TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, January 18, 2014

BABY MADAHA ANASWA LIVE BILA CHENGA AKIFANYA BIASHARA YA NGONO.

AMA kweli maovu yanazidi kuongezeka, shetani naye mbioni siku 
zote kunasa waliyo wake, kauli hizo zote ziko sambamba na staa wa 
sinema za Kibongo na mkali wa muziki wa Kizazi Kipya, Baby Joseph 
Madaha amenaswa baada kuingia mkenge mtego wa kujiuza, Ijumaa limesheheni.
 
 Kumekuwa na skendo kuwa baadhi ya mastaa wa kike Bongo 
hujihusisha na biashara ya kujiuza ili kujipatia kipato na 
kufanya sanaa 
kuwa kama chambo cha kunasa wanaume.
 OFM MZIGONI
Oparesheni Fichua Maovu (OFM) chini ya Global Publishers, mwaka
 jana ilinasa mastaa wawili kwenye mtego wake, mke wa mtu, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ na Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’.
Mwaka huu, OFM imeanza kazi zake ambapo kwa kuanzia iliamua 
kumtega Baby Madaha aliyejaa kwenye kumi na nane zake.
 Mmoja wa wadau wa OFM alijifanya mfanyabiashara kutoka Mwanza ambaye ni mgeni wa jiji a.k.a Ngosha akijipachika jina la Frank ambapo baadaye katika mazungumzo, Baby Madaha alimbana na 
kutaka ampatie majina matatu ndipo mwana-OFM Frank (feki) akajipatia 
jina Frank Michael Lugwisha.
ILIKUWAJE?
Mchezo mzima ulianza Januari 13, mwaka majira ya saa 11:52 
jioni
 kwa kuchati kwenye simu ya kiganjani ambapo Baby Madaha
 aliingia kichwakichwa bila kujua anachati na ‘sumu’ wa OFM kama 
ifuatavyo;
Frank/OFM: Mambo vipi Baby Madaha? Nilikuwa naomba tuonane.
Baby Madaha: Kuhusu nini?
 Frank/OFM: Niwe mkweli, Madaha nimekupenda, nilipofika hapa 
Dar ndo nikaona nikutafute.
Baby Madaha: Unampendaje mtu usiyemjua?
Frank/OFM: Jamani nakuonaga magazetini na video zako.
Baby Madaha: Safi, so unataka kuniambia nini ambacho 
sijakisikia?
 Frank/OFM:  Nataka tu-meet (kukutana) Madaha nimetokea 
kukupenda sana lakini Alhamisi (jana) narudi mkoani Mwanza.
 Baby Madaha: Huwezi ku-manage kuwa na mimi, baki kuwa shabiki 
wangu tu.
Frank/OFM: N’take radhi Madaha, kwa nini nisiweze, kikubwa kipi?
Baby Madaha: Huh! Tuma vocha tuone how worth are you? (Tuma 
vocha tuone utajiri wako)
Frank/OFM: Acha utani bwana, vocha kitu gani, ongea mambo 
makubwa Madaha
Baby Madaha: Hahaha…yote ninayo-except vocha tajiri.
 Frank/OFM: Acha bwana. Vocha ndo kikwazo kwako?
Baby Madaha: Yap! Kama hutaki acha au unadhani natumia wireless kuchati na wewe?
Frank/OFM: Madaha wewe ni mkatili kiasi hicho?
 MAMBO YASIMAMA KWA MUDA
Masuala ya kuchati yalisimama kwa muda lakini ilipofika saa
 2:22 usiku, mazungumzo yaliendelea ambapo siku iliyofuata Frank 
wa 
OFM aliamua kuendelea kumtengenezea mtego ili kujiridhisha kama 
ni 
kweli baadhi ya mastaa wa Bongo wanafanya biashara hiyo haramu.
Januari 14, mwaka huu, majira ya saa 5:00 asubuhi, Frank wa 
OFM alianza tena kuchati na Baby Madaha kama ifuatavyo;
 
