondoko ya Hip-hop Fareed Kubanda – Fid Q amekutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sports Lounge katikakati ya jiji la Dar es Salaam, kujadili maswala ya msingi yenye mustakabali chanya kwa maendelo ya taifa hili. Ameitisha mkutano huu akiwa kama kijana na mwenye nafasi na ushawishi kwa vijana wenzie katika ushiriki wa kuleta mabadiliko chanya na maendeleo ya nchi yetu. Fid Q amesukumwa kuzungumza na waandishi wa habari baada ya kutanabai kwamba vijana japo ni asilimia 80 ya taifa lakini hawana mwamko na msukumo wa kujitokeza kushiriki mchakato wa uchaguzi wa viongozi waowataka na wanaowaamini wanauwezo wa kuleta mabadiliko ya ki nidhamu kwenye masuala ya msingi ya taifa letu. “Kuna kitu kimoja ambacho watu wengi hasa hasa vijana wenzangu hawakifahamu, Nchi yetu ni changa sana. Vijana nchi hii chini ya umri wa miaka 35 ni zaidi ya asilimia 80 ya idadi ya watu, wakati watu wazima zaidi ya miaka 60 ni asilimia chini ya 5 ya watanzania wote. Hizi ni takwimu za sensa iliyopita. Nimetanguliza takwimu mapema kwa sababu, twakimu huwa hazisemi uwongo. Changamoto zinalolikumba taifa hili kwa kiasi kikubwa zinatuathiri sisi vijana wa nchi hii ambao ndio wengi wetu. Madhara yanayotokana na uongozi mbovu, vile vile yanatuathiri sana sisi vijana kwa wingi wetu. Tutake tusitake, ustawi na kunawiri kwa vijana ndio kutaamua mustakabali wa Tanzania, vijana tukilala basi na Tanzania pia italala.” Alisema Fid Q. Bado kuna changamoto ya upatikanaji wa ajira kwa vijana. Vijana wengi wamezagaa mitaani bila shughuli za kufanya. Hata wale wenye degree hawana kazi. Vijana wanakata tama na kuona kwamba wao sio sehemu ya taifa hili. Kuna changamoto ya viongozi waadilifu watakaosimamia kuhakikisha kwamba keki ya taifa inagawanywa kwa Watanzania wote na hailiwi na wachache. Baada ya utangulizi huo, ni dhahiri kwamba kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa unaoendelea, na uchaguzi mkuu wa 2015 lazima vijana tuamke na tushiriki kikamilifu. Kwanza, vijana wenye uwezo na sifa za kugombea nafasi za uongozi ni lazima wafanye hivyo, pili vijana wenye vigezo vya kupiga kura pia ni lazima wafanye hivyo maana ni wajibu wetu, tatu, vijana ni lazima tushiriki kikamilifu katika mchakato wa kampeni ili kuhakikisha ishu zetu za msingi zinajadiliwa na wagombea na zinapewa kipaumbele. Kama vijana wanakuwa na hofu basi niwakumbushe kwamba, Mwalimu Nyerere alikabidhiwa nchi hii akiwa na miaka 39 tu na kuanza harakati za kupigania Uhuru ambao tumeuenzi jana. Alikuwa ni kijana mdogo tu. Mzee wetu Dr. Salim Ahmed Salim alianza kuwa mwanadiplomasia mahiri akiwa na rika dogo tu, akiwa na umri wa miaka 22 alikuwa Balozi wa Tanzania, nchini Misri. Mifano ipo mingi, hivyo vijana tusipate woga – Tumechangia kupatikana kwa Uhuru na kujenga nchi hii, na sasa ni wakati mwingine tena wa kuibadilisha nchi yetu. “Hivyo mimi Fareed Kubanda, nimeamua kufanya matamasha ili kusimamia haya niliyoyasema hapo juu. Kwa kutumia nafasi zenu ndugu wana habari naomba mnisaidie kutangaza azma yangu hii pamoja na nitawapigia baadhi ya wasanii wenzangu kuwaomba waniunge mkono ili tufanikishe hili na tushiriki katika kuleta uongozi utako leta mabadiliko tunayoyataka na kwa kasi yetu sisi vijana.” Fid Q aliendelea “Ninatumaini kwamba wasanii wenzangu wataniunga mkono, ili kuanza kuwaamsha vijana wenzetu, tuweze kutimiza wajibu wetu wa kihistoria wa kufanya mabadiliko katika nchi yetu, hasa pale tunapokuwa tunahitajika sana na jamii. Tayari nimefanya mazungumzo na Mkubwa Fela, Babu Tale, Mwana FA, Nick wa Pili, Lamar, P-Funk, Mwasiti, Barnaba, Ditto ambao wamekubali kuwa sehemu ya harakati hizi. Bado nahitaji wasanii wengine wengi washiriki ki mawazao, hali na mali kufikia lengo kuu la Tanzania mpya na bora zaidi”. Huu ni mwanzo wa harakati hizi, mwakani tutafanya amsha amsha kubwa ya vijana. Mwaka huu tunasema Tuonane January (#Tuo8January). Tutengeneze nchi yetu!! Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania!
===========================================================

