TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, November 7, 2014

DANGOTE AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA KIWANDA CHAKE KIKUBWA CHA SARUJI MTWARA

Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko Dangote (kulia) mfanyabiashara maarufu kutoka Nigeria, akiteremka kwenye ndege alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara, kwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda kikubwa cha saruji kinachojengwa mkoani humo.,
 Dangote akilakiwa na Mwakilishi Mkazi wa kampuni hiyo nchini, Esther Baruti (kushoto)
 Dangote akisalimiana na Balozi Mdogo wa Nigeria nchini, Adamu Mussa
 Dangote akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa kampuni ya Dangote nchini, Esther Baruti na Balozi Mdogo wa Nigeria nchini, Adamu Mussa
Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko Dangote (kulia) mfanyabiashara maarufu kutoka Nigeria, akilakiwa na Mwakilishi Mkazi wa kampuni hiyo nchini, Esther Baruti (katikati) pamoja na Balozi Mdogo  wa Nigeria nchini, Adamu Mussa alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho, mkoani Mtwara
Balozi Mdogo wa Nigeria, Adamu Mussa akizungumza na Dangote Uwanja wa Ndege wa Mtwara
Dangote akisalimiana na wafanyakazi wa kampuni inayojenga kiwanda hicho ya Dil & Sinoma, baada ya kuwasili eneo la ujenzi wa kiwanda.
Dangote akiwa katika kikao na baadhi ya wahandisi na mafundi wa wanaojenga kiwanda hicho
Alhaji Aliko Dangote akitabasamu baada ya kuwasili eneo la ujenzi wa kiwanda hicho
Dangote akitumia gari kukagua ujenzi wa kiwanda hicho
Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko Dangote akiwa kwenye gari huku akipata maelezo ya ujenzi wa kiwanda hicho kutoka kwa mafundi na wahandisi wa kampuni ya Dil & Sinoma inayojenga kiwanda hicho kitakachokuwa cha tatu kwa ukubwa Afrika.
Msafara wa Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Groupof Industries), Alhaji Aliko Dangote, ukikagua ujenzi wa kiwanda hicho kinachotarajiwakuanza kazi Aprili, mwakani. Awamu ya kwanza ya kiwanda hicho ujenzi wake ukikamilika kitakuwa kinazalisha tani 6000 kwa siku.
Dangote akiangalia moja ya majengo yanayoendelea kujengwa kiwandani hapo
Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko Dangote (kulia) mfanyabiashara maarufu kutoka Nigeria, akizungumza na Meneja Mkuu wa Kiwanda kikubwa cha cha saruji cha Dangote Tanzania, Daljit Singh (katikati), alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho,mkoani Mtwara. Kushoto ni Kenneth Kasigila ambaye ni Msaidizi Maalumu wa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, iliyopewa fursa ya kwanza kujenga benki karibu na kiwanda hicho.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, ambaye ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Ponsiano Nyami (kushoto), akizungumza na Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko Dangote, muda mfupi kabla ya mfanyabiashara huyo kuondoka Uwanja wa Ndege wa Mtwara jana, baada ya kukagua ujenzi wa kiwanda chake.
Dangote akisindikizwa kwenda kupanda ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara
Dongote akiagana na Kaimu Mkuu wa Mkoawa Mtwara, Ponsiano Nyami
Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko Dangote, akiaga alipokuwa akiondoka na ndege yake kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara jana. Alitumia takribani saa mbili kuwepo nchini, baada ya kuwasili asubuhi saa 1:42 na kuondoka saa 3:42 baada ya kupata maelezo ya ujenzi na kukagua kiwanda chake.
 Ndege ikiwa imepaa

No comments:

Post a Comment