 Frank/OFM: Mambo Madaha? Mi Frank
(akaamua kumpigia simu Frank wa OFM, ilikuwa mshtuko kwa Frank 
kwa sababu hakujipanga kuongea naye kwa hiyo hakupokea simu ya 
Baby Madaha ambayo ilipigwa saa 6: 30 mchana.
Dakika moja baadaye, Baby Madaha alituma meseji ya kumtoa hofu 
Frank wa OFM;
Baby Madaha: Frank ‘am calling you in vain uh afraiding of me 
(Frank nakupigia kwa nia njema unaniogopa?)
 Frank/OFM: Sorry nilikuwa tight, naweza kupiga?
Baby Madaha: Yap!
Frank/OFM: Frank wa OFM aliongea na Baby Madaha na kuanza kumchomekea ambapo alitoa ushirikiano wa kutosha na kuonesha 
nia ya kujenga uhusiano huku akimtaka staa huyo kuwa ‘siriaz’ 
akimuahidi kuwa atakuwa naye na kuwa ajenti wake wa muvi jijini Mwanza.
Baada ya maongezi ya kutongozana kwenye simu, Frank wa OFM 
alimtumia tena meseji Baby Madaha kama ifuatavyo;
 
 Frank/OFM: Nimefurahi sana kuongea nawe, sijui itakuwaje
 tukionana?
Baby Madaha: Wait, you I’ll see.
Frank/OFM: Eti ee, nimetokea kukupenda sana.
Baby Madaha: Thanks.
 Baada ya hapo Frank wa OFM alimaliza kumtumia ‘sms’ siku 
hiyo, ilikuwa saa 9:12 alasiri.
Hata hivyo, Frank wa OFM aliamua kumhoji zaidi kupitia sms 
akitaka kujua hasa akiwa naye hata kwa saa tatu atataka shilingi ngapi?
Frank/OFM: Sasa hivi nataka kutoka niende ATM kuchukua pesa, 
sasa hebu kuwa muwazi tu wangu, kuwa na wewe kwa kama saa tatu utakuwa poa nikupe Sh. ngapi? Mtu mzima nisije nikaumbuka si
 unajua tena
 kwa staa kama wewe?
 Baby Madaha: Milioni 10!
Frank/OFM: Baby usinikomoe, mimi na wewe tuna safari ndefu, 
kila nikija Dar tutakuwa pamoja.
Baby Madaha: (...anapiga simu lakini Frank wa OFM hapokei).
Baada ya kuona hivyo, Baby Madaha alituma sms hii “Call” (piga).
 
 MAONGEZI YA SIMU
Frank/OFM: Mambo vipi Baby, habari za muda tena?
Baby Madaha: Salama tu, kwani wewe ulikuwa unataka kutoa sh. 
ngapi ATM?
Frank/OFM: Mimi ndiyo nilikuwa njiani naelekea ATM natoka hapa hotelini nilipofikia nina Shilingi Mil.4 kwa usiku mmoja, hapo
 vipi?
Baby Madaha: Katoe 5 fresh, sasa benki gani utaenda kutoa
 wakati benki zote zimeshafungwa na ATM mwisho kutoa ni Mil.1,
 sasa
 hapo itakuwaje?
 Frank/OFM: Nitatoa kwa ATM, hata hivyo, nina master-card, 
naweza kutoa Mil.1 hadi mara 5, usijali kwani pesa kitu gani, 
cha
 msingi mimi ni kuwa na wewe!
Baby Madaha: Okay, fine unaweza kuja Kijitonyama (Dar) hapa 
kwenye hoteli ya (anaitaja jina)?
Frank/OFM: Nimefikia hapa hotelini (jina kapuni), sasa kutoka
 ni vigumu.
Baby Madaha: Okay, poa nitakuja hapo hotelini saa 1:00 usiku.
 Frank/OFM: Usijali karibu sana, nakupenda sana Baby Madaha 
yaani niko tayari kwa lolote, sema unataka nikupe nini?
Baby Madaha: Hahaha....(anachekaaa) nikija nitakwambia vyote ninavyotaka kwani unafanya biashara gani?
 Frank/OFM: Nauza nguo, mara nyingi nafuata Jakarta, Indonesia 
mara kwa mara lakini natumia muda mwingi kufanya kazi zangu
 Mwanza.
 Baby Madaha: Wee Msukuma eti? Mimi mwenyewe Msukuma kwani 
unadhani jina Madaha ni la nini hilo, mimi mwenyewe Msukuma.
Frank/OFM: Nimefurahi sana kusikia hivyo, unaweza kuongea 
Kisukuma?
Baby Madaha: Naweza, wewe nisemeshe tu!
Frank/OFM: Nakutogilwe gete Madaha (Frank anaongea Kisukuma 
kwamba anampenda sana Madaha)
Baby Madaha: Tukuhoya ntondo nduhu tabu (anajibu kwa Kisukuma 
kuwa hakuna tatizo tutaongea kesho).
 Ulipofika muda waliokubaliana na Frank wa OFM, Madaha alisema 
kuna foleni kubwa hivyo kuna sababu ya kubadilisha hoteli hiyo 
iliyoko maeneo ya Ubungo alipopanga Frank wa OFM waonane, Baby Madaha akataka wakutane nyingine iliyoko Kijitonyama.
“Siwezi kuja huko, kwanza kuna mifoleni isitoshe ni vizuri 
ukafika mwenyewe maeneo haya ya hoteli ya… (anataja), ni sehemu nzuri 
kwangu hivyo kama huna nia mbaya na mimi ni vizuri ukaja maana 
kesho nasafiri kwenda Kenya kwenye shughuli zangu za muvi, kwa 
hiyo unaweza kuja wewe tu maeneo haya,” alisema Madaha.
 Frank aliendelea kumbana kwamba tayari alikuwa ameshaandaa 
pesa shilingi Mil.5,
 kama walivyokubaliana lakini asingeweza kubeba mfuko wa fedha 
wote huo isitoshe ni
 hoteli ambayo ameizoea kwa muda mrefu.
“Ujue Dar mimi siyo mzoefu, achilia mbali kuogopa kutapeliwa
hivyo nakuomba uje kwenye hii hoteli nitafurahi sana dear, 
nakuomba unielewe ujue nakupenda sana mpenzi wangu Baby Madaha, tulia tuyajenge maisha,” alisema Frank wa OFM.
 Msanii huyo alimkomalia Frank wa OFM wakutane siku ya Jumanne
 usiku ambapo alimwambia pia kuwa amepata dharura anakwenda 
kumuona mfanyabiashara mwenzake kwenye hoteli moja iliyopo 
Masaki (jina tunalo) ambapo Baby Madaha alitaka waonane na Frank 
wa OFM 
kwenye hoteli hiyohiyo.
“Nimepata dharura sitaweza kuonana na wewe, naenda kumuona 
mfanyabiashara mwenzangu maeneo ya hoteli…(jina tunalo), tuonane kesho muda wa asubuhi,” 
alisema Frank.
 Baadaye Frank alimjulisha mteja wake kuwa yuko njiani anafuata mzigo bandarini 
akitoka wataonana na Baby Madaha kesho yake asubuhi ya Jumatano iliyopita, alituma 
sms hii;
Baby Madaha: Kuna stage tano in anything, nakupa tatu, coz uko 
siku ya tatu, 
denying, bargaining, accepting..... tomorrow if you be still on game, i give you the 
remained good
 day, enjoy Mr Frank, ukitoka cargo call me, we meet!
Frank/OFM: Okay, siku njema nitakutafuta.
 Baby Madaha: Matajiri wengine hawana maneno kama wewe kwa 
mfano…(anataja
 jina la pedeshee mmoja maarufu Dar). Wanatuma pesa na siyo
maneno, wee tuma
 hela (-)-pesa ipo kila sehemu we tuma ndo nitaweza kujiongeza 
kama nakuja au laa.
Frank/OFM: Nakutumia muda siyo mrefu, usijali.
 IJUMAA LAMBANA BABY MADAHA
Hata hivyo, Baby Madaha hakutumiwa pesa alizotaka ili 
kukamilisha zoezi badala yake, 
OFM walitua mzigo wa ushahidi kwenye dawati la Ijumaa ambalo lilikuwa na 
jukumu la kutafuta mzani wa ishu hiyo.
Ijumaa lilipomtafuta Baby Madaha alikiri kuwa kwenye mawasiliano 
na 
mwanaume aliyemtaja kwa jina la Frank Michael Lugisha ambaye 
alisema alikuwa
 akifanya naye makubaliano ya kusambaza filamu yake ya The Gal Bladder. Alipobanwa
 juu ya makubaliano ya kujiuza kwa mwanaume huyo kwa Sh. milioni 
5 alikataa 
pamoja na kwamba alielezwa kuwa kuna ushahidi wa meseji na sauti
Alipotakiwa kufika kwenye ofisi za gazeti hili ili 
 kusikilizishwa sauti na kuoneshwa 
meseji zake, Baby Madaha alisema hawezi kwa kuwa alikuwa na 
safari ya kwenda 
nchini Kenya muda mfupi baadaye. 
STORI HII NI KWA HISANI YA GLABOL PUBLISHERS LTD

No comments:

Post a Comment