TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, January 15, 2014

“TUMEPATA TAARIFA SAHIHI KUHUSU GESI NA MAFUTA’’, – VIONGOZI WA DINI

IMG_0239-1

Asteria Muhozya ( Mtwara, Lindi na Kilwa)
Kusudi la Wizara ya Nishati na Madini kufanya kazi kwa kushirikiana na viongozi wa dini katika sekta za gesi na mafuta kwa manufaa ya Watanzania limefikiwa.
Akizungumza baada ya ziara ya kutembelea Bomba Jipya la gesi asilia Mtwara- Dar es Salaam, Mtambo wa kusafisha umeme wa Mnazi Bay, na maeneo mbalimbali ya uendelezaji wa gesi asilia katika Mkoa wa Mtwara na Lindi, Katibu wa Jumuiya ya Kikrsito Tanzania (CCT) na Mwenyekiti wa Sekretariati  ya kongamano la viongozi wa dini Bw. John Mapesa, alieleza kuwa, viongozi wa dini wamepata elimu sahihi ambayo hawakuifahamu kabla kuhusu sekta hizo.
Aliongeza kuwa, viongozi hao wamekuwa wakipata habari ambazo si sahihi kuhusu rasilimali hizo lakini baada ya kutembelea, kujifunza, kuona na kusikia kutoka kwa watalaamu mbalimbali kuhusu namna miradi hiyo inavyofanyika, wanatarajia kuwa walimu kwa watanzania wengine ili kuwa na uelewa wa pamoja.
“Sisi tuna nafasi kubwa sana ya kukutana na wananchi kutoa elimu, kwani wanatuamini na wanatusikiliza kwa kwasababu tunawasaidia kiroho. Wizara imefanya sehemu yake na sisi tunayo sehemu yetu ya kuwafikia kupitia umoja wetu”.  Alisema.
Aliongeza kuwa, viongozi wa dini ni sehemu ya jamii na wanaposhirikishwa kwa kuelezwa mipango mbalimbali ya Serikali ni jambo la muhimu kwasababu wanayo nafasi ya moja kwa moja ya kuwasiliana na wananchi ikiwemo kushauri. Hivyo, elimu waliyoipata na taarifa walizozipata zitakuwa na mchango katika kuleta amani na ustawi wa jamii wakati huu ambapo nchi inaelekea katika kupokea uchumi mkubwa kupitia rasilimali hizo.
“Nawaambia Watanzania wenzangu tushiriki kikamilifu katika uchumi huu wa gesi na mafuta  kila mmoja kwa namna yake  kwani kuna mafanikio makubwa sana yanakuja. Kuna fursa nyingi na Mwenyezi Mungu hawezi kuleta baraka kwa ajili ya kutuangamiza, analeta kutuletea furaha ili tufaidike. Juhudi za Serikali kuhakikisha kila mmoja anafaidika tumeziona”. Alisema.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini aliyeongoza ujumbe huo, Mhandisi Ngosi Mwihava alisema kuwa, kufuatia ziara hiyo ya viongozi wa dini, inaonesha kuwa serikali ni sikivu na inasikiliza matarajio ya wananchi.
“Tuliona kuwa kuna uelewa tofauti tofauti katika rasilimali hizi, viongozi waliomba tuwaelimishe na sisi tumefanya hivyo kwasababu tunajua wanayo nafasi kubwa ya kuwafikia wananchi na wana mchango mkubwa katika kufikia maendeleo tunayoyatarajia”. Alisema   Naibu Katibu Mkuu.
Aliongeza kuwa, lengo kubwa la ziara hiyo ya viongozi wa dini ni kutaka kuweka uelewa wa pamoja kuhusu rasilimali hizo kwa makundi mbalimbali yenye uwakilishi Kitaifa hali ambayo itasaidia kufahamu fursa zilizopo, mipango ya serikali na kila mmoja kwa nafasi yake ajue namna fursa zilizopo katika sekta hiyo zitakavyotumiwa.
“Katika mchakato wa maendeleo, kuna wadau wengi, hivyo mwanya upo kwa wadau kuchangia katika uwekezaji inaweza kuwa kuwekeza kwa kushirikiana na serikali au kufanya binafsi”. Alisema Naibu Katibu Mkuu.
Aliongeza kuwa, anaamini ziara hiyo imetoa mwanga kwa viongozi wa dini katika kuelekea kwenye kongamano la kujadili rasilimali hizo na namna zitakavyowanufaisha watanzania.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Mstaafu Mhe. Joseph Simbakalia aliwataka viongozi hao kuwasaidia wananchi kuyaweka matarajio ya uchumi huo kwenye  kiwango halisi  kwa kuzingatia kwamba, uchumi wa gesi ni sekta mpya Tanzania na hivyo, maandalizi yakutosha yanahitajika ikiwemo kujifunza kwa usahihi kutokana na ukweli kwamba biashara hiyo ni ghali.
“Mmefanya vizuri sana kuja, kawaambieni vijana na wananchi wajiandae kujua watafanya nini katika uchumi huu kuanzia kwenye elimu na uwekezaji ili tufike tunakotaka kwenda. Msipofanya hivyo, hatutakwenda vizuri”. Alisema Simbakalia.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Ludovick Mwananzila aliwataka viongozi hao kuwaelimisha wananchi ukweli kuhusu gesi kusafirishwa kwenda Dar es Salaam, ugunduzi wake na manufaa yake kwa Taifa kwasababu wamepata nafasi ya kuona yale  yanayofanyika na kusikia mipango mbalimbali.
“ Waelimisheni ukweli, Dar es Salaam ndio kuna viwanda vingi vya uzalishaji tofauti na Lindi na Mtwara, lakini haimanishi kwamba Mikoa hii itabaki bila manufaa, tuna kiwanda cha sementi kinatarajiwa kujengwa hapa Lindi tunatarajia kitatoa fursa nyingi, si hilo tu, tuna mipango mingi ya kuhakikisha kuwa wananchi wote wananufaika”. Alisema.
Aidha, aliwataka viongozi hao  kuwaelimisha wananchi kuacha kuchukua mifano ya nchi ambazo hazikujiandaa katika uchumi wa gesi na kuongeza kuwa, ni elimu pekee ndio itasaidia kuleta mabadiliko kwa wananchi.
“Kilwa kwa mfano, katika kijiji cha Songosongo wanapata si chini ya milioni 20 kwa mwezi kutokana na faida za gesi, wanapata umeme bure, maji bure, sasa katika hayo vurugu za nini? Alisema Mkuu wa Mkoa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Abdalah Ulega aliutaka ujumbe huo kuwaeleza wananchi kuwa, mafanikio katika sekta ya gesi yapo na wananchi wameanza kufaidika nayo.

No comments:

Post a Comment