TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, January 12, 2014

Yatima Dar walilia madarasa yakujisomea

001(1) 
Baadhi ya watoto yatima wa kituo cha Sifa Group Children Foundation Center kilichopo Bunju, Dar es Salaam wakiwapokea kwa furaha wafanyakazi wa Idara ya mauzo na Usambazaji wa kampuni ya Vodacom Tanzania wakati walipoenda kutoa msaada kwenye kituo hicho. Msaada huo wa chakula na vitu mbali mbali kupitia kampeni ya pamoja na Vodacom.
……………………………………………………………………
 Mkurugenzi wa kituo  cha kulelea yatima cha Sifa Group Foundation Children Center kilichopo Bunju mkoani Dar Es Salaam ametoa wito kwa wadau mbali mbali nchini kuwa tayari kujitolea kusaidia vituo vya watoto yatima kikiwemo kitu chake ili kuweza kutatua matatizo yanayokabili vituo vingi nchini ikiwemo uhaba wa madarasa ya kujisomea, ubovu wa vyoo na malazi.
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi huyo wakatiakipokea misaada kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kupitia taasisi yake ya Vodacom Fondation iliyojumuisha vitu mbali mbali ikiwemo magodoro, vifaa vya shule, vyombo vya ndani, vyakula pamoja na ada za shule kwa watoto wa kituo hicho.
“Tuna tatizo la uhaba wa fedha ili kuweza kumalizia kituo chetu kipya ambacho tumejitaidi kupata kiwanja hadi sasa lakini bado hatujapata fedha zakuweza kujengea kituo hicho, vile vile tunahitaji tujenge madarasa ambayo yatasaidia watoto wetu kujisomea lakini fedha hatuna zakuweza kufanikisha mradi huo.”
“Tunapokea watoto wengi ambao hawana uwezo wa kusoma wala kuandika tumechukua jukuma la kuwafundisha hapa kwa uwezo mdogo tulionao na darasa hili dogo ambali haliwatoshi na pia halina vifaa kamili vya kufundishia, tunawaomba wadau wajitolee kutusaidia ili tuweze kutoa elimu kwa watoto hawa amba ndio msingi pekee wa kuwapatia ili wajiendeleze katika maisha a
Yao.”
Mkurugenzi huyo alitanabaisga kuwa, “Tumekuwa tukilalamika siku hadi siku kuhusiana na ubovu wa vyoo tulio nao ambao mara kwa mara husababisha maradhi mbalimbali kwa watoto kutokana na wingi wa watoto kuto kuendana na idadi ya vyoo wanavyotumia ni vichache hivyo inakuwa vigumu kuviweka vikiwa visafi wakati wote,”.Alisema
Kwa upande wake Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan Saleh wakati wa makabidhiano ya misaada hiyo ameeleza kuwa ni jambo la busara wao kama kampuni kusaidia kutatua matatizo yaliyondani ya jamii kwani wao ndio wanaowaunga mkono kila siku.
“Tunaamini misaada tuliyoitoa itaweza kusaidia watoto hawa kwa namna moja au nyingine, tunatambua changamoto wanazokumbana nazo lakini sisi kama kampuni tuataendelea kuhakikisha tunasaidia jamii kadri tuwezavyo, hiyo imekuwa ni jadi yetu na hatuwezi kuicha.”Alisema Saleh
Mmoja wa watoto anaelelewa katika kituo hicho Shantala Mussa aliwashukuru wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa kutoa sehemu ya fedha zao na kuwasaidia kwa kuwaletea misaada hiyo na kuwaomba waendelee na moyo huo huo wa kujitolea na kutoa wito kwa makampuni mengine kuweka mazoea yakujitolea ili kuweza kuwafanya watoto yatima wasahau matatizo wanayokumbana nayo na kujihisi nao ni watoto wanaohitaji matuzo kama watoto wa kawaida.

No comments:

Post a Comment