TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, December 13, 2014

Mgodi wa Resolute wakabidhi eneo la Mgodi kwa Chuo cha Madini Dodoma, Masele asema tukio hilo limefungua ukurasa mpya

unnamedNaibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Stephen Masele (aliyesimama katikati) akishuhudia halfa fupi ya kusaini makabidhiano ya eneo la Mgodi wa Resolute kwa Chuo cha Madini Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma, Mjiolojia Mwandamizi Subian Chiragwile, katikati ni Kaimu Kamishna wa Madini Mhandisi Ally Samaje, na kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Resolute Peter Beilby. Wengine wanaoshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Nzega Bintuni Msangi (wa pili kuchoto aliyesimama),Mkurugenzi Kampuni ya Resolute Rose Aziz na baadhi ya waliohudhuria.
unnamed1Meneja Mazingira   baada Mgodi wa Resolute Jackie Sinclair (Kulia), akimkabidhi funguo mbalimbali za majengo ya eneo la mgodi wa Resolute Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini) Stephen Masele (Kushoto) mara makabidhiano ya eneo la mgodi.
unnamed2Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma Mjiolojia Mwandamizi Subian Chirangilwe funguo mbalimbali za majengo ya mgodi wa Resolute kwa ajili ya Chuo cha Madini Dodoma.
unnamed6Meneja Mazingira wa Mgodi wa Resolute Jackie Sinclair akikabidhi moja ya vifaa ambavyo vitatumiwa na Chuo cha Madini Dodoma kwa wanafunzi kujifunza kwa vitendo wakati wa halfa ya kukabidhiana eneo la mgodi wa Resolute. Wanaoangalia kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele, Kaimu Kamishna wa Madini Mhandisi Ally Samaje na Mkuu wa Wilaya ya Nzega Bintuni Msangi
unnamed7Sehemu mgodi ambao shughuli za uchimbaji zilikuwa zikifanywa na mgodi wa Resolute ambao pia umekabidhiwa kwa Chuo cha Madini Dodoma. Kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo Madini Dodoma Mjiolojia Mwandamizi Subian Chirangilwe ameeleza kuwa,mgodi huo utatoa fursa kwa wanafunzi kujifunza kwa vitendo kuhusu shughuli za uchumbaji.
…………………………………………………………………………..
Na Asteria Muhozya, Nzega Mgodi wa Resolute uliopo Wilayani Nzega Mkoani Tabora jana tarehe 12 Desemba, 2014, ulikabidhi eneo la Mgodi kwa Chuo cha Madini Dodoma katika hafla fupi iliyofanyika na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia madini Stephen Masele aliyekuwa mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Nzega aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Bituni Msangi, Viongozi Waandamizi wa Wilaya ya Nzega, Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje, Kamati ya Kitaifa ya uchimbaji, Uongozi wa Juu wa kampuni ya Resolute na wananchi. Akihutubia katika hafla hiyo, Naibu Waziri Masele alieleza kuwa, tukio la kukabidhiwa eneo hilo la Mgodi kwa Chuo ni tukio ambalo limefungua ukurasa mwingine kutokana na kwamba Chuo cha Madini Dodoma kitaiwezesha Tanzania kuzalisha wataalamu zaidi waliobobea katika tasnia hiyo ambao mchango wao kwa taifa unahitajika katika kuendeleza sekta ya madini. “Tunataka wanafunzi wasome kwa vitendo, hii itawezesha kupata wataalamu waliobobea. Ni nafasi kwa wanafunzi na Chuo cha Madini kuitumia fursa hii vizuri. Najua kuna mawazo mchanganyiko ya kupoteza mapato kwa Halmashauri na mengine ya kupata Chuo lakini, kufunga mgodi ni sehemu ya Sheria ya madini”, aliongeza Masele. Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nzega Bintuni Msangi, akizungumza katika halfa hiyo, alieleza kuwa, Mgodi wa Resolute una historia ya kuwa mgodi wa kwanza nchini kuzalisha madini ya dhahabu na kuogeza kuwa, ndani ya kipindi cha miaka 12 cha uhai wa mgodi huo umeweza kuchangia kiasi cha shilingi bilioni 290 za Kitanzania ikiwa ni kodi mbalimbali zilizotolewa na mgodi huo kama mrahaba. Aliongeza kuwa, Halmashauri iliweza kupata kiasi cha shilingi bilioni 6 ikiwa ni kodi na kiasi cha Tsh bilioni 6 kilitumiwa na mgodi huo kuwezesha za kijamii ikiwemo ujenzi wa zahanati, shule, upatikanaji wa huduma safi ya maji katika eneo linalozunguka mgodi huo. Pamoja na eneo la mgodi huo kukabidhiwa kwa Chuo cha Madini Dodoma, vilevile mgodi umekabidhi majengo, mitambo, maabara ambapo, kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo cha Madinini Dodoma, Mjiolojia Mwandamizi Subian Chiragwile alieleza kuwa, eneo hilo litatumiwa na wanafunzi wa mwaka wa pili kwa ajili ya masomo ya vitendo. Mgodi wa Resolute umefunga rasmi shughuli zake za uchimbaji madini ya dhahabu katika eneo hilo, ambapo ulianza kazi zake mwaka 1998. Kabla ya makabidhiano hayo, mgodi huo umefanya ukarabati, ujenzi wa madarasa, na uhifadhi wa mazingira.

No comments:

Post a Comment