TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, November 2, 2014

UJENZI WA UWANJA MPYA WA MICHEZO YA UMMA JIJINI DAR-ES-SALAAM WASHEREHEKEWA SYMBION POWER & SUNDERLAND AFC

unnamed5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akiwaonyesha jezi yenye jina la Tanzania kwa wageni waalikwa pamoja na wananchi waliohudhuria hafla ya kutoa Kibali kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Umma uliopewa jina la Rais Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park. Tukio hilo limefanyika leo 1 Novemba, 2014 eneo la Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.unnamed4Mkurugenzi wa Biashara wa Chama cha Michezo cha Sunderland, Bi. Gary Hutchinson akimkabidhi zawadi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya kutoa Kibali chake kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Umma uliopewa jina la Rais Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park. Tukio hilo limefanyika leo 1 Novemba, 2014 eneo la Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.unnamed3Mkurugenzi wa Biashara wa Chama cha Michezo cha Sunderland, Bi. Gary Hutchinson akitoa maelezo machache kabla ya kumkaribisha rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete kwa ajili ya kutoa hotuba pamoja na kutoa Kibali chake kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Umma uliopewa jina la Rais Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park. Tukio hilo limefanyika leo 1 Novemba, 2014 eneo la Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.unnamed2Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Symbion Bwana Paul Hinks akitoa maelezo yake juu ya ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Umma uliopewa jina la Rais Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park. Tukio hilo limefanyika leo 1 Novemba, 2014 eneo la Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.unnamed1Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mushi akitoa maelezo machache kabla ya kumkaribisha rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete kwa ajili ya kutoa hotuba pamoja na kutoa Kibali chake kwa Chuo cha Michezo cha Sunderland kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Umma uliopewa jina la Rais Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park. Tukio hilo limefanyika leo 1 Novemba, 2014 eneo la Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
01 Novemba, 2014.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Jakaya Kikwete amevitaka Vilabu vya mpira wa miguu nchini kuwekeza katika timu za vijana wadogo walio chini ya umri wa miaka 18 ili viweze kuwa na mafanikio ndani na nje ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa na Rais Prof. Kikwete leo jijini Dar es saam alipokuwa akizindua ujenzi wa kituo cha michezo cha vijana wadogo waliochini ya miaka 18 kinachojengwa nchini eneo la Kidongo Chekundu manispaa ya Ilala.
“Katika nchi yetu, timu ya soka ya taifa haifanyi vizuri na michezo mingine nayo vivyo hivyo, vilabu mbalimbali vya michezo navyo havifanyi vizuri katika michezo yao ya ndani na nje” alisema Prof. Kikwete.
Prof. Kikwete aliendelea kusema “Kiini cha timu yetu ya soka ya taifa na vilabu vyetu kutokufanya vizuri katika mashindano, haviwekezi katika vijana wadogo”.
Katika kufanikisha adhima ya kuwa vilabu na timu ya taifa ya mpira wa miguu kuwa na mafanikio, Rais Kikwete amewaagiza viongozi Shirikisho la Mpira wa Miguu na wa vilabu vya mpira wa miguu nchini watekeleze majukumu yao ipasavyo ili soka la Tanzania liwe la mafanikio kwa wachezaji mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Aidha, amelishauri Shirikisho la mpira wa miguu nchini liweke utaratibu ambao utailazimu kila timu kuwa na timu ya vijana wadogo kama ilivyo katika mataifa mengine duniani ambapo kwa mataifa hayo, suala la kuwa na timu ya vijana wadogo na uwanja wao sio la hiyari.
Kwa upande wake Kurugenzi Mtendaji wa Timu ya soka ya Sanderland ya nchini Uingereza ambao ndiyo watakaotoa wataalamu wa michezo watakaofundisha katika kituo hicho Bi. Margaret Byrne amesema kuwa kituo hicho kitakuwa na uwanja wa mpira wa miguu wa kisasa wenye ukubwa wa mita 100×60, viwanja viwili vya mpira wa kikapu, sehemu ya kuegesha magari 20 na kituo cha daladala, kiwanja cha kuchezea watoto.
 Bi. Margaret alisisitiza kwa ndani ya kituo hicho,  kutakuwa pia na jingo la utawala, vyumba vine vya wachezaji kubadilishia nguo vikiwa na vyoo na bafu, vyumba viwili vya wafanyakazi pamoja na chumba cha chakula ambacho kitaendana na madhari ya kituo hicho.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Symbion ya nchini Marekani Paul Hinks amesema kuwa kampuni yake iko mstari wa mbele na wataendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo kukuza sekta ya michezo nchini kwa kujenga kituo cha soka kwa vijana wadogo.
Ujenzi wa kituo hicho ulizinduliwa na Rais Kikwete kwa kupanda mti wa mnazi ikiwa ni alama ya kuashiria kuanza ujenzi huo rasmi ambao unatarajiwa kukamilika mapema mwakani 2015 ambapo alibainisha kuwa kuwa siku ya Oktoba Mosi mwaka huu, imekuwa ni siku ya aina ya kipekee ambayo inafungua ukurasa mpya katika historia ya michezo nchini.

No comments:

Post a Comment