TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Wednesday, December 23, 2015
MADEREVA WATAKAOZIDISHA ABIRIA KWENYE VYOMBO VYA USAFIRI KUKIONA
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na Jeshi la Polisdi Nnchi zima kupambana na watu watakaovunja sheria ya usafirishaji wa watu kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
Na Chalila Kibuda,Globu ya JamiiJESHI la Polisi Nchini limewatahadharisha madereva watakaozidisha idadi ya abiria kuliko uwezo wa chombo cha usafari kwani ni kosa kisheria na watakaozidisha abiria kwenye vyombo vyao vya usafiri watachukuliwa hatua za kisheria.Operesheni hiyo inaanza leo baada ya tamko la Jeshi la Polisi na kuanza kutekeleza kwa wale wote wataobeba abiria wengi tofauti na uwezo wa basi, watachukuliwa hatua madereva wa daladala,mabasi ya mikoani pamoja na magari aina ya Noah.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba amesema kuwa Jeshi la polisi linaanza operesheni ambayo ni endelevu na kuwataka watu wafuate sharia ya ubebaji wa abiria.Advera amesema kuwa katika kipindi hiki cha siku kuu Jeshi la polisi limejipanga katika kuwadhibiti waendesha bodaboda kwa wataopandisha watu zaidi ya wawili (mishikaki) kukiona cha mtema kuni kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani.Aidha amewataka wananchi kutoa taarifa za kihalifu katika msimu wa sikukuu na uimarishaji wa ulinzi wa watu na mali zao na maisha yaweze kuendelea baada ya sikukuu.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment