TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, January 18, 2014

Wanachuo wa Chuo cha St. Joseph Songea Waingia katika Mgomo


WANACHUO wa Chuo kikuu cha St,Joseph tawi la Songea wamegoma kuingia  madarasani na kutoka kufanya shughuli za aina yeyote ndani ya chuo  hicho huku wakiwa wamebeba mabango yaliyoandikwa jumbe mbalimbali  zikiwemo zilizoandikwa wamechoka kunyanyaswa na wakufunzi ambao wengi  wao raia wa India baada ya uongozi wa serikali ya wanachuo kutimuliwa  nyadhifa zao na kuwasimamisha masomo kwa muda wa miezi sita. 
Kundi la waandishi wa habari wa mjini Songea mara tuu baada ya kupata  taarifa ya tukio hilo walifika kwenye eneo la chuo kikuu cha St,Joseph  kilichopo eneo la Luhuwiko mjini Songea ambako walishuhudia maandamano  makubwa ya wanafunzi wakiwa wamebeba mabango yaliyo ujumbe mbalimbali ikiwemo ya wamechoka kunyanyashwa na wakufunzi ambao ni wahindi. 
Pia wanachuo hao walishuhudiwa wakiimba nyimbo mbalimbali zenye ujumbe  wamechoka kunyanyashwa kwani wao ni watu wazima hapaswi kulinganishwa na wanafunzi wa shule za msingi au sekondari huku wimbo mwingine ukiwa na  ujumbe kama siyo mwalimu Nyerere kuleta amani wahindi msingefika kwetu  kufanya biashara. 
Kufuatia mgomo huo ililazimika askari polisi kufika kwenye eneo hilo  huku wakiwa wamebeba silaha kwa lengo la kutuliza gasia ambao  walitawanywa katika maeneo mbalimbali ya chuo lakini wanachuo waliendelea na maandamano yao huku wakiimba nyimbo za kushinikiza  uongozi wa chuo uwarejeshe viongozi wa serikali ya wanachuo kwa sababu  ya kutetea haki za wanachuo ambazo walizodai wahidi hao wamekuwa  wakizikiuka. 
Wanachuo hao ambao walidai kuwa malalamiko yao walishayafikisha kwa 
mkuu wa mkoa wa Ruvuma Saidi Mwambungu wakidai kuwa hali ya mazingira ya chuo hicho siyo manzuri lakini bado wahindi hao wameendelea na vitendo viovu licha ya mkuu wa mkoa kuwaangiza kuwa waache kuunyanyasa uongozi  wa serikali ya chuo na wayaweke vizuri mazingira ya chuo hicho ikiwa ni  pamoja na kufanyia matengezo ya vyoo ambavyo vimesababisha baadhi ya  wanachuo kwenda kujisaidia polini.
Walisema kuwa chuo hicho kinavyoo vyenye matundu na wayaweke vizuri 
mazingira ya chuo hicho ikiwa ni pamoja na kufanyia matengezo ya vyoo 
ambavyo vimesababisha baadhi ya wanachuo kwenda kujisaidia polini. 
Walisema kuwa chuo hicho kinavyoo vyenye matundu 14 ambapo kati ya 
matundu hayo saba ya wanawake na saba ni wanaume wakati chuo hicho 
kinawachuo zaidi ya 1,200 na kufanya kusababisha tundu moja kutumiwa na  wanachuo 64 badala ya kati 20 au 25.
Kwa upande wa viongozi wa serikali ya wanachuo waliyotimuliwa Aristides 
Munjwahuzi na waziri mkuu wake Deogratius Sanga waliwaambia waandishi wa habari kuwa matatizo makubwa yaliyopo ndani ya chuo hicho ni mengi   ambayo wanachuo wakijaribu kulalamika kupitia uongozi wa serikali ya  wanachuo badala yake uongozi wa chuo umefikia kuufukuza uongozi wa  serikali ya chuo na kuwasimamisha masomo kwa muda wa miezi sita jambo  lilionekana kuwa ni uonevu mtupu.
Hata hivyo mmoja wa viongozi wa chuo hicho mtawa Antonia Emmanuel 
alisema kuwa suala la viongozi wa serikali ya wanafunzi la kuvuliwa 
madaraka na kusimamishwa masomo walishapewa maelekezo kuwa malalamiko  yao walete kwa maandishi ili yajadiliwe lakini hawakufanya hivyo jambo  ambalo aliliita kuwa ni dharau na badala yake ameshangazwa kuona  wanachuo wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali lakini amesema  tatizo hilo linahitaji kuwepo mazungumzo ya pande zote mbili yakiwa na  lengo la kumaliza tatizo hilo.

No comments:

Post a Comment