TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, January 15, 2014

CCM IRINGA MJINI CHAMVAA MBUNGE MSIGWA CHADAI AJIANDAE KUNG’OKA UBUNGE


Na Francis Godwin Blog
CHAMA Cha mapinduzi (CCM) wilaya ya  Iringa mjini  kimesema kimejipanga kwa nguvu zote kuhakikisha mbunge wa  jimbo hilo mchungaji Peter Msigwa anaachia jimbo hilo hata kama hataki ikiwa ni  pamoja na  wiki tatu kwa mstahiki meya  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa Amani Mwamwindi kufuatilia kero mbali mbali za wananchi ikiwa ni pamoja na kujua kiasi cha Tsh milioni 15  zinazotolewa kwa  ajili ya mfuko wa  maendeleo ya  jimbo hilo kama zinatumika vema . Mbali ya  hilo pia  kufuatilia huduma  zinazotolewa katika vituo  vya afya  Hospital na Zahanati kama zinafanyika kwa ubora  ama  zinafanyika kwa kuwanyanyasa  wananchi.
“Ushindi  wa  Msigwa  jimbo la Iringa mjini ulitokana na CCM wenyewe ila  sasa tunasema kamwe hatutarudia makosa yaliyojitokeza ni lazima turudishe  jimbo na Msigwa fedha zake azitumie  vema asijaribu kuingia katika ubunge tena”

  katibu wa CCM Iringa mjini Hassan Mtenga  aliyasema  hayo  juzi wakati wa mkutano wake wa kwanza uliofanyika katika  uwanja wa Mwembetogwa toka alipohamishiwa wilaya ya Iringa mjini akitokea Hai mkoani Kilimanjaro
 Alisema zama za ubunge wa Mchungaji  Msigwa katika jimbo la Iringa mjini umekwisha na sasa atake ataondoka na asipotaka ataondoka. 
“Mwambieni mbunge Msigwa wakati  wa kuwadanganya  wananchi umekwisha  na lazima sasa awaeleze  wananchi  wa jimbo la Iringa mjini  wapi  anapelekea  fedha za mfuko wa  jimbo ambazo  zinatolewa kila mwezi na Rais Jakaya  Kikwete”
Hata  hivyo alimuagiza meya  kupambana ili  fedha  kiasi cha Tsh milioni 15  zinazotolewa na rais Kikwete kuona zinafanya kazi gani katika ofisi ya mbunge  pia kutembelea  Hospital  na vituo vya afya  ili  kuona changamoto mbali mbali ndani ya wiki tatu kupeleka majibu katika ofisi yake.
Kuhusu  kupanda kwa gharama za umeme ni matokeo ya Dr Slaa ambae  alipigia kelele suala la Richmond na  Dowans ambapo baadhi ya  wabunge  waliunga mkono  suala  hilo ila leo baada ya mambo kuwa magumu tunalalamikia suala  hilo ambalo waasisi  wake ni Chadema kuleta kwele .
Alisema  kuwa  tunahitaji  vijana  kuleta maendeleo  ya mji wa Iringa na sio vijana  wa kutumiwa kuvuruga maendeleo ya mji wa Iringa.
” Nawaombeni  wananchi  kuwa tayari  tumemshika pua mbunge Msigwa na naomba  wananchi tusaidiane  kumnywesha panado na ninamuomba  Msigwa fedha za kiinua mgogo  zake asije  tena katika jimbo la Iringa mjini atumie  kwa kazi nyingine  ….tumeanza mkakati  huu kwa ajili ya kumnyoa Msigwa “

Katika  mkutano  huo  wananchi   walipewa nafasi ya  kuwaweka  kitimoto madiwani  wao ili kujibu kero  mbali  mbali za  katani kwani  huku  wananchi  wa  jimbo  hilo la Iringa  mjini  wakikitaka  chama hicho kusaidia  kukinusuru  chama  na  kura  za chuki  kutokana na shirika la ugavi  wa umeme nchini (TANESCO)  kuendelea  kupandisha  gharama  za  umeme.

