Bw. Moshingi akisalimiana na wana VICOBA
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
BENKI ya Posta Tanzania, TPB, imekabidhimkopo wa jumla ya shilingi milioni 244,500,000/- kwa vikundi vinane vya wajasiriamali.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Desemba 23, 2015 kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, (NEEC).
Akizungumza kwenye makabidhiano hayo, Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Bw. Sabasaba Moshingi alisema, fedha hizo ni awamu ya kwanza ya benki kutoa mikopo hiyo yenye masharti nafuu, baada ya kutiliana saini na NEEC Julai mwaka huu wa 2015, ambapo baraza hilo litadhamini vikundi hivyo ambavyo vitapaswa kwanza kufungua akaunti TPB kabla ya kupatiwa mikopo hiyo ambayo jumla ya shilingi bilioni 2 zimetengwa kwa dhumuni hilo.

No comments:
Post a Comment