TAMASHA LA WAFALME KUWEKA HISTORIA SIKUKUU YA XMAS DAR LIVE


================================

COASTAL YASHUSHA KOCHA MPYA WA MAKIPA.

indexNA MWANDISHI WETU,TANGA.

Katika kuimarisha Benchi la Ufundi  Klabu ya Coastal Union ya Tanga,umeingia mkataba wa mwaka mmoja  na aliyekuwa kocha wa makipa wa Yanga,Mfaume Athumani Samata ili kuweza kuwanoa makipa wa kikosi hicho.
Akizungumza leo ,Ofisa Habari wa Coastal Unioon  amesema kuwa kocha huyo anachukua mikoba ya Razack Siwa aliyewahi kuwanoa makipa wa timu hiyo kabla ya kuondoka.
Assenga amesema kuwa kocha huyo aliwahi kuzifundisha timu za soka Yanga ,Ashanti United na Timu ya Taifa ya Vijana U-20 wana matumaini makubwa sana ataimarisha safu ya walinda milango kwenye kikosi hicho ili kuweza kukipa mafanikio.
Akizungumzia mipango yake mara baada ya kutua kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyokuwa yakiendelea jana kwenye viwanja wa Disuza jijini Tanga,Kocha Mfaume alisema kuwa malengo yake makubwa ni kuhakikisha kikosi cha timu hiyo kinashika nafasi za juu kwenye michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara.
Kocha huyo ndio aliyeiongoza timu ya Yanga kufungwa goli saba mpaka ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ilipomalizika akiwanoa makipa kama vile Mustapha Barthezi na Yaw Berko.
=================================================================

MARTHA MLATA AMWAGA SOLA SEKONDARI YA MKALAMA

Na mwandishi wetu
KERO ya maji safi na salama katika Shule ya Sekondari ya Nduguti wilayani Mkalama, imeanza kupatiwa ufumbuzi baada ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Martha Mlata, kubeba jukumu la kusaidia.

Martha, ambaye amekuwa akishiriki kwenye kusaidia huduma za kijamii kuhususan elimu na afya, ametosa sh. Milioni tatu katika kuhakikisha kero hiyo inapatiwa ufumbuzi.
Awali, wanafunzi walikuwa wakilazimika kukatisha masomo kwa saa 40 kwa mwezi ili kufuata maji umbali mrefu hivyo kukosa masomo.
Akizungumza kwenye mahafali ya Sita ya Shule hiyo ambapo mgeni rasmi alikuwa Martha, Mkuu wa Shule Frank Malile, alisema tatizo la maji limekuwa sugu shuleni hapo.
Hata hivyo, alipongeza msaada huo wa Martha akisema utasaidia kupunguza kero hiyo na kwamba, ni mwanga wa kuelekea kwenye mafanikio ya kero hiyo kubaki historia.
“Shule yetu inakabiliwa na tatizo sugu la maji ambalo hukwmisha shughuli ikiwemo chakula kwa wanafunzi. Maji hufuatwa umbali mrefu na baadhi ya visima yanapopatikana ni vya wazi hivyo kuhatarisha usalama wa wanafunzi wetu,” alisema.
Changamoto nyingine iliyowasilishwa mbele ya Martha ni uhaba wa nyumba za walimu, mabweni ya wanafunzi kutokuwa na madirisha, vitanda, vyoo na ukosefu wa jengo la utawala.
Akizungumza kabla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu, Martha alisema nyumba za walimu pamoja na umaliziaji wa majengo ya bweni la wanafunzi wa kike, nguvu za kila mzazi na mlezi zinahitajika.
Pia aliahidi kuwasiliana na uongozi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), ambayo imejikita zaidi kuhakikisha mabweni kwa ajili ya wanafunzi wakiwemo wa kike yanajengwa katika shule mbalimbali nchini.
Martha alisema TEA imeonyesha nia ya dhati ya kuanza kujenga mabweni 30 kwa ajili ya wanafunzi wa kike, ambao ni wahanga wa vitendo viovu katika jamii.
“Serikali imeamua kulivalia njuga suala hili kukomboa mtoto wa kike kutokana na vikwazo anavyopata katika elimu vikiwemo mila potofu kuwatumia watoto wa kike kama chombo duni kisicho na msaada.
Katika mahafali hayo, mbali na kukabidhi sh. Milioni tatu taslim mbunge huyo, miti 50 ya miembe kwa ajili ya kuimarisha mazingira, vifaa vya michezo kwa shule za wanawake na wanaume.
Pia, alikabidhi sola 19 ambazo zitasambazwa kwenye sekondari za kata kwa ajili ya kuwezesha wanafunzi kusoma nyakati za usiku.
===================================================================

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

uuuuuuuuuuu
MTU MMOJA MKAZI WA CHAPWA – TUNDUMA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA JULIUS LABISON HAONGA (34) AMEFARIKI DUNIA BAADA YA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.317 CNS AINA YA MITSUBISHI FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA JOACHIM MKENYA KUACHA NJIA NA KISHA KUPINDUKA ENEO LA CHAPWA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 09.12.2014 MAJIRA YA SAA 09:00 ASUBUHI HUKO MAENEO YA CHAPWA – TUNDUMA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO NA JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WATAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA/KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE. TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU AMBAO NI 1. ATUPAKISYE KAJOLO (22) MKAZI WA KIJIJI CHA BUTULO-MBOYO 2. LWITIKO SIMON (25) MKAZI WA KIJIJI CHA IBILILO NA 3. ESSAU JOHN (32) MKAZI WA KYIMO WAKIWA NA BHANGI UZITO WA KILO MOJA [1KGM] IKIWA KWENYE MFUKO WA RAMBO.
WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 09.12.2014 MAJIRA YA SAA 14:30 MCHANA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KATIKA ENEO LA KIWIRA, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na: [AHMED Z. MSANGI – SACP] KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
=============================================================

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMUWAKILISHA RAIS JAKAYA KIKWETE KWENYE MKUTANO WA MAZINGIRA LIMA PERU

unnamed
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wenzake wakati walipohudhuria katika Mkutano wa 20 wa Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, unaoendelea Jijini Lima nchini Peru, ambapo  alizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika kuhusu utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi. Pamoja na mambo mengine Dkt. Bilal alizungumzia namna nchi za Afrik zilivyojizatiti katika maazimio mbalimbali yanayolenga kunusuru majanga yatokanayo na Tabianchi. Picha na OMR unnamed1 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika Mkutano wa 20 wa Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, unaoendelea Jijini Lima nchini Peru. Makamu wa Rais alizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika kuhusu utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi. Pamoja na mambo mengine Dkt. Bilal alizungumzia namna nchi za Afrika zilivyojizatiti katika maazimio mbalimbali yanayolenga kunusuru majanga yatokanayo na Tabianchi. Picha na OMR unnamed3 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika Mkutano wa 20 wa Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, unaoendelea Jijini Lima nchini Peru. Makamu wa Rais alizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika kuhusu utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi. Pamoja na mambo mengine Dkt. Bilal alizungumzia namna nchi za Afrika zilivyojizatiti katika maazimio mbalimbali yanayolenga kunusuru majanga yatokanayo na Tabianchi. Picha na OMR unnamed4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mjumbe maalum wa Marekani katika masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi, Todd Stern, baada ya kuhudhuria katika Mkutano wa 20 wa Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, unaoendelea Jijini Lima nchini Peru, ambapo  alizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika kuhusu utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi. Pamoja na mambo mengine Dkt. Bilal alizungumzia namna nchi za Afrika zilivyojizatiti katika
maazimio mbalimbali yanayolenga kunusuru majanga yatokanayo na Tabianchi. Picha na OMR
unnamed5 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipiga picha ya kumbukumbu na Mkuu wa Ujumbe wa China, katika mkutano wa Mkutano wa 20 wa Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, Xie Zhenhua, wakati walipokutana kwa mazungumzo baada ya kuhudhuria na kuhutubia katika mkutano huo unaoendelea Jijini Lima nchini Peru, ambapo  alizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika kuhusu utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi. Pamoja na mambo mengine Dkt. Bilal alizungumzia namna nchi za Afrik zilivyojizatiti katika maazimio mbalimbali yanayolenga kunusuru majanga yatokanayo na Tabianchi. Picha na OMR unnamed6 Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya Mawaziri wakati wakitoka katika chumba cha mkutano huo. Picha na OMR unnamed7 Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya Mawaziri wakati wakitoka katika chumba cha mkutano huo. Picha na OMR unnamed8 0Picha ya kumbukumbu na wadau wa masuala ya mazingira walipokutana katika viwanja vya kumbi hizo za mikutano. Picha na OMR
……………………………………………………………………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal jana Desemba 09, 2014 amemuwakilisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni Mwenyekiti Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali Barani Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi, kwenye mkutano wa Kimataifa wa Mazingira Duniani (Cop20) unaofanyika jijini Lima, Peru.
 
Pamoja na shughuli nyingine ambazo zimemuhusisha Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal katika Mkutano huo ikiwa pamoja na kuwa eneo la Mazingira nchini liko chini ya Ofisi yake, Mheshimiwa Dkt, Bilal alipata fursa ya kutoa hotuba kwa niaba ya Wakuu wa Nchi za Afrika siku ya Ufunguzi wa Mkutano huo, huku akisisitiza katika hotuba hiyo umuhimu wa kila nchi kushiriki katika kukabiliana na hali ya mabadiliko ya tabia nchi na tena akaelezea kuwa, hakuna anayeweza kupona kwa kujificha ama kuachia kazi hii ifanywe na nchi baadhi na akaongeza kuwa, wanaochangia kwa kasi kubwa kuathiri mazingira wanatakiwa 
kutambua kwamba wanayoyafanya hayatawanufaisha milele hivyo nao washiriki kwa vitendo katika kukabiliana na janga hili kubwa linaloikumba dunia kwa sasa.
 
Awali akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alieleza kuwa yapo mabadiliko ya tabia nchi ambayo kimsingi yametengenezwa na binadamu wenyewe na kama binadamu wakiamua kukabiliana nayo 
wanaweza kabisa kuyatokomeza. Pia alifafanua kuhusu nadharia ya nchi kushirikiana kwa kuwa mabadiliko haya kwa sasa athari zake hazina mipaka na kwamba nchi zote lazima ziwe katika sehemu ya utatuzi wa tatizo hili kubwa linaloikabili dunia.
 
“Tutumie mapendekezo ya Lima kufungua njia mpya, tuwe na vipaumbele vinavyotekelezeka na kuonekana, Tutoke hapa Lima na twende kuandika historia mpya kwa dunia yetu,” alimalizia Ban Ki-moon.
 
