TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, December 25, 2015

WANAKIJIJI WACHARUKA WAMTAKA MKURUGENZI MBOGWE AKAZOE TAKA ZILIZOTUPWA KIJIJINI KWAO SIKU YA USAFI DECEMBER 9

UCHAFU ULIOZOLEWA KATIKA KATA YA MASUMBWE NA KUTUPWA KATIKA MAKAZI YA WATU KATIKA KIJIJI CHA SHENDA.Wanachi wa kijiji cha Shenda katika kata ya Masumbwe wilayani Mbogwe mkoani Geita Wameitaka ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya Mbogwe kuziondoa takataka zilizowekwa kijijini kwao kufuatia zoezi la usafi la December 9 Lililofanyika nchi nzima.Wakiongea na waandishi wa habari za mtandaoni wananchi hao wanakijiji hao wamesema kuwa wanashangazwa na kitendo cha halmashauri ya wilaya kutuma takataka katika kijiji chao licha ya kwamba hakuna dampo la uchafu eneo hilo.Wameongeza kuwa taka hizo ni hatari kwa afya zao kwani zimetupwa karibu na eneo la shule ya msingi,Makazi ya watu na vibanda vya mama ntilie hali inayozua hofu ya kuzuka kwa magonjwa ya mripuko kwani taka hizo zimeanza kuoza na kusambaa katika makazi ya watu kipindi hiki cha masika.Sambamba na hayo wameshangazwa na maamuzi ya ofisi ya mkurugenzi kutupa taka hizo katika kijiji chao licha ya kuwa yapo maeneo mengi ya wazi ambayo yangeweza kutumika kutupa taka hizo ambazo kwa sasa zimekuwa kero katika kijiji chao hasa kutoa harufu mbaya na funza.Kwa mujibu wa kaimu mtendaji wa kijiji cha Shenda Joseph Jaseda amesema sehemu zilizotupwa taka hizo ni makazi ya watu na kwamba walipouliza kuhusu hatua hiyo waliambiwa kuwa gari la kuzoa taka liliharibika sehemu hiyo na ndipo walipoamua kutupa taka hizo.Kwa upande wake diwani wa kata ya Masumbwe Shimo Kiyuyu amesema kuwa alifikisha malalamiko ya wananchi kwa mkurugenzi na Mkurugenzi akatoa gari ili uchafu uzolewe lakini juhudi hizo ziligonga mwamba kutokana na gari hiyo kwenda eneo la uchafu bila wazoaji wa taka hizo.Kwa upande wake afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya MbogweEdward Razalo amekiri uchafu huo kutupwa katika maeneo hayo na kuongeza kuwa baada ya wananchi kulalamika walienda kuweka dawa ya kuwa wadudu katika taka hizo na kwamba hawajaziamisha kutokana na taka hizo kutokuwa na madhara kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment