TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, January 15, 2014

Washiriki wamiminika mtandaoni kujiandikisha Kilimanjaro Marathon 2014

kilimanjaro-marathon
Mamia ya washiriki tayari wanajiandikisha kwa wingi kupitia mtandao wa intaneti ili kushiriki mbio za Kilimanjaro Marathon 2014 zinazotarajiwa kufanyika Moshi tarehe 2 Machi, 2014.
John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana kwamba idadi kubwa ya washiriki wanaendelea kujiandikisha kupitia tovuti yam bio hizo www.kilimanjaromarathon.com ukilinganisha na mwaka jana ambapo wachache walijiandikisha kupitia mtandao. Uandikishwaji huo wa mtandao ambao upo wazi mpaka tarehe 18 Februari, 2014 unawapa urahisi wa kujiandikisha hasa washiriki kutoka nje ya nchi ambao wanatakiwa kujiandaa na safari ya kuja nchini kutokana na mtandao huo kutoa uthibitisho wa usajili mara tu baada ya kujaza taarifa husika.
Addison aliongeza kuwa ongezeko kubwa la usajili kupitia mtandao ni ishara kwamba mbio za mwaka huu zitakuwa na washiriki wengi zaidi wa kigeni ukilinganisha na zaidi ya 400 walioshiriki mwaka jana. “Ongezeko la ushiriki lina maana kwamba mbio inazidi kukua kwa kiasi kikubwa na hii ni kutokana na mchango mkubwa unaotolewa na Kilimanjaro Premium Lager ambao wamewekeza kwenye mbio hizi tangu zilipoanzishwa mwaka 2003.”
Pia Addison alisema ukuaji wa mbio hizi ni matokeo ya jitihada kubwa zinazofanywa na waandaaji kupitia mtandao wa intaneti pamoja na mbio hizi kuonyeshwa bara zima la Afrika kupitia SuperSport na televisheni nyingine za kimataifa dunia nzima.
Zikiwa zimepangwa kufanyika Moshi tarehe 2 Machi, 2014, mbio za Kilimanjaro Marathon zitakuwa na matukio manne ambayo mbio ndefu za 42km Kilimanjaro Premium Lager Marathon,  21km Nusu Marathon, 11km GAPCO Disabled Run (zitahusisha viti vya magurudumu na baisikeli za mikono tu), na mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run ambazo hutoa fursa kwa watu wa rika zote kushiriki.
Kwa mara nyingine tena mbio hizi zitakuwa kivutio kutokana na ushiriki wa timu zitakazowakilisha makampuni mbalimbali kupitia shindano la Half Marathon Corporate Challenge.

No comments:

Post a Comment