TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, January 12, 2014

“TUMEJIFUNZA MENGI KUTOKA TANZANIA”, ALGERIA

Na Asteria Muhozya, Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Nishati katika Wizara ya Nishati naMigodi wa Algeria Bw. Bourraondj Mohamed Tawar amesema, Serikali ya Algeria imejifunza mambo mengi katika sekta ya madini, kufuatia ziara yao nchini Tanzania.
imagesAliyasema hayo jana wakati wakihitimisha ziara yao nchini kwa kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo ya uchimbaji na uzalishaji wa madini ya Tanzanite katika migodi ya TanzaniteOne Mererani na katika kiwanda cha kuzalisha mbolea ya kupanda ya Minjingu, Mkoani Arusha.
Aliongeza kuwa, ziara hiyo imekuwa ya manufaa kwa Serikali yao kutokana na kwamba pamoja na kufanikiwa katika sekta ya gesi lakini wamejifunza mengi katika sekta ya madini na katika mbolea ya kupandia ya Minjingu, hatua ambayo imewawezesha  kujifunza na kuona namna serikali ya Tanzania inavyoshughulikia sekta hizo kuanzia uchimbaji, teknolojia zinazotumika, uuzaji, na mambo yote yanayohusu sekta hizo.
Aidha, alieleza kuwa, wamekutana na mambo mengi mapya likiwemo la uchimbaji wa mbolea ya kupandia ya minjingu inayochimbwa kutokana na masalia ya ndege aina ya flamingo ambayo masalia yake yamekuwepo kwa miaka mingi.
“Nilikuwa nikisoma tu katika vitabu lakini sasa nimeona mwenyewe kwa macho, ni furaha sana na funzo kwetu, kwasababu tunatumia njia nyingine kuzalisha mbolea ya kupandia na si kama hii ya masalia ya ndege aina ya flamingo inayotumiwa na Tanzania”, Alisema.
Aidha, aliongeza kuwa, anaamini kuwa ushirikiano ulioanzishwa na nchi hizi mbili utakuwa wa manufaa kwa nchi zote na kuongeza kuwa,  anaamini kuwa, ushirikiano huo utaharakishwa ili  utekelezaji wake uanze haraka.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha kuzalisha mbolea ya Minjingu Bw. Tosky Hans alisema kuwa, ziara  hiyo ya wataalamu hao kutoka Algeria ni mafanikio kwao kwasababu ushirikiano huo utasaidia kujifunza mambo mengi kutoka Algeria ambao wamepiga hatua kubwa kiteknolojia na kitaaluma
“Tutaangalia upande wa teknolojia wanatumia nini na kuzalisha nini, kwasabababu nia yetu ni kuongeza uzalishaji, kuwafikia wananchi wengi zaidi na kukidhi mahitaji ya mbolea kwa nchi za Afrika Mashariki”. Alisema Hans.
Akielezea kuhusu kupata fursa ya kutembelea katika mbuga za wanyama katika bonde la Ngorongoro Bw. Bourraondj Mohamed Tawar alisema, imekuwa ni furaha kwao kuona makundi makubwa ya wanyama mbalimbali na ndege katika mbuga hizo wakiwemo simba ambao walipata nafasi ya kuwaona vizuri.
Vilevile, alieleza kufurahishwa kwao kufika katika eneo la boma wanapoishi Watanzania jamii ya Maasai ambapo walishangazwa kuona namna Maasai hao wanavyoishi jirani na wanyama wa porini.
Wakati huo huo, Kamishna Msaidizi kanda ya Kaskazini Mhandisi Bw. Benjamini Mchwampaka anayesimamia shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini amewataka wachimbaji na wamiliki wa migodi kufuata sheria na taratibu za leseni ikiwemo kulipa kodi. Aliongeza kuwa, serikali haina ubaguzi kwa wachimbaji wakubwa au wadogo wote wanapewa fursa sawa.
“Tunawaangalia wachimbaji wote kwa usawa, wafuate sheria, wachimbe kwenye maeneo yao bila kuingiliana”. Alisema Mchwampaka.
Vilevile, aliwataka wachimbaji kuwa wazalendo kwa kulipa kodi Kama inavyowapasa bila kufuatiliwa na maafisa madini na kuwataka wakumbuke kuwa, Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe pale wanapotimiza wajibu wao kikamilifu.

No comments:

Post a Comment