TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, December 12, 2014

POLISI YAONYWA WATAKAOLETA FUJO WAKATI WAKAMPENI NA WAKATI WA KUPIGA KURA

index
Na Kibada Kibada Katavi
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi limeonya kuwa halitasita kuwachukulia   hatua kali  za kisheria kwa mtu yeyote au kikundi cha chochote cha watu watakaojihusisha na Vitendo vya Vurugu, fujo ama  Vitisho vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani wakati wa zoezi zima la uchaguzi wa viongozi  wa Serikali za mitaa.
Kamanda wa  Polisi Mkoani Katavi Kamishina Msaidizi wa Polisi Dhahiri Kidavashari katika Taarifa yake kwa vyombo vya Habari ameeleza  kuwa Jeshi limejipanga vizuri kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na Usalama kuhakikisha kwamba hakuna vitendo vyovyote  vya uvunjifu wa amani vitakavyojitokeza  wakati wa Kampeni na hata siku ya kupiga kura na pale ambapo vitajitokeza vitadhibitiwa kwa haraka na wahusika kukamatwa na sheria kuchukua mkondo wake.
Amesema ulinzi umeimarishwa katika maeneo yote  na wananchi wasiwe na hofu, katika kipindi hiki chote cha kampeni za uchaguzi wa serikali za Mitaa na hasa siku ya upigaji kura.
Kamanda Kidavashari akawashauri wale wote waliojiandikisha kupiga kura wajitokeze siku ya kupiga kura bila hofu ya aina yeyote. Na kusisitiza kuomba ushirikiano kwa jamii na kutoa taarifa za mtu ama vikundi vya aina yeyote vinavyojihusisha na vitendo vya vitisho ,vurugu na fujo dhidi ya wananchi waliojiandikisha kupiga kura ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao mapema.
Katika hatua nyingine kampeni za kuwanadi wagombea kwa vyama vyote mkoani katavi zimeendelea huku kukiwa kunaripotiwa kuwepo kwa dallili za makundi Fulani kujipenyeza kutaka kuvuruga uchaguzi siku ya kupiga kura hata hivyo atakayekamatwa atashughulikiwa kwa mjibu wa sheria za nchi.

No comments:

Post a Comment