Kwa upande wa Rais wa mkutano huo (Cop20) Manuel Pulgar-Vida ambaye pia ni Waziri wa Mazuingira wa Peru, alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha washiriki wa mkutano huo nchini Peru kwa niaba ya Rais wa nchi hiyo Mheshimiwa Olanta Humala na kisha akafafanua kuwa nchi ya Peru imepitia masaibu kadhaa ya kimazingira na hivyo kupata nafasi ya kuandaa mkutano huu kwao ni heshima na wajibu katika dunia na kwamba anategemea maazimio ya Lima yasaidie dunia katika kukab iliana na tatizo hili 
linalokuwa la mabadiliko ya tabia nchi.
 
Kauli ya Mheshimiwa Manuel Pulgar inasadifu ile aliyoitoa pia  Christiana Fugueres, Katibu Mtendaji wa Umoja wa Mataifa wa Mkakati wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi ambaye aliuambia mkutano huo kuwa, wakati umefika kwa nchi zote kukabiliana na matatizo ya mabadiliko ya tabia nchi kwa pamoja kwa kuwa yanachangia kuongeza umaskini na ili jamii ipate ahueni, basi ni wajibu kwa kila binadanmu kuchukua nafasi yake katika kukabiliana na hali hii iliyopo.
 
Katika tukio jingine, Mheshimiwa Makamu wa Rais alipata fursa ya kukutana na Ujumbe kutoka Marekani uliongozwa na Mjumbe Maalum kutoka Serikali ya Marekani anayehusika na masuala ya Mabadiliko ya Tabia nchi Todd Stern, ambaye alimueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuhusu utayari wa serikali ya Marekani katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi na kwamba nchi yake itashirikiana nan chi zinazoendelea ikiwemo Tanzania katika suala hilo. Vile vile Mheshimiwa Makamu wa Rais alipata nafasi ya kukutana na ujumbe kutoka Jamhuri ya Watu wa China ulioongozwa na Mheshimiwa Xie Zhenhua ambaye alizungumzia kuhusu ushirikiano baina ya nchi zinazoendelea na zile zilizoendelea katika suala la mabadiliko ya tabia nchi na akafafanua kuwa Tanzania na China zina uhusiano wa kindugu hivyo kama kutakuwa na jambo la kipekee baina ya nchi hizi mbili basi serikali ya China iko wazi kulipokea.
 
Mkutano huo pia umehudhuriwa na Rais wa Bolivia Evo Morales, Rais wa Nauru Baron Waqa, Waziri Mkuu wa Tuvalu Enele Sopoaga, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Sam Kutesa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon. Mkutano huu unafanyika wakati dunia ikiwa imeanza kubadili fikra na misimamo kuhusu namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo nchi ambazo awali zilikuwa na misimamo mikali mfano Marekani na China sasa zimaeza kubadili fikra kuhusu suala hili na kwa sasa zinaanza kulipa uzito kutokana na athari yake pia kuzikabili nchi hizo.
Pamoja na Mheshimiwa Makamu wa Rais msafara wa Tanzia pia unawashirikisha Mawaziri Bilinith Mahenge (Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira) Waziri Fatma Fereji (Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais SMZ), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Juma Maalim pamoja na wataalam wengine wa masuala ya Mazingira na Maliasili pamoja na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
=====================================================================

