TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, December 23, 2015

MAKALLA AFANYA UZINDUZI WA MRADI WA MAJI WENYE THAMANI YA SH MILIONI 343


Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Amos Makalla mwenye miwani akizindua huduma ya maji katika kijiji cha Mabogini, mkoani Kilimanjaro wenye thamani ya Sh Milioni 343.Mradi wa maji wa sh Milioni 343 wazinduliwa kijiji cha Mabogini, RC Makalla ataka vyanzo vya maji vitunzwe


Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

ZAIDI ya wananchi 3000 wa kijiji cha Mabogini, kitongoji cha Shabaha, mkoani Kilimanjaro, watanufaika na huduma ya maji safi na salama, baada ya kupelekewa mradi wenye thamani ya Sh Milioni 343. Mradi huo uliozinduliwa leo na Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Amos Makalla, umesimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi Moshi (MUASA), ukiwa na lengo la kuwapatia huduma bora ya maji wakazi katika kijiji hicho.
Akizungumza katika uzinduzi huo, RC Makalla aliwataka wananchi kutunza mazingira na kulinda vyanzo vya maji, bila kusahau upandaji wa miti ili wasiharibu vyanzo vya maji. Alisema bila hivyo hali ya maji katika maeneo hayo itakuwa ngumu, hivyo kuna kila sababu ya wananchi hao kuielewa na kuiabudu sera ya utunzaji wa mazingira na upandaji wa miti katika maeneo yao. “Naomba wananchi tulinde miundo mbinu ya maji ili kuhakikisha kwamba miradi ya maji inakuwa endelevu katika maeneo yetu tunayoishi, maana maji ni uhai. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Amos Makalla akimtwishwa ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Mabogini baada ya uzinduzi wa mradi maji katika eneo hilo.  Mazungumzo yanaendelea katika uzinduzi huo wa maji. RC Kilimanjaro Amos Makalla akifungua maji kama ishara ya kuzindua rasmi mradi huo. RC Kilimanjaro Amos Makalla wa nne kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali mkoani Kilimanjaro na watendaji wa MUASA.“Tunaamini tukiamua kwa pamoja kufuata maelekezo ya wataalaamu juu ya utunzaji wa mazingira tutaishi vizuri na huduma ya maji itapatikana kwa urahisi,” alisema RC Makalla. Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Amos Makalla, amekabidhi hundi yenye thamani ya Sh Milioni 100 kwa vikundi 45 kwa Halmashauri ya Moshi, huku vikundi hivyo vikiwa ni 39 vya akina mama na 6 kwa vijana. Fedha hizo ni utekelezaji wa maelekezo ya serikali kwa Halmashauri kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kutoa mikopo kwa akina mama na vijana.RC Makalla ni miongoni mwa viongozi wa serikali wanaokwenda na kasi ya Hapa Kazi Tu inayoendeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli, akisimamia na kuzunguuka katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kufanikisha maendeleo ya wananchi wake.

No comments:

Post a Comment