TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, November 2, 2014

Kila la Kheri Spika Makinda, Urais Bunge la SADC

unnamed
Na Owen Mwandumbya, Victoria Falls, Zimbabwe
 
Mkutano wa 36 wa Jukwaa la Mabunge ya Nchi wanachama wa SADC (SADC PF) ulioanza wiki hii mjini Victoria Falls nchini Zimbabwe na unatarajiwa kumalizika tarehe 3 Novemba, 2014, ikiwa ni baada ya kukamilika kwa ajenda ya Mkutano huu pamoja na kufanyika kwa uchaguzi wa Rais wa chama hicho atakayeongoza jukwaa hilo kwa miaka miwili ijayo.
 
Kauli mbiu ya mkutano huu ni “Bunge la kikanda la SADC – Wakati ni huu”  ama kwa lugha ya kimombo inasema “ SADC Regional Parliament – the Future is Now”.
 
Maneno yaliyo katika kauli mbiu ya Mkutano huu yamebeba ujumbe mzito sana wa Mabunge ya Nchi za SADC ikiwa ni dhamira ya dhati waliyokuwa nayo wanachama hawa ya kuundwa kwa Bunge la kikanda litakalokuwa na nguvu si tu ya kuzisimamia Serikali za Nchi Wanachama bali pia kuwa na uhalali wa kuhakikisha kuwa maamuzi na hata mikataba mbalimbali itakayofikiwa na chombo hiki katika ukanda huu vinatekelezwa katika nchi wanachama.
 
Pamoja na kwamba yapo mengi yaliyojadiliwa katika Mkutano huu wa Umoja wa Mabunge ya SADC hapa Zimbabwe, muhimu limekuwa ni uchaguzi wa Rais wa Jukwaa hili ambaye ataongoza jitihada za kufanikisha malengo ya chama hiki ya kufikia kuwa Bunge kamili ndani ya Miaka miwili ijayo yanafanikiwa.
 
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda amekuwa akipigiwa chapuo na Wajumbe wengi wa Mkutano ili aweze kukamata usukani wa kukiongoza chama hiki kwa miaka miwili ijayo baada ya Rais wa sasa ambaye pia ni Spika wa Mauritius Mhe. Abdool Razack Mahomed Ameen Peeroo, kumaliza muda wake. Kutokana na uungwaji mkono mkubwa alionao Mhe. Makinda ameibuka kuwa mgombea pekee na hivyo ni dhahiri atapitishwa na kukabidhiwa jukumu la kuongoza Jukwaa hili.
Msukumo wa Wajumbe wa Mkutano huu wa 36 kutaka Spika Makinda aweze kuongoza Bunge hili unatokana na heshima  na ushawishi mkubwa ilivyonayo nchi ya Tanzania katika nchi wanachama wa SADC swala ambalo linafanya wajumbe wengi wa Umoja huu waamini kuwa Mtanzania Makinda atasaidia sana kusukuma masuala ya Jukwaa hili kwa Wakuu wa nchi wanachama, kazi ambayo inahitaji mtu kutoka nchi inayokubalika na yenye sifa za kidemokrasia ya kweli kwa na hivyo kuweza kupenyeza na kufanikisha matakwa ya Bunge hili.
 
Kukubalika kwa Tanzania katika Ukanda wa huu wa Afrika Kusini na chapuo anayopigiwa Makinda ya kuongoza Bunge la SADC vinatokana na historia iliyoandikwa na Tanzania kupitia harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 1960. Kuanzia wakati huo nchi ya Tanzania chini ya Uongozi wa hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, iliongoza mapambano ya ukombozi Barani Afrika na kutoa msaada mkubwa kwa Vyama vya ukombozi vya nchi za Kusini mwa Afrika kama vile, Zimbabwe (ZANU), Afrika Kusini (ANC na PAC), Namibia (SWAPO), Angola (MPLA) na Msumbiji (Frelimo).
Continue reading →

No comments:

Post a Comment