WAFINYANZI WAOMBA MSAADA WA VIFAA VYA KISASA

DSC_0908Mratibu wa Mradi wa Ukimwi ILO, Getrude Sima (kushoto) akitoa maelezo ya kikundi cha kina mama ambao ni walengwa wa mradi wa Ukimwi unaofadhiliwa na SIDA chini ya shirika la kazi duniani (ILO), kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, katika ziara ya kikazi ya kutembelea miradi inayosaidiwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Iringa na Njombe. Kulia ni Practice Specialist HIV/AIDS, Dr Bwijo Bwijo.
Na Mwandishi wetu, Iringa
KIKUNDI cha wafinyanzi wanawake cha Lungemba,kilichopo Wilaya ya Iringa, wameomba kusaidiwa vifaa vya kisasa vya ufinyanzi, ili waweze kutengeneza vitu bora vitakavyokubalika katika soko.
Maombi hayo wameyatoa katika risala yao kwa Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Alvaro Rodriguez.
Mratibu huyo alikuwa katika ziara ya kikazi ya kutembelea miradi inayosaidiwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Iringa na Njombe.
Makundi yaliyotembelea ni yale ya ujasiriamali, yanayosimamiwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) chini ya mpango wa Kupunguza Maambukizi ya UKIMWI kwa Njia ya Uwezeshaji wa Kiuchumi kwa Wafanyakazi walio katika Sekta Isiyo Rasmi kando kando mwa Barabara Kuu iendayo Tanzania-Zambia maarufu kama “Corridor Economic Empowerment Project (CEEP) “
Aidha makundi mengine yaliyotembelewa ni ya wakulima wanaosaidiwa pembejeo na wanaotengeneza vikapu na kufanya shughuli binafsi ikiwamo mabucha.
DSC_0920 
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa amembeba mtoto wa mwanachama wa Mtwango SACCOS ya wilaya ya Njombe.
Mmoja wa wanachama hao Anna Nyongole alisema wanafanya kazi hiyo katika mazingira magumu, kwani bado wanatumia mikono pekee, badala ya kutumia vifaa vya kisasa, na hivyo kusababisha bidhaa zao kukosa ushindani katika soko jambo linalowadumaza kiuchumi.
“Tunatengeneza vyungu, sufuria, majiko, mitungi ya maji na ya maua, na vitu mbalimbali, lakini changamoto yetu kubwa ni namna tunavyotengeneza, kwani hatuna mashine za kutengenezea vitu hivyo wala mitambo ya kuchomea, tunaiomba serikali na wadau wa maendeleo nchini watusaidie, kwani tukipata vifaa vya kisasa tutaweza kutengeneza vitu vingi kwa muda mchache kuliko ilivyo sasa,” alisema Nyongole.
Naye Zena Omary amesema kukosekana kwa usafiri wa gari kwenda kusomba udongo wa kufanyia ufinyanzi kunawafanya kutembea umbali wa kilomita 40 kwenda na kurudi, kutoka katika eneo la Ikekeke katika kijiji cha Kitelewasi.
DSC_0904Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na Wanchama wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo kinachofadhiliwa na SIDA chini ya Shirika la kazi Duniani (ILO).
“Tunakokwenda kuchimba udongo ni Ikekeke katika kijiji cha Kitelewasi, tunatembea kilomita 20 kwenda na kurudi kilomita 20, kwa hiyo unajikuta siku moja umeshindia kuchimba udongo na kusomba tu, na kwa kuwa tunajitwisha kichwani, huwezi kuchukua udongo mwingi,” alisema Zena.
Licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali, akinamama hao wamesema kupitia mafunzo ya UKIMWI na Ujasiriamali waliyopata kutoka ILO wameweza kuboresha biashara hiyo ya ufinyanzi kwa kujenga banda la kuhifadhia bidhaa hizo, kuweka akiba na kukopeshana katika kikundi hatimaye wamefanikiwa kuyabadili maisha yao kwa kujenga nyumba bora na hata kuwasomesha watoto wao kwa kumudu gharama za ada.
“Hapa kila mmoja wetu anayo nyumba ya kisasa ya tofali za kuchomwa na iliyoezekwa kwa bati, na pia tumefanikiwa kusogeza huduma ya maji ya bomba katika nyumba zetu, ili kupunguza usumbufu wa kuchota maji visimani… kwa kweli biashara hii ya ufinyanzi imetusaidia lakini tukiboreshewa zaidi mazingira tutakua zaidi kiuchumi,” Walisema.
DSC_0932Msafara wa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez ukiongozwa na Mratibu wa Mradi wa Ukimwi ILO, Getrude Sima (kushoto) kuelekea kukagua baadhi ya miradi inayofadhiliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa wilayani Njombe.
Hata hivyo Umoja wa Mataifa UN kupitia Shirika la Kazi Duniani “ILO” Kwa mkoa wa Iringa pekee- limefanikiwa kuwafikia akinamama na vijana wapatao 1,000 wa vikundi mbalimbali vya kiuchumi na vyama vya Kuweka na Kukopa (SACCOS), huku wanachama wa vikundi hivyo wakipatiwa mikopo, Elimu ya Maambukizi Virusi vya UKIMWI, pamoja na mafunzo ya Ujasiriamali.
Mratibu huyo alitembelea vikundi hivyo kuona namna msaada wa Umoja wa Mataifa ulivyobadili maisha ya wahusika ambao walikuwa katika mazingira magumu hapo awali.
Makundi mengine yaliyotembelewa yapo Nyololo na pia hospitali ya Mafinga ambako kuna mafunzo yanayoendeshwa kwa ajili ya ushauri nasaha kwa wanawake wenye kuishi na VVU.
Miradi hiyo ambayo mashirika ya UNICEF na IFAD yanashiriki, imelenga kusaidia makundi hata yale yenye wanachama wanaoishi na virusi vya ukimwi kujitambua na kuishi kwa kujitegemea.
DSC_0926Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kwenye picha ya pamoja na kikundi cha kinamama wa Nyololo wanaotengeneza vikapu.
DSC_0935Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akicheza na baadhi ya watoto yatima wa kituo cha Nyololo Centre ambao wengine wakiwa ni ndugu wa wakinamama wanaosaidiwa na ILO.
DSC_0946Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akikagua shamba la Mradi wa miche na matunda ambalo linasimamiwa na wanawake wa kikundi cha Nyololo wanaofadhiliwa SIDA chini ya shirika la kazi duniani (ILO).
DSC_0952Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akishiriki kupanda mti kwenye shamba hilo kama kumbukumbu wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi inayosaidiwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Iringa na Njombe.
DSC_0954
DSC_0965Katibu wa Kikundi cha wafinyanzi wanawake cha Lungemba, Bi. Leokadius Mfukwe akisoma risala ya kikundi chao na changamoto zinazowakabili mbele ya Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (mwenye miwani) alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kutembelea miradi inayosaidiwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Iringa na Njombe.
DSC_0967Baadhi ya vyungu vinavyotengenezwa na kikundi hicho.
DSC_0974

