TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, December 13, 2014

Watakaopamba Tamasha la Krismasi

images
Na Mwandishi Wetu
WAKATI zikiwa zimebaki siku chache kuelekea Tamasha la Krismasi linalotarajia kuanza Desemba 25 kwenye mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, wadau na waumini wa dini mbalimbali hapa nchini  wanatarajia kupokea neno la Mungu kupitia waimbaji wenye mvuto wa aina yake katika muziki huo ambao unafanikisha ukaribu baina ya Binaadamu na Mungu.
Ukaribu huo baina ya binaadam na Mungu pia unafanikishwa kupitia Wachungaji na Maaskofu mbalimbali watakaojitokeza katika tamasha hilo ambalo litafanyika kwenye mikoa ya Mbeya, Iringa na Ruvuma katika Wilaya ya Songea.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions ambayo inaandaa tamasha hilo, Alex Msama maandalizi ya tamasha hilo yamefanyika kwa asilimia kubwa kama viwanja na maeneo mengine muhimu yamekamilika.
“Maandalizi ya Tamasha la Krismasi mwaka huu yamefanyika kwa kiasi kikubwa, hivyo wadau wa muziki huo wajiandae kupokea injili kutoka kwa waimbaji na maaskofu mbalimbali watakaohudhuria,” alisema Msama.  
Tamasha la Krismasi lina lengo la kudumisha amani kwa Tanzania kwani mwaka huu Kauli mbiu  ya tamasha hilo ni “Tanzania ni ya Kwetu, Tuilinde na Tuipenda,” alisema Msama.
Kupitia Tamasha la Krismasi na Pasaka, vituo mbalimbali vya kulelea watoto wenye uhitaji maalum wanapata mahitaji muhimu kupitia viingilio vinavyopatikana.
Kampuni ya Msama Promotions haikuishia hapo imeenda mbali zaidi kwa kuelekeza nguvu zake zaidi kwa kujipanga kwa lengo la kujenga kituo cha Kimataifa katika eneo la Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kitakachojulikana kama Jakaya Kikwete Rafiki wa Wasiojiweza.
 Anasema Tamasha la Krismasi ni zao la Tamasha la Pasaka ambalo limeshika hatamu ya muziki wa Injili Afrika Mashariki na Kati, ambako waimbaji mbalimbali kutoka katika nchi hizo wanashiriki kutoa huduma.
 Aidha Msama anawataja waimbaji watakaopanda jukwaani kwenye tamasha hilo ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Bonny Mwaitege, Emmanuel Mgogo, Fraja Ntaboba, Solomon Mukubwa, Edson Mwasabwite, Upendo Kilahiro, Joshua Mlelwa, Tumaini Njole na Martha Mwaipaja.

No comments:

Post a Comment