TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, December 11, 2014

Wizara ya Fedha yahitimisha mashindano ya Tamasha la Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne.

unnamedMkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwansoko akitoa hotuba wakati wa kufunga Mashindano ya Tamasha la Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha kwa kushikiana na Taasisi zake liLIlofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es salaam.
unnamed2Meneja Mawasiliano Jamii kutoka Mfuko wa Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-T) Margaret Mussai akifafanua jambo kwa Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwansoko wakati wa kufunga Mashindano ya Tamasha la Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne yaliyofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombekuanzia Disema 6-9 mwaka huu jijini Dar es salaam ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
unnamed4Mwongoza kwaya (conductor) kutoka kwaya Wizara ya Fedha makao makuu Revocatus Mtiro (kushoto) akipokea kombe la ushindi wa kwanza kutoka kwa Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwansoko wakati wa kufunga tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es salaam. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (GCU) Ingiahedi Mduma.
unnamed5. Meneja Mawasiliano Jamii kutoka Mfuko wa Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-T) Margaret Mussai akifurahia kombe la ushindi kwa upande wa maonesho kupitia mabanda alilopokea kutoka kwa Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwansoko wakati wa kufunga tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es salaam. 
unnamed7Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwansoko (katikati) akimkabidhi Charles Maganga (wa kwanza kushoto) kombe la ushindi wa sanaa ya maigizo wakati wa kufunga tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es salaam.
unnamed9Washindi wa kwanza wa kwaya kutoka kwaya Wizara ya Fedha makao makuu wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwansoko (katikati mstari wa nyuma waliosimama) mra baada ya kutoa zawadi kwa washindi mbalimbali wakati wa kufunga tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment