TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, January 14, 2014

KAMATI KUU YA CCM YATEUA MGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA KIEMBESAMAKI ZANZIBAR


ZANZIBAR, Tanzania
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM,  imefanya kikao cha siku, Januari 13, 2014 mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wa CCM Dk. Jakaya Kikwete na kujadili mambo kadhaa ikiwemo kumteua Mahmoud Thabit Kombo kuwa mgombea wa kiti cha Uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki.
NAPE Taarifa iliyotolewa leo mjini Zanzibar na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, mgombea huyu wa CCM kesho, Jumanne, Januari 14, 2013, atachukua fomu za tume za kugombea. Nape amesema uzinduzi wa kampeni za CCM utafanyika tarehe 22/01/2014 kwenye viwanja vya Kiembesamaki ambapo mgeni rasmi atakuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mohamed Gharib Bilal.
“Kampeni za CCM zitafungwa tarehe 01/02/2014 huko Chukwani na mgeni Rasmi atakuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Ndg. Balozi Seif Ali Idi”, alisema Nape na kuongeza;
“Kampeni itaendeshwa na Kamati ya Siasa ya wilaya ya Dimani viongozi na wanachama wa wilaya husika, na ngazi zingine za Chama zitashirikiana na ngazi ya wilaya kuhakikisha CCM inashinda tena jimbo hili na Kamati Kuu inawatakia kila lakheri kwenye kampeni na hatimaye uchaguzi huo. Kampeni na hata upigaji kura uendeshwe kwa amani na utulivu kama ulivyo utamaduni wetu”.
Nape alisema, pamoja na uteuzi huo, Kamati Kuu pia imeipongeza sana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kwa kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar na kufanikisha sherehe zake kwa ufanisi kutokana na maandalizi mazuri.
Kamati Kuu imetambua na kupongeza hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa tangu mapinduzi mwaka 1964 mpaka leo. Wito umetolewa kuyalinda na kuyaendeleza mema yote yatokanayo na mapinduzi hayo na mafanikio yaliyoletwa na serikali inayoongozwa na CCM.

Mwenyekiti wa CCM, Dk. Rais Jakaya Kikwete, akifungua kikao cha Kamati Kuu ya CCM, leo katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui mjini Zanzibar. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. (Picha na Adam Mzee)

No comments:

Post a Comment