TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, December 7, 2014

Njuweni Institute Hoteli, Eden Hill College zatesa bonanza la vyuo mkoa wa Pwani(NACTE INTER COLLEGE DAR ES SALAAM).

Na: Mwandishi Wetu

Chuo cha njuweni Institute na Eden Hill College vyote vya mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki viliweza kutama kwenye Bonanza la Wanavyuo lililofanyika kwenye viwanja vya Shirika la elimu Kibaha ikiwa ni sehemu ya tatu kwa kanda ya kaskazini chini ya Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania  &  Entertainment C.o Ltd .
Timu ya Chuo cha Njuweni kwa upande wa mchezo wa mpira wa miguu ndiyo iliyong’ara zaidi huku ikifuatia na timu ya chuo cha Eden hill waliokuwa washindi wa ili na kujihakikishia kuingia kwenye hatua ya timu 32 bora za NACTE zitakazoshiriki kwenye fainali kubwa ya Kanda ya Kaskazini itakayofuata baada ya awamu hii ya mchujo wa awali kumalizika katika mfuno wa Bonanza.
Akizngumzia Bonanza hilo ambalo ni kwa ajili ya kupata timu zitakazoshiriki michuano ya NACTE,  Mkurugenzi wa chuo cha Njuweni Institute Hoteli, Bwana Saidi Mfinanga aliema kuwa ni jambo la kupendeza kutokana na kukutanisha vyuo mbalimbali kwa ajili ya kushiriki kwa pamoja michezo inayojenga ubora wa afya zao lakini pia ikiwa ni njia ya kuwaunganisha wanavyuo, Makampuni pamoja na wadau mbalimbali.
“mfumo huu unapendeza sana, na hata niwapongeze walioanziasha utaratibu huu wa vyuo vya elimu ya kati kukutanishwa na michezo, mimi binafsi hata chuo changu kisingetwaa nafasi ya kwanza lakini ningebaki na amani tu kwani huu ni mwanzo, lakini tuwapongeze hawa walioweza kubuni njia hii sahihi na uliokuwa tukiitamani wakati mwingi, mimi vijana wangu unisumbua sana inapofika wakati fulani wakidai niwatafutie timu wakacheze nao, huwa inasumbua sana lakini sasa ufumbuzi umekuja na si kwangu tu nadhani hata kwa wenzangu, tuwape ushirikiano hawa waliobuni hili jambo, na pia sisi wenyewe tujitunzie heshima zetu wakati tunashiriki siku zote katika michezo hii, michezo ni furaha, amani na upendo hivyo tushiriki kwa Upendo” alisema Mfinanga

Jumla ya Vyuo nane vilishiriki katika bonanza hilo linaloendelea katika siku za jumamosi kwa kushirikisha michezo ya Soka, Netball, Basketball na Voleyball, ambapo kwa upande wa mchezo wa Netball ni timu ya chuo cha Njuweni na Dacico waliofanikiwa kufuzu hatua ya pili huku Heden hili pia ikiibuka kidedea katika mchezo wa Basketball.
Aidha kwa upande wa mchezo wa Voleyball ni chuo cha Njuweni waliofanikiwa kuingiza timu huku vyuo vingine vikishindwa kuwasilisha wachezaji na hivyo kuwafanya njuweni kuingia hatua ya pili bila jasho katika mchezo huo.
Mratibu wa Michezo hiyo Vyuoni, Mpalule Shaaban alisema kuwa Michezo hiyo imeanza kwa kusuasua kutokana na washiriki wengi (Wanafunzi) kutokuwa na vifaa vya michezo jambo linalowapa tabu wakati wawapo michezoni.

“Jambo ni jema na hata mwitikio kwa wanavyuo pia ni mkubwa, lakini tatizo ninalolitazama hapa ni ukosefu wa vifaa vya michezo kwa vyuo pamoja na wachezaji wao, wengi hata viatu vya mchezo husika hawana wanacheza na viatu visivyokuwa vya mchezo husika, jezi wakati mwingine wanatumia hazina namba, hivyo bado ni tatizo kwa upande mwingine, ila kuhusu mwitikio wao kama wanafunzi wamependa sana michezo hii, kubwa tu mimi niombe kwa serikali na wadhamini wajitokee wasaidie michezo hii ya vyuo, Wanavyuo ndiyo wafanyakazi wa kesho hapo Ofisini kwako, sasa ni nani anapenda kuwa na mfanyakazi goigoi? Na hata watu binafsi kama wewe ni mdau jitokeze kusaidia vifaa vya michezo” alisema Mpalule.
Na kuongeza kwamba, heshima hii ni ya pekee ambayo Serikali imetoa kwa Vijana wa vyuo vya elimu ya kati kushiriki michezo, haijawahi kuwepo tangu NACTE imeanzishwa hivyo hii ni fulsa ya pekee tuliyonayo katika kuhakikisha kwamba tunahamasisha michezo hii wakati wote ili vijana wanaojiunga na Vyuo vya Elimu ya Ufundi, Veta, na wale wa ngazi ya Diploma kushiriki michezo vyuoni.

 Sehemu ya kwanza mpaka sehemu ya tatu zimefanyika mwezi uliopita kwenye viwanja vya D.I.T, Ustawi wa jamii kijitonyama na Viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha ambako Vyuo mbalimbali vya NACTE mkoa wa pwani na dar es salaam vilicheza katika michezo ya soka, Basketball, Voleyball na netball katika kutafuta timu zitakazoshiriki ligi ya NACTE Tanzania katika msimu wa 2014/2015.


Ukiachilia mbali michezo hiyo, michezo mingine itakayokuwa ikifanyika kati ya wanafunzi na wanafunzi ni DEBATE, Marathon, Modoling, Mashindano ya Vipaji  kwa viongozi wanaosimamia serikali za wanafunzi kwa nafasi za Rais na Makamu, Waziri Mkuu, Mawaziri wa Michezo, Fedha,  na Spika , watakaokuwa wakichuana katika kujielezea, kujibu maswali, na kuelezea Mada katika nafasi zao na changamoto wanazokabiliana nazo na washindi watakuwa wakipata tuzo mbali mbali kulingana na ushindi wa kila mmoja.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment