TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, January 15, 2014

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR IMETILIANA SAINI MKATABA WA KUTOA HUDUMA ZA MAGONJWA YA AKILI KATIKA HOSPITALI YA MAKUNDUCHI KUSINI UNGUJA.

 01(1)
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohammed Jiddawi  na Dk. Peter McGovern  wakitia saini makubaliano ya kuanzisha huduma za Aya ya magonjwa ya akili katika Hospitali ya Makunduchi. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya Dk. Sira Ubwa Mamboya akishuhudia utiaji saini  katika sherehe  zilizofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
 ………………………………………………………………………………….
RAMADHANI ALI/MAELEZO ZANZIBAR
Wizara ya Afya ya Zanzibar imetiliana saini mkataba wa makubaliano  wa kuanzishwa kwa majaribio kutolewa huduma za maradhi ya afya ya akili katika Hospitali ya Makunduchi iliyoko Mkoa wa kusini Unguja. 
Uwamuzi wa kuifanya Hospitali ya Makunduchi  kuanzisha  huduma hiyo inatokana na mapendekezo ya Wizara ya Afya   ya mwaka 2008 na taarifa ya Afya ya akili  Zanzibar  ya Jumuia ya Ulaya.
Wadau watatu  wanashirikiana katika mpango huo ambao  ni Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland cha Norway,  Hospitali ya Afya ya akili ya Kidongochekundu na Mradi wa kuimarisha Afya Zanzibar.
Katika sherehe za utiaji saini zilizofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja, Wizara iliwakilishwa na Katibu Mkuu Dk.  Mohammed Jiddawi, Chuo Kikuu cha Haukeland kiliwakilishwa na Dk. Ingavr Bjelland, Dk. Peter McGovern alitia saini kwa upande wa Mradi wa kuimarisha Afya kijiji cha Makunduchi na Dk. Khamis  Othman alitia saini kwa upande Hospitali ya Kidongo Chekundu.
Wadau hao watatu watashirikiana katika kuimarisha kujenga uwezo huduma za maradhi ya Afya ya akili kwa visiwa vya Unguja na Pemba, kuanzisha mtaala wa kufundisha masomo ya afya ya akili wafanyakazi wa Hospitali ya Makunduchi kwa mujibu wa  Shirika la Afya duniani (WHO)  na kuunga mkono maendeleo ya mafunzo yanayotolewa kwa wauguzi wa Hospitali ya Makunduchi na Hospitali ya Kidongo chekundu.
Katika hatua za awali zitakazoanzia mwaka huu, kliniki ya afya ya magonjwa ya akili  ya Hospitali ya Mkunduchi itasimamiwa kwa kiasi kikubwa na Hospitali ya Kidongo chekundu na mafunzo yatatolewa katika mwaka wa kwanza wa kuanzishwa huduma  katika Hospitali hiyo.
Hatua  ya pili ya mpango huo itakayoanza mwezi Januari mwakani  ambapo kliniki hiyo itakuwa imeimarika na Hospitali mama ya Kidongo chekundu kuridhika na hatua iliyofikia, Hospitali hiyo itaruhusiwa kujiendesha yenyewe katika masuala mbali mbali ya uongozi na tiba.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland itasimamia na kuimarisha mitaala ya elimu ya magonjwa ya Afya ya akili kwa wafanyakazi wa Hospitali ya Makunduchi ikiwemo kusimamia mafunzo hayo.
Wadau wote kwa pamoja wamekubaliana kuendeleza na kuimarisha  huduma za  magonjwa ya afya ya akili katika kliniki ya Makunduchi  kwa mujibu wa misingi ya Shirika la Afya Duniani.  
Hospitali ya Makunduchi itakuwa ni  ya pili kutoa huduma za magonjwa ya  Afya ya akili kwa kisiwa cha Unguja na kwa Kisiwa cha Pemba huduma hiyo bado inaendelea kutolewa katika Hospitali ya Chake Chake tu.


No comments:

Post a Comment