Rais Milos Zeman wa Jamhuri ya Czech amesema wimbi la wakimbizi barani Ulaya ni "uvamizi uliopangwa", na sio suala la bahati mbaya. Kiongozi huyo anayefahamika kwa misimamo yake mikali dhidi ya wahamiaji, amewataka vijana wa kiume nchini Syria na Iraq kukamata silaha kupambana na kundi lijiitalo Dola la Kiislamu, IS, badala ya kukimbilia Ulaya. Katika ujumbe wake wa Krismasi uliotolewa jana, Rais Zeman alisema "inawezekana" kuwahurumia wakimbizi wazee, wagonjwa, na watoto, lakini sio vijana wa kiume, kwani kukimbia kwao kunalipa nguvu kundi la IS. Hata hivyo, ujumbe huo wa Rais Zeman ulikanushwa na Waziri Mkuu
Bohuslav Sobotka akisema umejikita kwenye dharau na tabia ya kuyachukulia mambo kijuujuu. Utafiti wa hivi karibuni unaonesha kuwa asilimia 70 ya raia wa Czech, ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya, wanapinga uingiaji wahamiaji na wakimbizi kwenye nchi yao.
No comments:
Post a Comment