Watu wapatao 140,000 wameokolewa kufuatia mafuriko makubwa katika mataifa manne ya Amerika ya Kusini. Paraguay ndiyo nchi iliyoathirika vibaya na mafuriko hayo, ambapo hali ya hatari imetangazwa. Maafisa wanasema wengi wa watu waliopoteza makaazi yao ni familia masikini zinazoishi kandoni mwa Mto Paraguay, karibu na mji mkuu, Asuncion. Maelfu ya watu nchini Uruguay, Brazil na Argentina pia wamekimbia makaazi yao. Watabiri wa hali ya hewa wanasema kumekuwa na mvua kali za El Nino na zisizo za kawaida katika msimu huu wa kaskazi. Kwengineko, barani Ulaya mvua kubwa imesababisha mafuriko kaskazini mwa kisiwa cha England. Mito mikubwa katika miji ya Manchester na Leeds imefurika na wakaazi kwenye kaunti za Lancashire na West Yorkshire wamehamishwa. Jeshi la Uingereza limeitwa kusaidia uokozi.
No comments:
Post a Comment