=====================================

TIMU YA EALA WAICHAPA BURUNDI 4-2

SAM_0035
Wachezaji wa Timu ya EALA waliovalia jezi rangi ya blue wakipambana na wenzao timu ya Burundi
Timu ya wabunge wa EALA wameicharaza mabao manne kwa mbili timu ya Burundi jana katika Uwanja Sheikh Amri Abeid  jijini Arusha ikiwa ni muendelezo wa mashindano ya wabunge Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
Mchezaji mahiri wa timu ya Eala John King aliipatia mabao 3 timu yake dakika ya 9 na 21 kipindi cha kwanza hali iliyosabaisha mashabiki waliomiminika katika uwanja huo kumshangila Kipindi cha pili hali ilibadilika  baada ya timu ya Burundi kujipatia mabao mawili  dakika ya nne na dakika ya 18, mpigaji wa magoli hayo ni Simon Gahinja
Baada ya mchuano mkali wa timu zote mbili ,Eala waliongeza bao la 4 lililofungwa na mchezaji Wilyclif Keto dakika ya 25 baada ya kupata penalt dakika 33  ambapo mpigaji penalt alikosa baada ya mlinda mlango wa Burundi Ibrahim Uwizey kudaka
SAM_0039
Mbunge wa EALA kutoka nchini Tanzania Mh.Twaha Taslama jezi namba 12 akiwa uwanjani
SAM_0038
Mh Mbunge wa Eala Bernad Mrunya akiwa anajiandaa kukabilia na timu ya Burundi katika Uwanja Sheikh Amri Abeid  jijini Arusha ikiwa ni muendelezo wa mashindano ya wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
(Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog Arusha)
====================================================================

LA VEDA: IDRIS, FEZZA KESSY NA DIAMOND WAMETOA GUNDU KWA WASANII WA BONGO


La Veda baada ya kuwasili jijini Dar akitokea nchini Afrika Kusini alipokwenda kushiriki fainali za BBA.
La Veda akipokelewa baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.


La Veda akipozi na baadhi ya wadau waliofika kumpokea.
MWANADADA, aliyeiwakilisha Tanzania katika shindano la Big Brother Hotshots, Irene Neema Vedastous ‘LA VEDA’ amefunguka kuwa Diamond, Fezza na Idris wameondoa gundu kwa ushindi wao.
Akizungumza na GPL leo jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wakati akiwasili kutoka Afrika ya Kusini alipokwenda kuungana na washiriki wengine wa BBA katika fainali, La Veda alisema,
“Binafsi nimefurahi sana kwa Idris kushinda Dola za Kimarekani 300,000, ni furaha kubwa sana kwangu na kwa Watanzania kwani naamini pia Diamond kuchukua tuzo tatu za Channel O na nyingine aliyopata juzi kutoka Nigeria, Fezza kuingia tena mjengoni wote watakuwa wameondoa gundu kwa wasanii wa Kitanzania’, alisema.
Aidha La veda amewaomba Watanzani kujitokeza kwa wingi kumpokea Idris siku atakapowasili maana ushindi wake unazidi kuiweka Tanzania katika ramani nzuri kimataifa.
Kujua zaidi Mahojiano aliyofanya La Veda baada ya kuwasili, usikose kutembelea www.globaltvtz.com
(PICHA / HABARI: Na Gabriel Ng’osha/GPL)
====================================================================

SHEREHE ZA UHURU MIAKA 53 UWANJA WA UHURU LEO

unnamed Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mikono wananchi waliofurika  katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara akiwa katika Gari maalum liliozunguuka katika uwanja huo leo. [Picha na Ikulu.] unnamed1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mikono wananchi waliofurika  katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara akiwa katika Gari maalum liliozunguuka katika uwanja huo leo. [Picha na Ikulu.] unnamed2 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mikono wananchi waliofurika  katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara akiwa katika Gari maalum liliozunguuka katika uwanja huo leo. [Picha na Ikulu.] unnamed4Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikitoa salamu ya heshma wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam leo katika sherehe  za kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara, [Picha na Ikulu.] unnamed5Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Viongozi wa Kitaifa wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika kilele cha sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, [Picha na Ikulu.] unnamed7Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lilioandaliwa katika sherehe za kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, [Picha na Ikulu.] unnamed8Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lilioandaliwa katika sherehe za kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, [Picha na Ikulu.] unnamed9Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Makamo wa Pili wa  Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,[Picha na Ikulu.] unnamed10 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Mama Salma Kikwete akisalimiana na Makamo wa Pili wa  Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,[Picha na Ikulu.] unnamed11Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Mama Salma Kikwete akisalimiana na Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,[Picha na Ikulu.]
unnamed12Baadhi ya wananchi kutoka mitaa mbali mbali ya Jiji la Dar es Salaam na Mikoa jirani wakiwa katika   Uwanja wa Uhuru  Jijini Dare Salaam katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambazo hufanyika kila mwaka,[Picha na Ikulu.] unnamed13Mabalozi  wa Nchi mbali mbali wanaoziwakilisha Nchi zao hapa nchini pamoja na Wananchi wakiwa katika Sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika Uwanja wa Uhuru  ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, [Picha na Ikulu.] unnamed14Mabalozi  wa Nchi mbali mbali wanaoziwakilisha Nchi zao hapa nchini wakiwa katika Sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, [Picha na Ikulu.]

No comments:

Post a Comment