Msemaji wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bi. Riziki Abraham (kushoto) akiongea na waandishi wa Habari kuhusu Umuhimu wa Utunzaji Nyaraka kwa waombaji kazi katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Jijini Dar es Salaam, kulia ni Naibu katibu anayehusika na Udhibiti na Ubora Bw. Humphrey Mniachi .
Naibu Katibu Kutoka Sekretarieti ya Ajira anayesimamia Idara ya Udhibiti na Ubora Bw.Humphrey Mniachi akitoa Ufafanuzi wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari kuelezea Umuhimu wa Utunzaji Nyaraka kwa waombaji kazi kushoto ni Msemaji wa Sekretarieti ya Ajira Bi. Riziki Abraham.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi. Riziki Abraham (Kushoto) akionyesha vipeperushi kwa waandishi wa Habari vinavyoelezea utekelezaji wa Mchakato wa Ajira Serikalini kulia ni Naibu katibu Ofisi hiyo anayehusika na Udhibiti na Ubora Bw. Humphrey Mniachi .
Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia Mkutano
huo. Picha na Fatma Salum)
……………………………………………………………………………………….
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma katika kutekeleza jukumu lake la uendeshaji wa mchakato wa Ajira serikalini imekuwa ikikumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya matukio ya upotevu wa vyeti vya kitaaluma na nyaraka nyingine za msingi kutoka kwa waombaji kazi.
Tunaendelea kusisitiza na kuwakumbusha wadau wetu kwamba miongoni vya vigezo vya msingi vinavyotumiwa na Sekretarieti ya Ajira pamoja na Waajiri ili kujua kama muhusika anayeomba kazi ana sifa na vigezo vinavyotakiwa katika nafasi husika ni pamoja na kuwa na
vyeti vya kuhitimu taaluma husika.
No comments:
Post a Comment