Rais Alpha Conde wa Guinea amemteua waziri mkuu mpya, baada ya kuapishwa mapema wiki hii kwa muhula mpya wa miaka mitano wenye utata. Mamady Youla, mchumi ambaye amefanya kazi serikalini na kwenye sekta binafsi, anachukuwa nafasi ya Mohamed Said Fofana, aliyejiuzulu Jumatano iliyopita. Youla, mwenye umri wa miaka 54, amepewa jukumu la kuunda serikali itakayojikita kwenye uundaji wa nafasi mpya za ajira, kuinua maisha ya vijana na kuuimarisha uchumi wa taifa hilo la kipato cha chini. Conde, mwenye umri wa miaka 77, alichaguliwa kwenye uchaguzi wenye utata hapo mwezi Oktoba na akaapishwa Jumatatu iliyopita. Mwezi uliopita, mahakama ya katiba ilitupilia mbali madai ya wapinzani kwamba ushindi wa asilimia 57.8 wa kiongozi huyo ulikuwa wa wizi.
No comments:
Post a Comment