TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, January 18, 2014

MKE WA MTU SUMU, MME WA MTU JE????MWANAFUNZI AMWAGIWA MAFUTA YA MOTO BAADA YA KUFUMANIWA NA BOYFRIEND WA RAFIKI AKE.

http://www.theclicktz.com/

Mwanafunzi wa chuo kimoja alimwagiwa mafuta ya moto na rafiki yake kipenzi baada ya kumkuta na boyfriend wake wakifanya mapenzi.
Ilikuwa ni siku ya ijumaa Nasra alipokuwa akitoka darasani na kurejea hostel alipokea sms ikisema "Nenda kwa Rafiki yako kipenzi Naima kuna Bonge la Surprize, tafadhali usikose nenda sasa hivi" Nasra aliamua kuchukua pikipiki hadi kwa rafiki yake alipofika tu alikuta viatu vya boyfriend yake nje, akashtuka kwanza kwani sio kawaida ya jamaa huyo kwenda kwa Naima bila ya kuwa na Nasra, Nasra alijaribu sana kugonga lakini hakufunguliwa, na baadae aliamua kupiga simu zote mbili ya rafiki yake na ya boyfriend wake pia zote zikaita tu bila kupokelewa, Alikaa pale nje hadi majira ya saa sita usiku, ambapo alishajua kunakitu kinaendelea. Muda ulivyozidi kwenda  Nasra alitoka na kwenda kuchukua marafiki zake wengine wawili, aliporudi alikuta bado hawajatoka ndani.
Mpaka majira ya saa saba hivi usiku, Nasra akiwa amebeba mafuta ya moto kwenye chupa ya chai yeye na marafiki zake walivunja mlango na kuwakuta wawili hao ndani wakiwa katika hali ya uoga jamaa alifanikiwa kukimbia na kumuacha Naima chumbani ambapo Nasra alifungua chupa ya chai na kumwagia mafuta hayo ya moto rafiki yake huyo msaliti.
Nasra alikamatwa baadae na kufikishwa kituo cha polisi ambayo alihojiwa na kusema kwamba, alikuwa akipata tetesi na uvumi kwamba mchumba ake anatembea na rafiki yake kwa siku nyingi hivyo alikuwa anatafuta tu uthibitisho, na ameupata baada ya kuatilia kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment