TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, November 3, 2014

Zanchick watoa msaada wa chanjo 600,000 kwa wafugaji kuku Zanzibar

Logo-ya-taifa
Mkurugenzi wa Kampuni inayojishughulisha na uboreshaji wa kuku Zanzibar(Zanchick) Bw.Issa Khasim Issa akikabidhi chanjo 600,000 zenye thamani ya Tshs 9,000,000 kwa  Naibu katibu katika kitengo cha kutoa huduma kwa wanyama kutoka Wizara ya Ufugaji na Uvuvi Zanzibar, Dr.Omar Ali Amir kwa  ajili ya kuwalinda kuku na ugonjwa wa Mdondo,  anayeshuhudia kulia Mkurugenzi katika kitengo cha kutoa huduma kwa wanyama kutoka Wizara ya Ufugaji na Uvuvi Zanzibar, Dr.Yusuf Hajj Khamis
………………………………………………………………………………….
Kampuni inayojishughulisha na uboreshaji wa kuku Zanzibar, Zanchick, leo imetoa chanjo 600,000 zilizo na thamani ya Tshs 9,000,000 kwa wafugaji kuku kwa ajili ya kuwalinda kuku wao na ugonjwa wa Mdondo.
Utoaji wa chanjo hizo ulifanyika kwa msaada wa wizara ya Ufugaji na Uvuvi Zanzibar ambao wata ratibu na kusimamia zoezi zima.
Meneja wa Uendeshaji, kutoka Zanchick, Bwana Christopher Kontonasios alisema: “Tunashukuru Wizara ya Ufugaji na Uvuvi kwa kuwa washiriki wakubwa katika kuratibu zoezi hili na tunataraji serikali itazidi kuwasaidia wazalishaji kuku wa kawaida, kwa kuondoa kodi ya kuagiza chakula cha kuku, jambo ambalo litawaruhusu wazalishaji wa kawaida kupata chakula bora cha kuku chenye bei nafuu. Hii ndio njia pekee ya kuwawezesha wakulima wa kawaida kuendeleza ufugaji wa kuku, kwa kiwango cha hali ya juu, na pia kuwaruhusu kukidhi biashara zenye faida.
Mkurugenzi katika kitengo cha kutoa huduma kwa wanyama kutoka Wizara ya Ufugaji na Uvuvi Zanzibar, Dr.Yusuf Hajj Khamis alisema, “Tunafarijika na juhudi za Zanchick katika kuboresha uzalishaji wa kuku Zanzibar, hii ni hatua kubwa kwa wafugaji wa kawaida. Tunatarajia kuongeza juhudi katika kushirikiana kukuza viwango na jitihada za ufugaji kuku kisiwani hapa.”
Kirusi cha ugonjwa wa Mdondo kwa ujumla hakisababishi madhara yoyote kwa afya ya binadamu, lakini kina uwezo wa kuleta maafa makubwa kwa wafugaji wa kawaida, kwa kumaliza kiasi kikubwa cha kuku na hatimaye kuangamiza biashara yao.
Msaada huu mkubwa na muhimu ni katika juhudi za Zanchick kufanya kazi na wafugaji wa kawaida ili kuongeza, kuboresha na kunadi uzalishaji wa kuku Zanzibar.

No comments:

Post a Comment