TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, December 26, 2015

Israel yauwa Wapalestina wawili

Vikosi vya Israel vimewauwa Wapalestina wawili kwenye mashambulizi mawili tafauti hapo jana. Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 56 alipigwa risasi na kuuawa wakati akijaribu kumponda mwanajeshi kwa gari katika kituo cha ukaguzi cha Huwara, Ukingo wa Magharibi. Masaa kadhaa kabla ya hapo, polisi mjini Jerusalem walimpiga risasi na kumuua kijana mmoja wa Kipalestina katika eneo la Mji Mkongwe, wanayesema alitoa kisu wakati  wa kukaguliwa. Kwa mujibu wa vyanzo vya upande wa Wapalestina, maafisa wa polisi wa Israel walirusha mabomu ya machozi na risasi za mpira dhidi ya waandamanaji wapatao 150, ambapo watu 20 walijeruhiwa. Tangu kuanza kwa vuguvugu jipya la maandamano ya mitaani hapo mwezi Oktoba, vikosi vya Israel vimeshawauwa zaidi ya Wapalestina 130, huku Waisraili 18 wakipoteza maisha kwa kushambuliwa kwa visu.

No comments:

Post a Comment