TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, December 21, 2015

WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM) WAHAMASISHA UTALII WA NDANI KWA VITENDO


Mnyama Ngiri akiwa amejipumzisha kwenye tope kama alivyokutwa na kamera yetu

Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) wamefanya ziara ya siku mbili ya kitalii katika hifadhi ya taifa ya Saadani pamoja na sehemu ya kihistoria ya Kaole iliyopo Bagamoyo ikiwa ni sehemu ya kujifunza pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani.

Wanafunzi hao kutoka katika "Collage" tofauti tofauti ikiwemo utalii , uchumi na biashara waliofanya ziara hiyo ikiwa chini ya mwamvuli wa University of Dar es Salaam Tourism Association (DUTA) ,walipata fursa ya kujifunza na kushuhudia wanyama pori pamoja na sehemu ya kihistoria ya Kaole na kuhamasisha jamii hasa ya wasomi kuwa mfano wa kuigwa kwa kuzuru hifadhi pamoja na makumbusho ili kuhimiza utalii wa ndani. 
Hii ni tabia ya kipekee ya ngiri ambapo hula nyasi akiwa amepiga mfano wa magoti kwa kukunja miguu ya mbele .
Waterbucks kama wanavyojulikana wakiwa miongoni mwa wanyama walioonekana wakati wa ziara hiyo.Akizungumzia ziara hiyo aliyekuwa kiongozi wa msafara huo ambaye ni mwanafunzi wa kozi ya utalii ,Gabriel Lyimo alisema huu ni muendelezo wa ziara ambazo wamekuwa wakizifanya kama sehemu ya kujifunza pamoja na kuhamasisha watanzania na hasa wanafunzi pamoja na wasomi kujenga utamaduni wa kukuza pato la taifa kwa kufanya utalii wa ndani na sio kuona kama ni jukumu la wageni
.
Picha ya pamoja 

Sambamba na hilo wanafunzi hao walipata fursa ya kuweka kambi pembezoni mwa mwambao wa bahari ya hindi na kutumia fursa hiyo kupata upepo mwanana , kupumzika na kuogelea.
Saadani National Park ni Hifadhi ya Taifa ya 13 ya Tanzania yenye eneo la 1,062 km za mraba ambapo watalii wanaweza kuona wanyama pamoja mwambao Bahari ya Hindi.Mbuga hii ilikuwa rasmi katika gazeti la serikali mwaka 2005, Saadani National Park ni hifadhi pekee nchini Tanzania ambayo imepakana na bahari ya Hindi.
Mtembezi na muelekezi katika hifadhi ya Saadani Bw.Mollel akifafanua jambo wakati wa ziara ndani ya hifadhi .
Baadhi ya wanafunzi wakisikiliza historia kuhusu mji huu wa Saadani huku toka kwa mwenyeji na mkongwe wa eneo hilo mzee Mlelwa (mwenye shati la kijani) wakati wa jioni 
.
Mambo ya Msosi: baadhi ya wanafunzi wakiwa katika harakati za kuchoma kitoweo kwa ajili ya mlo wa usiku .
Hakika anapendeza!! 
wanafunzi hao wakiwa karibu na eneo ambalo maji kutoka mto wami yanakutana na maji ya bahari ya hindi 
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakichagua shanga na vito vya asili walipozuru Kaole Mamba Ranch iliyopo Bagamoyo 
Moja kati ya mamba wanaopatikana katika eneo la Kaole Mamba Ranch 
Kwa umakini na huku wakipewa fursa ya kuuliza maswali , wakisikilza historia ya eneo la Kaole na mfululizo wa matukio ya kihistoria kutoka kwa mtaalamu wa historia Bw.Ramadhani
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa mbele ya msikiti wa kwanza uliojengwa katika pwani ya Afrika ya mashariki 
Kulingana na historia ya eneo hili ,inasemekana kuwa mbuyu huu umeishi zaidi ya miaka mia tano na wengi wamekuwa wakiamini kuuzunguka mbuyu huu (kutoka upande wa kushoto kwenda kulia) kunaweza kumuongezea mtu miaka ya kuishi 

No comments:

Post a Comment