Wananchi  hao  walisema  kuwa  ili CCM jimbo  hilo na Tanzania kwa ujumla kiweze  kushinda katika uchaguzi  mkuu wa mwaka 2015  na ule wa  serikali za mitaa utakaofanyika mapema mwaka  huu ni lazima gharama  za umeme ishuke

Kwani  walisema  kuwa  hatua ya  TANESCO  kuendelea  kuongeza  bei ya  umeme  ni  kuongeza  ugumu  wa maisha  kwa  watanzania na kuwa ushindi  wa CCM  utatokana na utetezi  wa chama katika  kuwaondolea  mzigo  wa bei ya umeme watanzania.
Mbali  ya  hilo pia  wananchi  wa  kata ya Kihesa walimbana  diwani  wao Bw  Mussa Wanguvu  kutokana na hatua ya  kushindwa  kupigania  wananchi ambao  wanatakiwa  kuvunja  nyumba  zao ambazo  zimejengwa katika eneo la  Semtema Majengo  mapya eneo ambalo halitakiwi  kisheria
Diwani  Wanguvu  akijibu  swali  hilo alisema  kuwa eneo  hilo  lilizuiwa baada ya kufanyika kwa mkutano wa hadhara  hasa  wale  ambao  wamejenga katika mlima na wapo hatarini  kuangukiwa na mawe  ila baadhi ya maeneo ambayo  si  rasmi  ni waliachiwa .
Kwa  upande  wao  wananchi  wa kata ya Mtwivila  walimtaka diwani  wao Bw  Victor Mushi  kueleza  ni  lini atatekeleza ahadi yake  ya zahanati na ubovu  wa barabara katika  eneo la Mkimbizi pamoja .
Kwa  upande  wake diwani Mushi  kuhusu  suala  la ujenzi  wa  kituo cha afya  alisema  kuwa ahadi hiyo haikuwa ya kwake  ila  ilikuwa katika ilani  ya  CCM  japo alisema ujenzi  wa  mradi huo  upo mbioni  baada ya  kumaliza miradi ya zamani utaanza mradi huo  wa ujenzi  wa  kituo cha afya.
Kuhusu  barabara  alisema  kuwa kata  hiyo  wamejitahidi  kutengeneza  mifereji na zaidi ya Tsh  bilioni 1.8  zitatengeneza  barabara  ya lami  kutoka Mtwivila  kwenda Mkwawa  na tayari  zoezi hilo linaendelea.
Katika  hatua  nyingine  Mushi  alipinga  madai ya  wananachi  kuwa  uongozi  wa Halmashauri  ya Manispaa ya  Iringa  umekuwa  ukifanya usafi  katika mji  kutokana na kuwepo kwa ugeni ama  vikao  kuwa jambo  hilo  si kweli na kuwa linafanyika kulingana na bajeti  na ufinyu  wake.


Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati pia aliweza kueleza  kazi mbali mbali alizozifanya katika jimbo la Iringa mjini ikiwa ni pamoja na kujenga kituo cha polisi kwa gharama zake eneo la Tumaini na kuwa ataendelea kuchonga sana juu ya kero za wananchi wa Iringa mjini. Kabati alisema kuwa kamwe hatarudi nyuma katika utendaji na kuwa siku zote atawapigania wananchi wa jimbo la Iringa mjini na kuwa kuwa siku zote kwake atahakikisha anatenda zaidi. 
 Akielezea mambo ambayo amepata kutekeleza alisema ni pamoja na kusaidia sekta ya elimu vitabu na kompyuta pamoja na kusaidia vikundi vya vikoba katika jimbo hilo la Iringa mjini.
Mstahiki  meya  wa Manispaa ya  Iringa Aman Mwamwindi  akijibu kero mbali mbali akianza na Hospital ya  wilaya ya Iringa  mjini alisema kuwa  Hospital  hiyo  imeendelea  kutoa huduma .
Huku  ujenzi  wa barabara  za lami katika mji  huo kupitia pesa za benk ya Dunia  alisema barabara  itajengwa kuanzia  Samora ,Hospital ya Frelimo , Itamba na maeneo mengine ya mji .

No comments:

Post a Comment