TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, January 12, 2014

MGIMWA;;- MIMI SI MBUNGE MZIGO NIMETEKELEZA AHADI KUBWA ZOTE JIMBONI NITAGOMBEA TENA

Mbunge Mgimwa

 
MBUNGE  wa  jimbo la Mufindi Kaskazin Mahmoud  Mgimwa  amesema  kuwa  kuwa  kati  ya  wabunge wachapakazi  yeye ni miongoni na  kuwa  yeye si mbunge mzigo kwa  jimbo  hilo kwani amefanikiwa  kutimiza ahadi  zake kubwa zote  alizopata  kuwaahidi  wapiga kura  wake.
Akizungumza katika mahojiano maalum  juu  ya ahadi  alizopata  kuwaahidi  wapiga kura  wake  wakati wa  wa kampeni  za uchaguzi  mkuu  mwaka 2010 ,Mgimwa  alisema  kuwa mbali ya jitihada  kubwa ambazo amezifanya  kama  mbunge  katika  kutekeleza ahadi mbali mbali  ila bado anampongeza  zaidi Rais Dr  Jakaya Kikwete ambae  alipata  kuahidi  kuweka lami katika mji wa Mafinga na tayari  lami hiyo  imewekwa na kuzidi  kumwongezea heshima kubwa yeye kama  mbunge na Chama cha mapinduzi (CCM)
Alisema  kuwa miongoni mwa ahadi ambazo  alipata  kuzitoa kwa  wapiga  kura  wake  wakati wa kampeni ni pamoja na uboreshaji wa  miundo mbinu kwa maana ya  barabara ya Mafinga – Madibila ambayo tayari  imefanyiwa  matengenezo  na ipo  katika  orodha ya barabara  zitakazowekwa lami,pamoja na ahadi  za elimu ,afya ,maji  ambazo zote  zimefanyiwa kazi.
Hivyo  alisema  iwapo asingefanikiwa  kutekeleza ahadi  zake ambazo aliwapa  wapiga kura  wake  asingekuwa na haja ya  kuendelea  kuutaka  ubunge  wa  jimbo hilo ila kwa  kuwa sehemu kubwa ya ahadi amepata  kutekeleza ni  wazi  kuwa  yeye  si mbunge mzigo   hivyo bado  ana uwezo  wa  kuendelea  kuwaongoza  wanananchi  wa  jimbo  hilo.
Mbunge  Mgimwa  alisema  kuwa  wananchi  wa  jimbo  hilo  wameendelea  kuwa na ushirikiano mzuri  katika  kujituma  kufanya kazi na  kuwa  imani  ambayo wananchi hao  wameendelea  kuionyesha  kwake imezidi  kumpa nguvu  zaidi  ya  kuwatumikia  na kuwaomba  kuendelea kujituma zaidi.

No comments:

Post a Comment