Mkurugenzi wa Masoko Limited, Bwana Constantine Majavika (kushoto) akionyesha aina za mifuko ijulikanayo kama Envirobags mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) itakayoweza kusaidia kuondokana na tatizo la utupaji taka ovyo nchini. Kulia ni Mkurugenzi Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Ofisi ya Mazingira, Bwana Julius Ningu akiangalia moja ya mifuko ya Envirobags.
Mkurugenzi Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Ofisi ya Mazingira, Bwana Julius Ningu (kulia) akiwapongeza Vijana wa Shule ya International School of Tanganyika (IST) mbele ya Waandishi wa Habari leo 23 Desemba, 2015 katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) kwa ubunifu wa kutengeneza mifuko kwa ajili ya utunza mazingira dhidi ya utupaji taka ovyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Limited, Bwana Constantine Majavika, anaemfuatia ni Alyanz Nasser na mwenzie Shilen Dauda (wa pili kulia).
Mkurugenzi wa Masoko Limited, Bwana Constantine Majavika (kushoto) akifafanua kuhusu ubunifu uliofanywa na vijana wa Shule ya International School of Tanganyika (IST) mbele ya Waandishi wa
Habari leo 23 Desemba, 2015 katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) wa kutengeneza mifuko kwa ajili ya utunza mazingira dhidi ya utupaji taka ovyo. Kushoto ni Shilen Dauda na katikati ni Alyanz Nasser.
Kijana wa Shule ya International School of Tanganyika Alyanz Nasser (katikati) aieleza dumuni lao kubwa la kubuni mifuko ya Envirobags inayowezesha kuepukana na utupaji taka ovyo nchini wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo 23 Desemba, 2015 katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). Kulia ni Mkurugenzi Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Ofisi ya Mazingira, Bwana Julius Ningu, kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Limited, Bwana Constantine Majavika na wa pili kulia ni kijana wa shule hiyo Shilen Dauda.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa ya ubunifu uliofanywa na Vijana wa Shule ya International School of Tanganyika (IST) leo 23 Desemba, 2015 katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Benedict Liwenga) .
………………………………………………………
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa ya ubunifu uliofanywa na Vijana wa Shule ya International School of Tanganyika (IST) leo 23 Desemba, 2015 katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Benedict Liwenga) .
………………………………………………………
No comments:
Post a Comment