TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, January 15, 2014

Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana inavyompa Kijana Fursa ya Kujitambua na kujiamini

IMG_9189 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na vijana katika moja ya matukio.
………………………………………………………
Na Benjamin Sawe
WHVUM
 “Vijana ni nguvu kazi ya Taifa”. Hii ni kweli na kwa mujibu wa
utafiti wa Nguvu Kazi Nchini ya mwaka 2006 asilimia 68% ya nguvu kazi
nchini ni Vijana ambao idadi yao kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi
ya mwaka 2012 ni 15,587,621 sawa na asilimia 34.7% ya idadi ya watu
wote nchini. Kati yao Vijana wa kike ni 8,273,505 sawa na asilimia
35.9% na Vijana wa kiume ni 7,314,116 sawa na asilimia 33.4%.
Kutokana na umuhimu huu, kumekuwa na jitihada mbalimbali za Serikali
zinazolenga katika masuala ya maendeleo ya Vijana nchini hii ikiwa ni
pamoja na kuwa na Sera, Mipango na Mikakati inayokidhi mahitaji
mbalimbali ya vijana kama vile, Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana
2007,Sera ya Taifa ya Ajira 2008 (Iliyo chini ya Wizara ya Kazi na
Ajira), Mpango Kazi wa Taifa wa Ajira kwa Vijana 2007 na Programu ya
Kukuza Ajira zenye Staha kwa Vijana nchini inayoratibiwa kati ya
Wizara Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Shirika la Kazi Duniani
(ILO).
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi
anasema Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana 2007 ni matokeo ya
maboresho ya Sera ya Vijana ya mwaka 1996 ambapo, maboresho ya Sera
hiyo yanatokana na mabadiliko, mahitaji au changamoto mbalimbali
zinazojitokeza za kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Vilevile, suala la ukuaji wa kasi ya Sayansi na Teknolojia huilazimu
Serikali kufanya maboresho muhimu ili kuendana na wakati. Anasema
Bwana Kajugusi.
Anafafanua kuwa msukumo mwingine unaopelekea kufanyika kwa maboresho
ya Sera ni pamoja na utekelezaji wa maazimio yanayofikiwa na Tanzania
ikiwemo kama vile Jumuiya ya Madola, Umoja wa Mataifa, EAC, SADC na
AU.
Aidha kwa upande mwingine Sera hutoa Mwongozo na Dira kwa wadau
mbalimbali kuweza kutekeleza yale ambayo yametamkwa kwenye Sera hiyo.
Hivyo, Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana 2007 inatoa fursa kwa
vijana kujiamini na kujitambua.
Bwana Kajugusi anasema, Ibara ya 3(3), Sera inatamka kuwa “kutakuwa na
utaratibu wa kutoa mwongozo kwa ajili ya kuwezesha malezi sahihi ya
Vijana na kuendeleza vipaji vya Vijana”.
Hivyo katika kutekeleza tamko hilo la Sera, Serikali kwa kushirikiana
na wadau wa maendeleo ya Vijana nchini imeweza kuandaa programu za
kuwawezesha Vijana kujiamini na kujitambua kama vile “Programu ya
Stadi za Maisha kwa Vijana Nje ya Shule”
Anasema Vijana wengi waliopata elimu hiyo, wamefanikiwa kwa kiasi
kikubwa kubadili fikra na kuchukua hatua ya maendeleo katika kufanyia
kazi vipaji walivyokuwa navyo ambapo ni sehemu mojawapo ya utekelezaji
wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana 2007.
Pia Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana 2007 vilevile inatambua
umuhimu wa ushiriki na ushirikishwaji wa Vijana katika kubaini na
kutumia rasilimali zilizopo kwa ajili ya ustawi wa maendeleo yao na ya
nchi kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment