TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, November 6, 2014

Upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Kawanzige wasababisha wanafunzi kukaa chini

unnamed
Wanafunzi wakiwa wamekaa chini darasani kwa kukosa madawati wakati halmashauri ya mji inazunguukwa na mistu kibao na wanachi wanashindwa kutengeneza madawati ni abu kwan wazazi kukka chini watoto.
Walimu na  wazazi wanafunzi wanaokaa chini shule ya msingi kawanzige halmashauri ya mji wa Mpanda wakimsikiliza mkuu wa Wilaya alipokuwa akiwaeleza umuhimu wa kuwahudumia watoto ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanapata elimu bora kwa kukaa kwenye dawati haina maana.
unnamed3
Mkuu wa wilaya akiwa na wanafunzi wa darasa la tatu na tano kwenye chumba kimoja cha darasani kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa wanalazimika kutumia chumba kimoja kusomea kwa wakati mmoja hali ambayo haiendani na taratibu za  miongozo na sera ya  elimu madarasa tofauti kusomea darasa moja tena kwa wakati mmoja. (Picha na Kibada Kibada -Katavi)
………………………………………………………………………………………..
Na Kibada Kibada –Katavi.
Upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Kawanzige Halmashauri ya Mji wa Mpanda umechangia wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili kukaa chini na wengine wa darasa la tatu na la tano kukaa darasa na kuwapa wakati mgumu walimu kufundisha madarasa mawili tofauti.
Hayo yalibainika wakati Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima alipofanya ziara ya kushitukiza kutembelea shule hiyo na kukuatana sakata hilo la watoto wa shule ya Msingi Kawanzige kukaa chumba kimoaja madarasa mawili tofauti.
Akizungumzia mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mwalimu Mkuu Msaidizi Masele Kibona na mwalimu  wa Taaluma katika shule hiyo walieleza kuwa shule hiyo yenye wananfunzi wapatao 484 ina mikondo 12 kuanzia darasa la (I-Vii)  inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa hali inayofanya wanafunzi wakae chini na wengine wakae chumba kimoja  madarasa tofauti.
Mwalimu Kibona alieleza kuwa shule hiyo ina vymba vine vya madarasa  na upungufu ni vyumba vine , na hakuna nyumba ya mwalimu hata mmoja  katika shule hiyo.
Mbali ya upungufu huo wa vyumba vya madarsa pia upo upungufu mkubwa wa matundu ya vyuo ambapo shule inahitaji matundu ya vyoo 14 lakini yaliyopo ni matundu matatu tu amabyo hayatoshelezi mahitaji kwa wanafunzi hao.
Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Wilaya amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda  Seleman Lukanga aliyewakilishwa na Kaimu  Mkurugenzi ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mji wa Mpanda Zena Kapama aliagizwa kuhakikisha wanashughulikia changamoto ya upungufu wa madarasa katika shule hiyo.
Akatakiwa kuangalia katika bajeti yao kuona namna ya kushughulikia changamoto inayoikabili shule hyo ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wananchi kuchangia katika ufyatuaji wa tofali,kusomba mchanga na serikali inachangia vifaa ya ujenzi vya dukani mabati,nondo na misumari na rangi nakadhalika hivyo wajibu wa wananchi kuhakikisha wanachangia katika ujenzi wa shule kwa kuwa shule ni mali ya wananchi.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima ameutupia lawama uongozi wa  Halmashauri ya Mji wa Mpanda kwa kushindwa kuwatembelea wananchi na kubaini changamoto zinazowakabili badala yake wanakaa ofisini bila kuwatembelea wananchi na kubaini changamoto wanazokabiliana nazo.
Alilazimika kutoa kauli hizo baada ya kubaini kuwa zipo kero nyingi kwa wananchi ambazo zingeweza kupatiwa ufumbuzi na watalaam iwapo wangekuwa wanawatembelea wananchi na kubainichangamoto zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi kuliko kusubiri mpaka viongozi wa ngazi ya wilaya au Mkoa kufanya ziara ya kukagua maendeleo.
Viongozi kama Mkuu wa Wilaya, Mkoa na Viongozi wa Kitaifa ambapo wananchi wanakuwa na kero ambazo zingeweza kupatiwa ufumbuzi na watalaamu na siyo kusubiri viongozi wa ngazi za juu, maana kero zinakuwa nyingi bila kupatiwa majibu.
Kufuatia hali hiyo amewaagiza watendaji wote kutoka maofisini na kufanya ziara ya kutembelea vijijini na kupata changamoto na kuzifanyia kazi ili kuzipatia ufumbuzi ili kuwaondolea kero wananchi na kuwaletea maendeleo.

No comments:

Post a Comment