TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, November 6, 2014

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima awapa changamoto watumishi wa umma

unnamed
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Panza Mwamlima akiongea na uongozi wa Kata ya Kakese katika kikao chake na uongozi huo kuzungumzia shughuli za maendeleo katika kata hiyo,kushoto kwa mkuu wa Wilaya ni Afisa mtendaji wa Kata ya Kakese Rebeni Kasomo aliyeshika kichwa,kulia kwa mkuu wa wilaya  ni Kaimu Mkurugenzi wa Mji Zena Kapama na mwisho ni Kaimu Afisa Katibu Tawala wilaya Reginal Mhango.
…………………………………………………………………
Na Kiada  Kibada- Katavi.
 Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima  amewapa changamoto watumishi wa umma kuwa wabunifu kwa kubuni mbinu zitakazo wasaidia kupambana na changamoto za kimaisha  kukabiliana na mazingira wanayofanyia kazi.
 Changamoto za kimazingira katika utendaji wa kazi kukikabiliana nazo  na zitakufanya kuwa mbunifu na kuweza kukabiliana nazo na  mazingira hayo ambapo utapata fikra mpya na  akili itakayo saidia kuwaletea Maendeleo wananchi wanaowatumikia na wewe mwenyewe.
Mkuu huyo wa wilaya alitoa  changamoto hiyo wakati akizungumza na watumishi  wa Idara ya Elimu, Afya, kilimo na mifugo Utawala pamoja na vikundi vya kuweka na kukopa wa Kijiji cha kawanzinge,kakese na mbugani wa kata ya Kakese   kwa nyakati tofauti alipokutana nao katika ziara ya kutembelea,kukagua na kuhimiza shughuli za maendeleo Kata ya Kakese Halmashauri ya Mji wa Mpanda kisha kuzungumza na watumishi hao.
Mwamlima akiwa katika Kijiji cha Kawanzige alikutana na walimu,watumishi wa Idara ya Kilimo, Mifugo na utawala ambapo katika mazungumzo yao alipokea changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi hao wa umma katika mazingira yao ya Kazi ya kila siku hasa kwa wale walioko nje ya makao makuu ya Halmashauri.
Wakiongea katika kikao hicho kwa nyakati tofauti kwenye ofisi ya Walimu Shule ya Msingi Kawazinge  watumishi  hao walimweleza Mkuu wa Wilaya kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiutendaji katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku kulingana na mazingira magumu ya kiutendaji wanayotendea kazi.
Baadhi ya changamoto walizibainisha kuwa ni kuwa kwa upande wa walimu ni upungufu wa Madawati,Nyumba za Walimu,upungufu wa vitabu vya kiada na ziada,huduma ya maji safi na salama pamoja na kutosikilizwa na wakuu wao wa elimu pale wanapoenda kufuatilia stahili zao mbalimbali kwenye ofisi wanapewa majibu yasiyostahili.
Kwa upande wake  Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kawanzige Koletha Nyambi alieleza kuwa changamoto katika kijiji hicho zipo za aina mbalimbali kama walivyoeleza watumishi wenzake ambapo kubwa ni ukosefu wa nyumba wa watumishi.
Nyambi alitaja changamoto nyingine kuwa ni upungufu wa vyumba vya madarasa,madawati na huduma ya maji.akaomba serikali kusaidia kuondoa changamoto hicho hasa kuwajengea nyumba watumishi ili waweze kuishi jirani na vituo vya kazi kuweza kuwahudumia wananchi na kuwaletea maendeleo.
Amesema Mtumishi wa umma ambaye ni mtalaam au kiongozi anapokuwa  eneo la kiutendaji akiwahudumia wananchi hatakiwa kulalamikia mazingira magumu bali anakabilaiana na changamoto hizon na kutafuta njia ya kutatua changamoto hizo kulingana  na Mazingira anayoishi nayo atumikie kila rasilimali zilizopo kuwasaidia wananchi kuleta maendeleao.
Awali Afisa Mtendaji wa Kata ya Kakese Reuben Kasomo alimweleza mkuu wa Wilaya kuwa changamoto mbalimbali zinazoikabili Kata yake ikiwa ni pamoja na upungufu wa watumishi hasa katika sekta ya utwala ,walimu,nyumba za kuishi watumishi , vyumba vya madarasa kwa kwa shule zilizoko kwenye kata yake pamoja na upungufu wa vitabu vya ziada na kiada,
Mbali ya hilo walieleza hali ya maandalizi ya upatikaji wa pembejeo za kilimo kwa kuwa msimu wa kilimo umekaribia kuanza lakini hadi sasa hawakulima hawajui hatma yao ya kupata pembejeo watazipataje kwa kuwa hawajaelezwa lolote kulingana na hali hiyo.

No comments:

Post a Comment