TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, December 11, 2014

FILIKUNJOMBE AWATIMIZIA AHADI YA MAJI WANANCHI WA KITEWELE ZAIDI YA TSH MILIONI 26 ZATUMIKA

Mbunge
wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe kushoto akikabidhi  masaada wa
vitaa vya  maji  safi  vyenye  thamani ya Tsh milioni 26  kwa wananchi
wa  kijiji  cha Kitewele  kata ya Mawengi Ludewa  leo
Wananchi  wa kijiji  cha  Kitewele  kata ya Mawengi  Ludewa  wakiwa wamebeba bomba za maji  zilizotolewa na mbunge  wao Deo Filikunjombe  kwenda  kijijini kwao umbali  wa  zaidi ya Km 6 kutoka eneo la barabara  ziliposhushwa  bomba  hizo
Wananchi  wa  kijiji  cha Kitelewe wakishiriki kubeba  bomba  za maji zilizotolewa  msaada   na mbunge  wao Filikunjombe
Wannchi  wa Kitewele  wakimpokea mbunge Filikunjombe kushoto
Baadhi ya  wananchi  wa kitewele  wakiwakatika mkutano huo
Wananchi  wakimsikiliza mbunge  wao kwa makini
Mbunge Filikunjombe kulia akijibu swali la mkazi wa kijiji cha Kitelewe  kushoto  huku  wakifurahi wote baada ya majibu mazuri ya kutaka wazee na vijana kuungana kushiriki katika maendeleo
WANANCHI wa Kijiji cha KITEWELE kata ya MAWENGI wilaya ya LUDEWA mkoani Njombe , wanatarajia kuanza kunufaika na huduma ya maji safi na salama ya bomba baada ya kukamilika kwa ununuzi wa vifaa ikiwemo mabomba ya kutandika ardhini ambayo yamegharimu kiasi shilingi zaidi ya Milioni 26  msaada  uliotolewa na  mbunge  wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe .
Akizungumza leo na  wananchi hao mara baada ya  kukabidhi vifaa hivyo  mbunge Filikunjombe alisema  kuwa  kukabidhi kwa  vifaa hivyo na mradi huo wa maji ni utekelezaji wa ahadi yake ya maji kwa  wananchi hao aliyoitoa mwaka 2012 kufiatia ombi  la  wananchi hao zaidi ya 800 waliokuwa  wakikabiliwa na adha ya maji .
Mbunge  Filikunjombe alisema  kuwa  toka  nchi itape uhuru mwaka 1961  wananchi  hao  hawajapata kuwa na maji  safi na  salama na  kuwa  miaka  yote  wamekuwa  wakitumia maji ya mito ambayo  si safi na salama kabla ya  kufika na  kuombwa  kuwasaidia kupata huduma   hiyo ya maji  safi .
“Ndugu zangu nikiwa  kama  mbunge  wenu  nimekuwa  nikiumia  zaidi  kuona  wananchi   wangu  mnapata  shida ya maji na  ndio   sababu ya  kuahidi  kuungana nanyi katika  kuwafikishia  huduma ya maji….ombi langu  kwenu tuzidi  kushirikiana  ili  kutatua  kero  zetu  bila  kusubiri wahisani “
Miaka miwili iliyopita, Mbunge wa Jimbo la Ludewa, DEO FILIKUNJOMBE alishuhudia kadhia hiyo akiwa katika Zahanati ya kijiji hicho na akawaahidi wananchi kuwafikishia maji, ahadi ambayo ameitekeleza mwaka huu na kukabidhi mabomba kwa wananchi yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 tayari kwa kuanza kazi ya kuchimba mitaro na kutandika mabomba hayo.
Hata   hivyo  alisema  kuwa  maendeleo ya  wananchi  wa KItelewe  na  jimbo  la  Ludewa  yataletwa na  wananchi  wenyewe  kwa  kuunganisha  nguvu  zao pasipo  kusubiri  wahisani na kuwa baadhi ya  maeneo ya wilaya  hiyo   wananchi   siku  zote  wamekuwa  wakijitolea  kushiriki katika maendeleo  mbali  mbali.
Akielezea  kuhusu adha ya maji katika  jimbo lake na jinsi  alivyoshiriki  kutatua  alisema  kuwa yapo maeneo ambayo wananchi  wamekuwa na adha kubwa ya maji  na tayari  ameanza  kumaliza kero  hiyo.
Kwa  upande  wake  diwani  wa  viti maalum tarafa ya Mawengi Bilgeter Haule aliema  kuwa moja ya  vitu  ambavyo  wana Ludewa  wanajivunia  ni  kumpata  mbunge ambaye  anawajibika kwa  wananchi kama  ilivyo kwa  mbunge   huyo.
“ Tanzania mtu  ambae hatakuj  kusaulik ni pamoja na baba wa Taifa mwalimu Julius Nyerere ambae  alitanagazwa  kuwa mwana heri ila kwetu  Ludewa kutokana na kero  tulizozipata  toka  uhuru  hadi  leo  ambapo  zinapatiwa ufumbuzi kwa pamoja  tutamkumbuka mheshimiwa  mbunge wetu  Deo Filikunjombe kama mwanaheri baada ya  kutatua  kero  zetu na kuondoka katika kundi  la  watanzania wasiofurahia uhuru  wao”

No comments:

Post a Comment